Msaada: Harufu ya utapeli!

rajoh

Senior Member
Joined
Jun 2, 2011
Posts
174
Reaction score
142
Kuna jamaa yangu amenunua truck na trailers kutoka Netherlands kwenye kampuni flan hivi.

Aliwasiliana nao na kutuma pesa toka mwezi juni mwanzoni, tatizo limekuja kwenye shipment ya hizo trucks. Kwa kweli kwa sasa jamaa hawaelewi kwani nikiwapigia simu wanaongea but information zinajichanganya na kutia mashaka.
Anaomba kama kuna mtz yupo Nertherlands au unamfahamu mtu anayeweza kusaidia, tafadhali tunaomba msaada huo ili atusaidie kufatilia.

Wakuu nime-edit post kidogo kwa sababu za kipelelezi kidogo. (I mean nimehide baadhi ya taarifa)-mkuu Belinda na Bobby nadhani tuko pamoja.
 
Mkuu rajoh siku nyingine wasiliana na wazalendo ambao wapo nchi hizo watafuatilia ununuzi wa mali yako mpaka kupakiwa kwenye meli. Kwa habari zaidi nitumie pm.
 
Ni kweli kabisa. unajua tatizo ni mazoea. siku zote tumekuwa tukiagiza magari na vinginevyo online na hatujawahi kupata changamoto kama hii. Nadhani ndio kujifunza kwenyewe. Nitakuwa nikifanya hivyo mkuu.
 
Ni kweli kabisa. unajua tatizo ni mazoea. siku zote tumekuwa tukiagiza magari na vinginevyo online na hatujawahi kupata changamoto kama hii. Nadhani ndio kujifunza kwenyewe. Nitakuwa nikifanya hivyo mkuu.


Rajoh unaweza kufunguka zaidi ili tujue namna ya kukushauri? Kwa mfano wanajichanganyaje kama ulivyosema kwenye post yako? Kwa kawaida meli Holland ziko kila baada ya wiki 2 wanasemaje juu ya hili maana ni miezi miwili sasa kama nimekuelewa vizuri toka mmetuma hiyo pesa. Sometimes dealer wana tabia mbaya ya kusubiri mtelemko wa bei meli ili waweze kumaximize faida zao.
 


Namaanisha ukipiga simu, maranyingi hawapokei- nadhani ni kwa sababu wanajua no hiyo ni kutoka TZ. Incase wakipokea, wanatoa sound tu kuwa mzigo ulishatumwa. Ukiwauliza copy angalau ya docs, wanasema wamesahau kutoa(kitu ambacho sikiamini). documents wametuma kwa njia ya posta, kitu ambacho sikiamini sana. Tulikubaliana watumie DHL lakini wametumia posta. Toka wametuma docs, ni karibu wik ya 4, bila bila huko posta.
 

Hapo kwenye kutuma hapa ndio panachanganya zaidi, how come BL ikatumwa kwa posta?
 
Mkuu nakubali hii ni harufu ya utapeli, watu tunaagiza vitu vya usd 1500 documents zinatumwa kwa dhl na fedex unapewa na tracking number unafuatilia kila kitu. Sembuse huo mzigo mnene wa mamilioni mengi. Halafu siku hizi ukijua jina la meli unaweza kufanya tracking ukaona safari ya meli. Usisite kupata ushauri kwenye ubalozi wa hiyo nchi kwa hapa TZ ili kujua kama kampuni hiyo ipo kweli au la. Hivi kwani ile Account ya Benki iliyotumika kulipa pesa haiwezi kusaidia kuwajua wamiliki wake? Nchi nyingi zilizoendela zinaudhibiti mkubwa juu ya utambuzi wa wamiliki wa akaunti za mabenki. Au malipo yalifanyika kupitia Western Union?
 

malipo yalifanyika kwa njia ya bank. Ukipiga simu inapokelewa lakini taarifa ndio ziko nusunusu. Nimetoka kuongea nao muda huu, ananiambia ananiscania copy ya docs, nimemwambia anisomee BL no; anadai tena hana docs mkononi. Inasumbua kidogo.
 
Hapo kwenye kutuma hapa ndio panachanganya zaidi, how come BL ikatumwa kwa posta?

Tulivyoambiwa ametuma docs kwa njia ya posta ndo ikatushtua zaidi.
 
Tulivyoambiwa ametuma docs kwa njia ya posta ndo ikatushtua zaidi.

