Msaada: Godoro gani zuri?

Kama upo Dar nenda HSC kule Ben Mkapa k'koo, jamaa wana magodoro poa sana...unajua kuwa ukikosea kununua godoro unahatarisha afya yako pia?

Ni kweli mkuu, ndo maana naamini kwa utaalamu wenu humu, nitatoka hima.
hapo HSC nitapita wiki ijayo nikiingia bongo, ili nithminishe na kuuliza dealers wao mikoani. niko Arumeru.
 
kumbe wewe umemwelewa,
manake godoro gani la kuulizia wakati yametapaa kila kona
kijana ebu tufafanulie hapa kamati ziingie kazini.

Mkuu hizo kamati zivumilie tu, muda bado bado.
mda ukiwadia wewe na Bishanga mtaongoza jahazi.
Sasa naona nimeelewa hilo godoro chapa mtu. teh teh teh.
 
Last edited by a moderator:

Wakuu nashukuruni sana, baada ya assesment yenu, hatimaye nina kitu mjengoni.
BAGAH, amini usiamini nimeota mfululizo kwenye hili godoro. BADILI TABIA na Baba V, kwa kweli pamoja na kuzunguka maduka mengi, sijafanikiwa kuapata godoro chapa mtu, lol. Kankwale, mandieta, figganigga, nimetest godoro dodoma likanesa na kunitupia pembeni, nikakoma hapohapo. charminglady na ummu kulthum, nadhani hata hili lina burudani. 🙂

So, nimeona niwaletee feedback wakuu.
weekend njema.
 
Last edited by a moderator:
Nimenunua godoro si zaidi ya miezi minne iliyopita la banco , lile la size ya mwisho. Niliamini Super banco ni zuri na wametoa guarantee ya mwaka. Lakini, sasa hivi ni chanzo cha kuamka shingo au mwili unauma kwani , godoro linabonyea chini.

Naomba uzoefu wa magodoro mengine, au ni spring mattress tu??
 
Yaani nimenunua godoro,nikilala usiku,nikiamka nakua nimechoka yaan mpaka kucha zinauma,tanfoam wabaya sana
 
nunua godoro lenye kunesanesa eti kaka Bujibuji lile godoro ambalo ukilalia linaspring linaitwaje vile ni spanco au? nimesahau jina nikumbushe
Wakuu hali zenu,
Nimechanganyikiwa kidogo baada ya mfululizo wa matangazo ya magodoro. Lipi ni bora zaidi? Nataka nitafute 6x4, sasa sijui lipi litanifanya niote vizuri.
Shukran!
 
Last edited by a moderator:
Yaani nimenunua godoro,nikilala usiku,nikiamka nakua nimechoka yaan mpaka kucha zinauma,tanfoam wabaya sana

Pole sana St. Duh, yaani sijui nianzie wapi, naona sasa tanfoam wanaanza kuwa associated na kucha. lol
 
Godoro chapa mtu linatengenezwa wapi?

Bubuji, godoro la pumba ni za mpunga au mahindi?
 
Yaani nimenunua godoro,nikilala usiku,nikiamka nakua nimechoka yaan mpaka kucha zinauma,tanfoam wabaya sana
hahaha hata mimi ilinitokea ila sikuchoka hadi kucha...tanfoam arusha ni magodoro mazuri ila mwanzo likiwa jipya ujiandae kuchoka mwili mzima...ila ukishalalia wiki hivi basi uchovu unaisha....ila kiukweli ni magodoro imara sana kibongobongo unalalia mpaka unalichoka mwenyewe ila ubora unakuwa palepale....
 



chukua super banco ndo mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…