Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Unavyoonekana ktk maelezo yako wewe siyo mtu wa kuchukua "MAAMUZI MAGUMU" hivyo hata ukishauriwa vipi iwapo unafanya mchezo wa kwenda mbele hatua kumi na kurudi nyuma hatua mia ushauri wowote hautakusaidia. Kwa kuwa wewe ndiye unayejua uzito na wepesi wa madhira ysnayokukuta pia ni wewe unayepaswa kujua ubakie ktk ndoa hiyo au uondoke. Ila udhsuri wangu pima una umri gani sasa kisha tafakari unakusudia kuendelea kuishi ktk kero hiyo ya ndoa kwa umri gani uliobakia mbele yako. Ukipata majibu hayo amua kutangaza nia ya ndoa nyingine au ubakie ktk hiyo. Lengo la wanandoa kusuhishwa ni kwenda mbele na kujirekebisha sasa wewe pamoja na kusuluhishwa kama bado hujaona matokeo chanya subili muujiza na zidisha maombi mungu atakujibu kwa wakati wake.
 
Atakaywvumilia mpaka mwisho ndiyevatakaye okoka. Ndoa haowezi kuvunjwa na mwamadamu yeyote.hata mahakama wanatoa talaka siyo kuvunja ndoa. Kumbuka kiapo chako. Tafuta suluhu
 
Sijajua kuhusu dhehebu lakini nakushauri ubadili dini uende dini yoyote hata ikiwa BUDHA,
uislamu n.k au uhame dhehebu sina uhakika sana kama ukihama dhehebu inakuwaje lakini
naona inaweza kukusaidia maana ndoa inakuwa imedvunjika automatically ikiwa utahama dini.
 
WAtu bwana....hajaomba ushauri! Anauliza process za kufuata kupata talaka....mna matatizo gani?

Kwa sisi wenye uzoefu na ndoa mtu akikwambia anataka kuachana Halafu ww ukamshsuri vinginevyo Unaweza kujikuta unagombana nae....km wameshindwana acha waachane kuliko madhara yanayoweza kutokea humo ndani ikiwemo hata kuuana!

Ndoa ngumu jamani, msione watu wanatembea wameshikana mikono!
 
WAtu bwana....hajaomba ushauri! Anauliza process za kufuata kupata talaka....mna matatizo gani?

Sasa wewe hii comment yako ni msaada kweli kwa huyo dada au unaungana na 'watu bwana?'
 
Kwa sisi wenye uzoefu na ndoa mtu akikwambia anataka kuachana Halafu ww ukamshsuri vinginevyo Unaweza kujikuta unagombana nae....km wameshindwana acha waachane kuliko madhara yanayoweza kutokea humo ndani ikiwemo hata kuuana!

Ndoa ngumu jamani, msione watu wanatembea wameshikana mikono!

Ndoa ndoa ndoa, why uamue kuishi na mtu msiye endana? Ujinga tu
 
Ndoa ndoa ndoa, why uamue kuishi na mtu msiye endana? Ujinga tu

Mkuu ndoa za siku hizi watu wansjuana tabia zao halisi baada ya kuanza kuishi pamoja....ndio maana ni vizuri kuishi na mwenza wako walau miezi6 ili kuona km mkioana mtaweza kuvumiliana...

Hii inakuwa km probation period kwa wote, mkishindwana basi mnapigana chini for good kila mmoja anachukua 50 zake!
 
njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha
 
Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe
daaah...huu ni ukweli unaoumiza
 
Mbona tatizo lako linaonekana "sio tatizo"? Watu wana matatizo makubwa katika ndoa jaribu kujishusha tatizo litaisha ila kama unataka liishe!
 
Tafuta mwanasheria/lawyer mwenye uzoefu na hili jambo otherwise utajikuta unazungushwa tu na watu wanaojaribu kulinda imani zao zaidi ya maslahi yako, life is too short.
 
