Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Msaada: Hatua za kuachana na mume wa ndoa

Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe

Sijaelewa wewe ni msajili wa ndoa za kikristu kivipi. Wewe ni Mchungaji au padri? Au ni waserikali? Nieleweshe Tafadhali.
Ushauri wangu kwa bidada: hujafafanua hiyo ndoa ni ya dhehebu gani. Km ni ya kikatoliki tafuta kitabu kinaitwa sheria za kanisa. Kinapatikana bookshop pale st.joseph. kisome vizuri.
Wakatoliki hawatoi talaka ila wanabatilisha ndoa kutokana na sababu zilizoainishwa ktk hicho kitabu. Wakishabatilisha wewe na mumeo mtakuwa huru kuoa ama kuolewa endapo mahakama ya serikali itashughulikia suala la Mali na malezi ya watoto.
Hakikisha sababu zako unazotaka kuombea talaka zimo kwenye hicho kitabu. Kama sivyo basi imekula kwako.
Hii process ni ndefu inaweza kuchukua ht miaka minne. Nimeshuhudia imefanyika kwa ndugu yangu wa karibu na sasa ameolewa tena.
Dada..ndoa sio karaha na manyanyaso... Kama vipi sepa kimya kimya.
Na isije ikawa wewe ndo Una matatizo unamsingizia mumeo. Kila la kheri.
 
Acha kuongopa na kupotosha, ndoa ya kikristo inavunjwa kama ndoa nyingine tu zinavyovunjwa, na kwa ukristo kama mmoja ametembea nje ya ndoa na kuna ushahidi hilo sababu kubwa ya kuvunja ndoa na inavunjwa kikanisa kabisa, hivyo acha kumdanganya na kumfanya aishi maishi ya shida wakati kuna uwezo wa kuachana!

Hakuna msamaha mmoja anapotembea nje ya ndoa!

Babrosa;
Hivi kati yangu mimi na weye ni nani anapotosha watu hapa? Sijui weye ni imani gani ila naomba nikuambie weye pamoja na hao waliopotoka mioyo yao ka weye kuwa wala si mimi ila ni kwa Neno la Mungu; HAKUNA TALAKA IWAYO YOTE katika ndoa ya Kikristo. Ni kifo tu kitakutenganisha. Sawa, wapo ambao huamua kujiondoa na kwenda watakako. Nimeona hata hayumkini wachungaji waliodiriki kwenda mahakamani na kuomba talaka. Kwa sababu tu ya ugumu wa mioyo yao, watapewa. Wengine wametafuta vijisababu na kuongeza fedha juu yake, talaka zikatolewa.
Kwako weye mwanadamu, umepata uhuru wa kumtafuta mwingine umchakazeee uende tena mahakama nyingine na fedha yako umtelekeze. Hayumkini, waweza tafuta Baradhuli limoja likajifanya kuwa umelifumania na mkeo, ukwamwacha huyo tena na wengine wengi tuu. Sawa, lakini mbele za Mungu, mkeo ni mmoja tuuu, hadi kifo kiwatenganishe. Sitaki kubishana ila nimeandika hivi kwa ajili ya yule mwenye hofu ya Mungu ndani yake, wala si vinginevyo.
 
Sijaelewa wewe ni msajili wa ndoa za kikristu kivipi. Wewe ni Mchungaji au padri? Au ni waserikali? Nieleweshe Tafadhali.
Ushauri wangu kwa bidada: hujafafanua hiyo ndoa ni ya dhehebu gani. Km ni ya kikatoliki tafuta kitabu kinaitwa sheria za kanisa. Kinapatikana bookshop pale st.joseph. kisome vizuri.
Wakatoliki hawatoi talaka ila wanabatilisha ndoa kutokana na sababu zilizoainishwa ktk hicho kitabu. Wakishabatilisha wewe na mumeo mtakuwa huru kuoa ama kuolewa endapo mahakama ya serikali itashughulikia suala la Mali na malezi ya watoto.
Hakikisha sababu zako unazotaka kuombea talaka zimo kwenye hicho kitabu. Kama sivyo basi imekula kwako.
Hii process ni ndefu inaweza kuchukua ht miaka minne. Nimeshuhudia imefanyika kwa ndugu yangu wa karibu na sasa ameolewa tena.
Dada..ndoa sio karaha na manyanyaso... Kama vipi sepa kimya kimya.
Na isije ikawa wewe ndo Una matatizo unamsingizia mumeo. Kila la kheri.

