Msaada: Gas inaisha haraka sana

Msaada: Gas inaisha haraka sana

kajansi

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2012
Posts
485
Reaction score
222
Habari wana jamvi! naomba msaada wa kujuzwa mimi nina familia ya watu 4 matumizi yangu ya gas yananipa wasiwasi! Mtungi wa kg 15 unadumu kwa takribani siku 25! ni avarage ya miezi mitatu sasa! je ni sahihi au kuna tatizo?
Asanteni nawatakieni mwisho wa mwaka mwema.
 
Sio sahihi. Kuna tatizo ama katika matumizi au gesi inavuja taratibu. Huwa unatumia kwa matumizi gani?
 
Ndugu ni mapishi ya nyumbani tu! na mdada wa kazi kama anapika maharagwe utumia mkaa!
 
Ndugu yangu kuna wauzaji uchwara nadhani kuna kamchezo huwa wanafanya. mimi niliponunua mara yakwanza ulikaa 4 months, ulipoisha nikanunua tena ukakaa mwezi mmoja, niliponunua ukakaa 2 months...nimefanya research fupi hawaauzaji wa mtaani kuna mchezo wanafanya. mimi kwasasa nanunulia sheli naona average 2 months kwa hawa wengine 25-30 days.
jaribu kubadilisha unaponunulia utaona mabadiliko, na ukiona hakuna angalia matumizi ya nyumbani sio mazuri..
 
sijaona cha ajabu hapo, kama mnatumia gesi peke yake kwa watu wanne it is fair usage/
 
Ndugu yangu kuna wauzaji uchwara nadhani kuna kamchezo huwa wanafanya. mimi niliponunua mara yakwanza ulikaa 4 months, ulipoisha nikanunua tena ukakaa mwezi mmoja, niliponunua ukakaa 2 months...nimefanya research fupi hawaauzaji wa mtaani kuna mchezo wanafanya. mimi kwasasa nanunulia sheli naona average 2 months kwa hawa wengine 25-30 days.
jaribu kubadilisha unaponunulia utaona mabadiliko, na ukiona hakuna angalia matumizi ya nyumbani sio mazuri..

Asante ndugu kwa ufafanuzi!
 
aangalie na matumizi yake! Kama wana ratiba ya kula makande mara 4 kwa wiki gas itadumu kweli!?!

Angalizo zuri mkuu naomba! check bandiko langu kande napikia mkaa! mara nne mbona chache!
 
kama alivyosema mwenzangu hapo juu ni kweli kuna usanii unafanywa na hawa dealers wa gesi,ukiwa unapimiwa kwanza hakikisha unaona reading za mizani na hakikisha iko zero,kisha utoe uzito wa mtungi wako ambao unakuwa steel-printed kwenye mtungi wako,hapo ndipo uakapojua,,,pia ujaribu kununua kwa dealers wengine,kama tatizo litaendelea nakushauri ukague pipe inayoenda kwenye plates na plates zenyewe ili kuhakikisha kwamba hazivujishi gesi,ikibidi badilisha kabisa...(ili kujua kama ni pipe inavujisha gesi,chukua maji yenye sabuni uparaze kwenye pipe kama kuna mahali imetoboka basi itatoa mapovu,fanya hivyo hivyo kwenye sehemu inapoingia kwenye mdomo wa plates.
cha msingi zaidi pia ukague Gas control valves,hizi hazitengenezeki kirahisi,so itabidi uingie mfukoni....pia kumbuka wakati unatumia sabuni ili kugundua leakage HAKIKISHA JIKO LAKO LIMEZIMWA.
nakutakia kila la kheri
 
Asante sana mkuu mungu akubariki kwa ushauri makini.
 
Asante sana kwa ufafanuzi huo namimi ntafanya huo uchunguzi.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Njoo uniangalizie la nyumbani

kama alivyosema mwenzangu hapo juu ni kweli kuna usanii unafanywa na hawa dealers wa gesi,ukiwa unapimiwa kwanza hakikisha unaona reading za mizani na hakikisha iko zero,kisha utoe uzito wa mtungi wako ambao unakuwa steel-printed kwenye mtungi wako,hapo ndipo uakapojua,,,pia ujaribu kununua kwa dealers wengine,kama tatizo litaendelea nakushauri ukague pipe inayoenda kwenye plates na plates zenyewe ili kuhakikisha kwamba hazivujishi gesi,ikibidi badilisha kabisa...(ili kujua kama ni pipe inavujisha gesi,chukua maji yenye sabuni uparaze kwenye pipe kama kuna mahali imetoboka basi itatoa mapovu,fanya hivyo hivyo kwenye sehemu inapoingia kwenye mdomo wa plates.
cha msingi zaidi pia ukague Gas control valves,hizi hazitengenezeki kirahisi,so itabidi uingie mfukoni....pia kumbuka wakati unatumia sabuni ili kugundua leakage HAKIKISHA JIKO LAKO LIMEZIMWA.
nakutakia kila la kheri
 
Hapo inabidi uchek valve. Au hata nunua mpya ni kama 15 hivi. Mimi huwa natumia pia kupikia maharage lakini hufika miezi miwili.
 
Mkuu nimecheck valve kwa ukweli haipo tight! je wenzangu inakuwaje? is too tight or somehow loose? nimejaribu kusoma juu ya mfuniko wa valve kuna maandishi 30mbar na mtungi ninaotumia gross weight yake ni 30.2! je vitu hivi vinauhusiano?
 
Kwasiku 25 sio mbaya sana ila mimi hutumia kama siku 38 hivi na matumizi yangu kwa upishi asilimia kubwa natumia gas ila hawa wauzaji huwa wanachakachua kuna siku inakuwa chini ya 30 hivyo najua kuna mchezo wamenichezea.kingine jiko nalo linaweza kuwa sababu ya kuvujisha kama ni lasiku nyingi.nunua jiko bora usiogope bei kwani ndio yenye matumizi mazuri ya gas.
 
Mkuu nimecheck valve kwa ukweli haipo tight! je wenzangu inakuwaje? is too tight or somehow loose? nimejaribu kusoma juu ya mfuniko wa valve kuna maandishi 30mbar na mtungi ninaotumia gross weight yake ni 30.2! je vitu hivi vinauhusiano?

Wakati jiko limezimwa na valve iko on ukiweka sikio hapo karibu na valve utasikia kama inavuja. Hutakiwi kusikia kitu.
 
Back
Top Bottom