Mtafute Joyce Kiria Wanawake Live atakueleza process nzima....Yeye aliachana na mme wake wa ndoa DJ Nelly na kufunga ndoa tena na Henry Kilewo.
 
Last edited by a moderator:
Wataalamu wanasema strong and true love inadumu three years maximum. ..kama marriage imefikia hatua ya luga chafu na kupigwa.....kula kona....ila bana strange enough mama yangu yuko 70s na bado analalamika baba haachi fedha...au anaacha kidogo...anawanawake nje na amezaa nao....ila wapo pamoja mpaka leo...anampikia anamfulia...na akiwa na shida ya hela mama anampigania...dah.
 
Kwa sisi wenye uzoefu na ndoa mtu akikwambia anataka kuachana Halafu ww ukamshsuri vinginevyo Unaweza kujikuta unagombana nae....km wameshindwana acha waachane kuliko madhara yanayoweza kutokea humo ndani ikiwemo hata kuuana!

Ndoa ngumu jamani, msione watu wanatembea wameshikana mikono!

Ila pamoja na yote hayo ndoa inahitaji uvumilivu
 
Wataalamu naomba mnisaidie nina tatizo la ndoa, Ndoa hii ni ya kikristo ina miaka sita kwa sasa lakini imekuwa na makelele mengi kila kukicha, tumeshatengana mara kadhaa na ksuluhishwa lakini kwa sasa hiv tunaishi tu kama mtu na adui yake ndani ya nyumba moja, watu wa nje wanadhani ni ndoa kumbe hamna kitu ni kuwaridhisha tu wale waamuzi kama mchungaji na washauri wa ndoa.
Mimi kwa upande wangu kama mwanamke siridhishwi kuishi na mwanaume ambaye haonyeshi kunipenda kiasi cha kuishi tu kama mtu na adui yake kwa nje watu watuone tuko pamija wakati rohoni kila mtu na mwenendo wake.
Nafikiria kutafuta talaka katika vyombo vya sheria lakini sijua nianzie wapi wala nimalizie wapi wala iweje
Naomba msaada kwa wanaojua

Juzi nimesuruhishwa na nimetulia. Jana jamaa yangu kamlapua mkewe..mleo niko kikaoni nasuruhisha ndoa ya watu na wewe huwezi kuishi na mumeo...haya nipm nikubebe mie. Sikia, ndoa siku hizi ni laana tu hebu tulia na sikiliza mumeo anatakaje. Acha wehu. Ukiona huwezi nishasema nipm nikubebe uwe nyumba ndogo nyie watu hamsikii kabisa sijui mnatakaje...
 
Sasa wewe hii comment yako ni msaada kweli kwa huyo dada au unaungana na 'watu bwana?'

Mimi sina msaada wa kumpa ila najaribu kuwarudisha watu wampe msaada aliouomba.....kama watu wamefikia hatua ya kuishi kama maadui ndani ya nyumba kuna hatari hapo
 
Ila pamoja na yote hayo ndoa inahitaji uvumilivu

Ni Yesu pekee aliehimili mikiki mikiki ya uvumilivu mpaka kifo cha mateso, kwa mwanadamu wa sasa hiyo ni ngumu sana Khantwe...naongea haya kwa experience niliyopitia mm!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ndoa za siku hizi watu wansjuana tabia zao halisi baada ya kuanza kuishi pamoja....ndio maana ni vizuri kuishi na mwenza wako walau miezi6 ili kuona km mkioana mtaweza kuvumiliana...

Hii inakuwa km probation period kwa wote, mkishindwana basi mnapigana chini for good kila mmoja anachukua 50 zake!
Probation period ya 5 years imetulia. Mnakuwa mmezoeana na gharama za kuachana na kuanzisha mahusiano mapya ni kubwa kila pande. Hivyo mtavumiliana kwa kila kikwazo.
 
Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe
Hapo kwenye rangi ya bluu amepata msaada, ni jukumu lake tu kumeza au kutema.
 
Back
Top Bottom