tatty;
Nimeusoma ushauri wako na kuuelewa vizuri sana. Pia, kwa mtazamo wako naamini kuwa weye ni mkatoliki mzuri tuu. Ila naomba nikufahamishe kuwa, mimi ni Mchungaji. Lakini, back ground yangu ni Mkatoliki mzuri saana.
Naamini, naujua Ukatoliki kuliko hata wengine wengi tu tuliokaa nao katika Seminary. Hayo tuyaache, ila nimependa kukuambia kuwa mimi ni Mkatoliki ili kukufahamisha kuwa, Hakuna talaka katika ndoa ya Kikatoliki pia.
Bidada aliomba namna ya kuweza kuachana na mume wake. Soma taratibu thread yake, utamwelewa kuwa yeye ndiye anataka kuachana. Sawa, umemwambia asepe kimya kimya. Je! Anaweza kwenda kukaa awe "Mjane Baridi" kwa miaka yake yoote? Haruhusiwi kuolewa tena!!! Huo ndio msimamo wa Kanisa!!!
Ndoa batilishwa ni zile zinatokana na kuolewa na mwenzi mwenye imani tofauti na Katoliki. Idhini inatolewa kutoka Roma. Upooooo??? Ndio maana inachukua muda mrefu hivyo. Na ukute pia keshazaa nje ya ndoa hiyo.
Kiufupi tu ni kuwa HAKUNA TALAKA. Ingelikuwa hivyo, wengi wala wasingelikuja andika humu.
 
Mangatara.
Najua kabisa kuwa katoliki hawatoi talaka Bali wanabatilisha. Na sababu za kubatilisha zimeainishwa vizuri tu kwenye hicho kitabu nilichosema.(SHERIA ZA KANISA,SAKRAMENTI YA NDOA- By David Mubirigi)
Sababu zilizopo humo ni za msingi mno..si nyepesi nyepesi tu. Ndo maana nikamshauri akisome ili aone km sababu zake zinaendana. Na Kama Hana sababu za msingi hawezi kufanikiwa.
Ninaongea kwa experience coz nimeshuhudia case km hiyo kwa ndugu yangu wa karibu sana. Na nilikuwa shahidi wa hiyo kesi.
Na km mtu anapata manyanyaso kwenye ndoa..awe mume au mke...kwann ukomalie hiyo ndoa? Kuna watu wanapata vipigo everyday,na manyanyaso ya kila aina mpk ya kuleta madhara makubwa km ulemavu,magonjwa ya moyo na kuathirika kisaikolojia.

Mfano ndo hivyo...hapo kuna ndoa kweli? Bora kusepa na hata mungu anaona. Tusikomalie tu Sheria za makanisa, tuangalie utu na reality.
Mimi kwenye ndoa kikubwa nilichokifata ni dyu.dyu I mean sex..na mapenzi niliyonayo kwake na yeye aliyonayo kwangu. Km napata vipigo,ushirikina,dharau na mateso ya kila namna hizo sheria zenu zitanisamehe kabisa.
Afya yangu kwanza...mengine baadaye. Na huyu Mungu wetu si mjinga..anatuelewa sana. Kuna ndoa kweli zimeunganishwa na mungu. Na ukiona ndoa haina amani ni vita tu na hawajawahi kuelewana ikafikia wanachukiana kupitiliza ujue kuwa ni shetani amewaunganisha. SI NDOA ZOTE ZINAUNGANISHWA NA MUNGU.
 
Tafuta divorce lawyer mzuri dada, ila uwe na pesa ya kumlipa.
Mahakamani utapata talaka,hata kama ndoa ya Christian .... kama kweli unasababu ya maana kuachana na huyo mume.

Au kama vipi ondoka hapo kwa mumeo, nenda kwa mjumbe akuandikie barua kwamba umeondoka kwa mumeo.
kajitegemee peke yako. Baada ya mwaka file divorce na uonyeshe barua ya kutengana na mumeo mwaka 1, utapata talaka yako.
 
Ni- pm ..ntakupa njia muafaka na itakusaidia.
wataalamu naomba mnisaidie nina tatizo la ndoa, ndoa hii ni ya kikristo ina miaka sita kwa sasa lakini imekuwa na makelele mengi kila kukicha, tumeshatengana mara kadhaa na ksuluhishwa lakini kwa sasa hiv tunaishi tu kama mtu na adui yake ndani ya nyumba moja, watu wa nje wanadhani ni ndoa kumbe hamna kitu ni kuwaridhisha tu wale waamuzi kama mchungaji na washauri wa ndoa.
Mimi kwa upande wangu kama mwanamke siridhishwi kuishi na mwanaume ambaye haonyeshi kunipenda kiasi cha kuishi tu kama mtu na adui yake kwa nje watu watuone tuko pamija wakati rohoni kila mtu na mwenendo wake.
Nafikiria kutafuta talaka katika vyombo vya sheria lakini sijua nianzie wapi wala nimalizie wapi wala iweje
naomba msaada kwa wanaojua
 
Kwasababu wewe ndio unahitaji kuachana na mmeo la kwanza anza kuishi na mme mwingne maana inaonesha unatabia ya kihuni, pili inaonesha mama yako aliwahi achana na baba yako kwa hiyo wewe unafuata roho ileile ya mama yako ya kuachana Tatu wewe unaonekana hushauriki Kwasababu unadhani unauwezo pengine unafanya kazi kumbuka unamtesa sana mtoto na huyo mtoto atafuata maisha hayohayo uliyonayo baadae.
 
