Tafuta wafanyabiashara kadhaa wanaofanya unachotaka kufanya,uongee nao(ana kwa ana) kuhusu hiyo biashara unayofanya,lengo ni kupata picha hiyo biashara inafanywaje,changamoto za biashara na wanavyozikabili na mbinu kadhaa za kuuza vizuri zaidi.Ujue bidhaa wanatoa wapi,faida ya bidhaa ipoje na mengine mengi utajifunza kama utauliza maswali muhimu.Kila mmoja ataeleza atakachotaka kukuambia,ni muhimu kuongea na zaidi ya mmoja upate picha pana ya unachotaka kufanya.Wengine hawatotoa ushirikiano mzuri,lakini nimejifunza watu wengi ni wema na wapo kutoa ushirikiano kwa wengine kama utaonesha una nia ya kujifunza.
Chagua location sahihi ya biashara,hata kama itakuchukua muda lakini location inamatter sana kwenye biashara,katika kuongea na hao wafanyabiashara,dadisi ni location zipi zinafanya vizuri zaidi kwa biashara unayotaka kufanya.Then utafute location ambayo angalau itakupa advantage uanze kwa ufanisi kwa asilimia kubwa.
Jua ni bidhaa gani muhimu ambazo ni lazima uanze nazo,hii unaweza kujua kutoka kwa mahojiano na watu wanaofanya biashara hiyo.Nyingine utaongeza kadiri ya uhitaji,maana mahitaji ya location mbili tofauti,hutofautiana pia.Biashara ni mzunguko wa pesa,usikubali kuweka bidhaa ili mradi ujaze duka tu,jitahidi uweke bidhaa zenye kuhitajika,zinazotoka.
Kwa mtaji utakaanza nao wowote ule,jitahidi sehemu yako ya biashara ivutie.Chagua design nzuri ya kupangilia muonekano wa sehemu yako ya biashara,hutokamilika..mengine unaweza kufanya baadae.
Ukishaanza biashara yako,kuwa mvumilivu,ondoa mategemeo ya mafanikio ya haraka,ipe muda na wekeza mapato katika kukuza biashara katika bidhaa zenye uhitaji na ambazo huna.Wahudumie vizuri wateja wako na kama utaweka mtu mwingine kama muuzaji hakikisha anahudumia vizuri wateja wako.Itakusaidia kuwa na wateja maalumu ambao watakuwa wakirudi mara kwa mara wakihitaji bidhaa fulani.
Hakikisha unaijua biashara yako vizuri ikiwezekana kuliko hata anayekuuzia,kama utaweka mtu,kuwa karibu na biashara,ujue kwa asilimia kubwa kila kinachotokea kwenye ofisi yako.
Kwa yote utakayojifunza kabla ya kuanza biashara hayototosha,jitahidi uwe na utulivu wa kusuluhisha kila changamoto mpya itakayojitokeza na ujiongeze pale itakapobidi ili kuhakikisha biashara yako inaenda vizuri.