Malilambwiga
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 485
- 296
Unavyoonekana ktk maelezo yako wewe siyo mtu wa kuchukua "MAAMUZI MAGUMU" hivyo hata ukishauriwa vipi iwapo unafanya mchezo wa kwenda mbele hatua kumi na kurudi nyuma hatua mia ushauri wowote hautakusaidia. Kwa kuwa wewe ndiye unayejua uzito na wepesi wa madhira ysnayokukuta pia ni wewe unayepaswa kujua ubakie ktk ndoa hiyo au uondoke. Ila udhsuri wangu pima una umri gani sasa kisha tafakari unakusudia kuendelea kuishi ktk kero hiyo ya ndoa kwa umri gani uliobakia mbele yako. Ukipata majibu hayo amua kutangaza nia ya ndoa nyingine au ubakie ktk hiyo. Lengo la wanandoa kusuhishwa ni kwenda mbele na kujirekebisha sasa wewe pamoja na kusuluhishwa kama bado hujaona matokeo chanya subili muujiza na zidisha maombi mungu atakujibu kwa wakati wake.