Wataalamu naomba mnisaidie nina tatizo la ndoa, Ndoa hii ni ya kikristo ina miaka sita kwa sasa lakini imekuwa na makelele mengi kila kukicha, tumeshatengana mara kadhaa na ksuluhishwa lakini kwa sasa hiv tunaishi tu kama mtu na adui yake ndani ya nyumba moja, watu wa nje wanadhani ni ndoa kumbe hamna kitu ni kuwaridhisha tu wale waamuzi kama mchungaji na washauri wa ndoa.
Mimi kwa upande wangu kama mwanamke siridhishwi kuishi na mwanaume ambaye haonyeshi kunipenda kiasi cha kuishi tu kama mtu na adui yake kwa nje watu watuone tuko pamija wakati rohoni kila mtu na mwenendo wake.
Nafikiria kutafuta talaka katika vyombo vya sheria lakini sijua nianzie wapi wala nimalizie wapi wala iweje
Naomba msaada kwa wanaojua

Hujatulia wewe mwanamke na inavyoonyesha unakiburi kwa mumeo. Mwanaume hawezi ishi na mkewe kama adui yake kama mwanamke anaadabu kwa mumewe. Kinachoweza mfanya mwanaume aishi hivyo ni jeuri ya mwanamke.
 
Jamani mwenzenu ashawaambia kuwa washasuluishwa sana na wazee na watu wa Dini pia mbona mnakuwa wagumu kuelewa.
Mpaka mtu anaomba process za kuachana na mtu ujue hali imefikia mwisho wa reli.....nashangaa sana hizi sheria zetu wakristo eti hakuna talaka. Jamani kuna binadamu wengine huwez ishi nao jamani, ni kama wana wadudu kichwani hawasikii hawaambiliki.
Plus mnamtuhumu as if yeye ndio shida.
We mdada nenda zako front kisheria mnatenganishwa, Mengi si yule pale kaachana na mkewe.....it means walishindwa kusuluishwa kabisa
 
We hujiulizi biblia hiyo hiyo inasema kilichotenganshwa na Mungu binadamu asikitengue but then
Mbele YESU anasema kwenye dhambi ya uzinzi mnaweza kaachana...?
Mi nadhani wakatoliki/waroma walitudanganya wakati wanakusanya haya maandiko wakachomeka ishu ya mke mmoja
 
Hujatulia wewe mwanamke na inavyoonyesha unakiburi kwa mumeo. Mwanaume hawezi ishi na mkewe kama adui yake kama mwanamke anaadabu kwa mumewe. Kinachoweza mfanya mwanaume aishi hivyo ni jeuri ya mwanamke.

Wanaume ni malaika au?
 
Jamani hili sio jukwaa la ushauri wa ndoa na mahusiano, hili ni jukwaaa sheria.......period

Kama hujui kitu kaa kimya na sio kujigeuza mshauri wa ndoa sababu hujui mapito aliopitia kufikia hapo

Joyce Kiria Nkongo alikua na ndoa ya kikristo na akaivunja mahakamani na talaka akaiposti online na ndio akaolewa tena na kamanda wa cdm
View attachment 289576
Josephine Mushumbusi mchumba wa Dr slaa alimburuza mumewe wa ndoa kanisani na talaka ikatoka
ImageUploadedByJamiiForums1442859858.007054.jpg

Kama hakuna wataalamu wa kukushauri humu ndani Nakushauri nenda mahakamani au hata kwa mtendaji kata watakupa utaratibu ingawa ni mgumu kidogo ila unawezekana
 
unatatizo kama lang. nataman sana kama utakua na nia tufarijiane, japo ni ngumu humu mtandaon najua anything is possible under the sun. mm pia mkatoliki.
kidini hairuhusiwi ni mpaka mmoja afariki. kam a ni ndoa za serikali najua inawezekana.
baba mtakatifu kapitisha talaka, find out more info ila kila nkisoma biblia inasema no. ndoa itatenganishwa kwa kifo tuu.
 
Kwenye bible ndoa huvunjika Mpaka kifo au mtu akikutwa na uzinzi basi. Ndoa ni tete siku hizi aisee
 
hakika ushauli huu nimeupenda na ewe uliotoa ushauri eeeehhhhh mwenyezi mungu akubariki na abariki fikra zako daima..... sikia dada unaetaka ushauri,, jaribu kumuomba mungu ainisulu ndoa yako na pia jaribu kuchukua hatua kwa kuchunguza tatizo la ndoa yako na chanzo ili uweze kupambana na jinamizi linalotetea ndoa yako na hapo utapata suluhu ya kila tabu upatayo sasa,,, kumbuku ulishika bible siku ya ndoa yako na kuapa kua utakua na mumeo katika vipindi vyote vya shida na raha na kifo pekee ndicho kitawatenganisha,, usife moyo omba mungu kila kukicha atajibu kilio chako.... Nakutakia uvumilivu na Mungu atainusulu ndoa yako kuwa na imani tu
 
Back
Top Bottom