Mama miye ni msajili wa ndoa za Kikristo. Nimewahi kukutana na wengine ka weye. Ushauri wangu ni huu; Huna pa kwenda tena!! Sijui ka utaniamini ila huo ndo ukweli kabisa wa ndoa ya Kikristo. Nadhani umewahi kusoma maandiko haya; Marko 10 : 9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Swali langu ni kwamba, Je ulikurupuka kuingia katika ndoa hiyo? Ulishurutishwa? Una uhakika gani kwamba mwenye tatizo sio wewe ni yeye?
Ushauri wangu; Acha kiburi, nyenyekea chini ya mumeo, sikiliza mashauri ya wakuu, mlilie Mungu zaidi kuliko kuwalilia watu. Kiila mtu, anayo mizigo yake. Nyumba nyingi leo hii zipo ICU, usitamani ya mwingine. Chezea yako mpaka uikute jehanam.
Kwa faida ya wale wenye mawazo ka yako; Ndoa ya Kikristo hainaga talaka. Mpaka kifo kiwatenganishe
Sijaelewa wewe ni msajili wa ndoa za kikristu kivipi. Wewe ni Mchungaji au padri? Au ni waserikali? Nieleweshe Tafadhali.
Ushauri wangu kwa bidada: hujafafanua hiyo ndoa ni ya dhehebu gani. Km ni ya kikatoliki tafuta kitabu kinaitwa sheria za kanisa. Kinapatikana bookshop pale st.joseph. kisome vizuri.
Wakatoliki hawatoi talaka ila wanabatilisha ndoa kutokana na sababu zilizoainishwa ktk hicho kitabu. Wakishabatilisha wewe na mumeo mtakuwa huru kuoa ama kuolewa endapo mahakama ya serikali itashughulikia suala la Mali na malezi ya watoto.
Hakikisha sababu zako unazotaka kuombea talaka zimo kwenye hicho kitabu. Kama sivyo basi imekula kwako.
Hii process ni ndefu inaweza kuchukua ht miaka minne. Nimeshuhudia imefanyika kwa ndugu yangu wa karibu na sasa ameolewa tena.
Dada..ndoa sio karaha na manyanyaso... Kama vipi sepa kimya kimya.
Na isije ikawa wewe ndo Una matatizo unamsingizia mumeo. Kila la kheri.