Keep us updated kwenye hili please. Nimejaribu kuwatembelea website yao just few minutes ago, actually nimewapigia pia simu n akuongea na Linda. They seem to be genuine lakini huo utoto wa kutuma docs kwa posta na wanajua kuna port charges kidogo unanisumbua kichwani pia huwezi kuokoa 20 euro za courier kwa kusababisha hasara ya thousands euro kwenye port charges. Nirudie endelea kutuupdate please!
 

exactly, huyo dada anaitwa Linda. Anadai boss wake ndio ana taarifa. ukitaka kuongea na boss wake, anakuunganisha lakini baada ya hapo inakuwa kama vile mtu kapokea halafu haongei chochote. ukiichek website, inaonekana wako genuine lakini shida ni hizi longolongo nyingi.
 

Boss wake kwenye email anasema usiwe na wasiwasi, tutakufidia port storage zote utakazopata kutokana na kuchelewa na documents.
 
Tulivyoambiwa ametuma docs kwa njia ya posta ndo ikatushtua zaidi.
Inanitia mashaka sana! Uzembe wanaouonyesha haufanani na hadhi ya nchi hiyo wala uzito wa aina ya biashara yenyewe! Isije kuwa kuna mkono wa Mnaijeria. Ikiwa itadhihirika kuwa kampuni hiyo si kampuni hewa na kunawatz unaowajua walishapata huduma yao na walitumia account ya Benk ile ile hapana shaka mzigo utacheleweshwa tu lakini mzigo utatumwa. Ndugu yangu usisite kutumia vyombo rasmi hasa vya kiserikali, wizara ya mambo ya nje wanaohusika na masuala ya biashara, huko ni rahisi hata kupata contacts za Netherlands. Hayo maofisi msiyachukie sana kila mahari kunawatu waungwana wenye msaaada sana na kama ikibidi kula acheni wale mradi suluhisho lipatikane.
 

Ni kweli mkuu.
hatua tunayofanya kwa sasa ni kuconfirm angalau uhalisia wa kampuni hiyo. kama iko legally na imeshatoa huduma kwa watu mbalimbali si mbaya, tutakuwa na matumaini lakini mzigo utachelewa. Nilipiga simu sana ya ubalozi mdogo wa Tz uholanzi, simu inaita bila majibu. Leo nimepita ubalozi wa uholanzi hapa tz, wakaniambia wanashughulika na visa zaidi. Kama nina isue yoyote niutafute ubalozi wangu uholanzi. Duh, labda kesho nitajaribu tena kuwatafuta. Nadhani Uholanzi wako saa 1 nyuma yetu.
 

Duh..! pole kwa hii situation mkuu, nimeona kuna mtu hapo juu atakusaidia ni vyema umsikilizie kwanza. Vinginevyo kuna mdogo wangu yupo pale Den Haag/The Hague angeweza kufuatilia. Ana namba ya simu ya balozi Kamala (anayewakilisha BENELUX hadi sasa) maana ubalozi mpya pale Uholanzi haujafunguliwa rasmi bado japo balozi kashaapishwa, ukiacha ile honorary consulate.
Nitamuomba dogo aulizie ''credibility'' kwa information tu ya hiyo kampuni siyo kuwasiliana nao. Siku nyingine ni vyema sana ufanye ''due diligence'' ya maana kabla hujanunua vitu mitandaoni..
 

Mkuu belinda asante sana. Hope by leo j4 utaweza mshirkisha mdogo wako huko uholanzi ajaribu kudadisi, au kama hutojali naomba uni PM no yake ili niweze fanya mawasiliano naye. Asante sana.
 
Mkuu belinda asante sana. Hope by leo j4 utaweza mshirkisha mdogo wako huko uholanzi ajaribu kudadisi, au kama hutojali naomba uni PM no yake ili niweze fanya mawasiliano naye. Asante sana.

Check your PM mkuu..!!
 
Belinda, nashukuru sana for your kind assistance. Ngoja nichek naye nadhani atakuwa msaada mkubwa sana. Asante sana.

BJ mimi pia nikushukuru kwani kama alivyo rajoh, mimi pia ni mdau kwenye hii tasnia. Rajoh usichoke kutuhabarisha muendelezo wa hii kitu ambacho Im sure wengi wako interested.
 
BJ mimi pia nikushukuru kwani kama alivyo rajoh, mimi pia ni mdau kwenye hii tasnia. Rajoh usichoke kutuhabarisha muendelezo wa hii kitu ambacho Im sure wengi wako interested.

Mkuu Bobby nitaendelea kuwahabarisha.... Belinda amenipa assistance kubwa sana kwani nimeshazungumza na huyo mtu Holland nadhan by kesho nitakuwa na majibu mazuri. Tuombe Mungu mambo yaende vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…