Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Hutasaidika, jitahidi upate TANFOAM hutajuta mkuu, niliwahi kununua 2002 nkiwa yanki hadi leo hajijaonyesha kubonyea. Hii godoro haina mshindani, nilinunuaga dodoma hakuna kitu ni uchafu, jaribu tanfoam na ujiridhishe imetoka Arusha na si vinginevyo.
Nimesikitishwa sana na kilichonikuta.
Mnamo mwezi wa tano mwaka huu nilijikunjua nikalinunua godoro super banco 6x6 inch 6 kwa Tshs. 220,000/= na muuzaji akanishawishi kuwa super banco ndiyo bora kwa sasa, nikalichukua ila tangu mwanzo likawa linabonyea na kutengeneza mashimo nikajua ndiyo mtindo wake ila kadili siku zilivyosogea likawa mtumbwi katikati, baada ya miezi 6 nimerudi kutoa taarifa kwa muuzaji ananambia muda umepita sana ilibidi nitoe taarifa ndani ya miezi mitatu na sikutakiwa kuwa nimechana karatasi la juu wala nembo, mambo ambayo hakunieleza wakati nalinunua lile godoro, nikamwambia kuwa natambua kuwa sio kosa lake bali ni kosa la kiwanda hivyo wanisaidie mawasiliano ya moja kwa moja na kiwanda ila wamegoma wanadai wao watawasiliana nao ila dalili ni kwamba wananikwepa.
Kusema kweli inaniuma sana na tatizo sio pesa tu ila nasikitishwa na utapeli tunaofanyiwa na hivi viwanda vya magodoro kwa kushirikiana na shirika la viwango Tanzania tbs, inakuwaje watuaminishe kuwa bidhaa ni bora wakati zina matatizo!?
Mwanzo nilidhani labda kama ilivyo jambo la kawaida labda walikosea kwa baadhi ya magodoro katika kutengeneza na hivyo wanaweza kuchukua hatua ya kukufidia kwa mapungufu ambayo ni bahati mbaya ila baada ya kupitia maoni yenu inaonesha ndiyo ubora wa magodoro ya super banco hata nikifidiwa nitaletewa aina ileile.
Nilikuwa na mpango wa kukiandikia kiwanda kukilalamikia na nakala nitume kwa tbs ili wanipatie bidhaa iliyo bora.
Ikionekana hawawezi basi na mimi nitumie namna yoyote kuuhabarisha umma wa watanzania kuwa super banco sio magodoro ya kutoa pesa yako kununu.
Naomba ushauri nifanye nini?