Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂na asije akachukulia poa kuna chuma ulete kuna kuwaloga wateja waje kuna kikinga biashara isitupiwe uchafu kuna ww mwenyewe kujikinga yaani ukienda kwa mganga asipokuambia lala makaburini basi hapo hajakupa dawa jiandae kuanguka kabla ya muda wako .
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo hayo ya kinaJambo la kwanza tafuta TIN ya biashara pamoja na vibali vyote vya biashara kama manispaa na TFDA
Tafuta location nzuri ambayo ina movement kubwa ya watu maana hiyo biashara haihitsji sehemu ambazo zimejificha.
Fanya research ni bidhaa zipi huwa zinauzwa kwa wingi na wapi pa kuzipata kwa urahisi.
Line zako zote za biashara zinasoma majina yako iwe nmb,crddb na hata tigo pesa kuepusha kupigwa kwa line hizi za watu
Hakikisha una record trend yako ya biashara kila mwez kwa bidhaa zinazopendwa na kama unapanda au unashuka wengine wataendelea
Uswahili wamaanisha niniKwanza kabisa, "hiyo sehemu Ina uswahili?" Wengi wanafeli kwa hilo. Eti Yesu atanisaidia.!!
Sent using Jamii Forums mobile app
Aksante! Kwanini kuna biashara zinahitaji lesseni na zingine hazihita? Na hiyo lesseni inapatikana wapi?Tafuta sehemu ambayo unadhani wateja wengi wanaishi/wanapita. Bila shaka Una mtaji tayari na umeishafanya forecast ya biashara ukaiona ni endelevu.
Tafuta duka/suppliers utakaponunua bidhaa kwa bei nafuu na ujue jinsi ya kufikisha dukani kwako hizo bidhaa kwa bei nafuu. Bei nafuu i dont mean substandard stuff.
Bahati nzuri biashara yako haihitaji kuwa na leseni zaidi ya leseni ya biashara from halmashauri/Manispaa. Pata TIN ya Biashara na ufanyiwe makadirio TRA ambayo utaanza kulipa baada ya miezi sita. Kama mauzo yako kwa mwaka (gross) yanazidi 11m, nunua machine ya efd, kama hayazidi hapo nenda stationery tengeneza cash sales zinazoonyesha TIN yako na jina.
Oh sorry vipodozi vinahitaji leseni pia from TMDA
You are ready for the business
Aksante sana mkuu umeniongezea kitu kikubwa hapoTafuta wafanyabiashara kadhaa wanaofanya unachotaka kufanya,uongee nao(ana kwa ana) kuhusu hiyo biashara unayofanya,lengo ni kupata picha hiyo biashara inafanywaje,changamoto za biashara na wanavyozikabili na mbinu kadhaa za kuuza vizuri zaidi.Ujue bidhaa wanatoa wapi,faida ya bidhaa ipoje na mengine mengi utajifunza kama utauliza maswali muhimu.Kila mmoja ataeleza atakachotaka kukuambia,ni muhimu kuongea na zaidi ya mmoja upate picha pana ya unachotaka kufanya.Wengine hawatotoa ushirikiano mzuri,lakini nimejifunza watu wengi ni wema na wapo kutoa ushirikiano kwa wengine kama utaonesha una nia ya kujifunza.
Chagua location sahihi ya biashara,hata kama itakuchukua muda lakini location inamatter sana kwenye biashara,katika kuongea na hao wafanyabiashara,dadisi ni location zipi zinafanya vizuri zaidi kwa biashara unayotaka kufanya.Then utafute location ambayo angalau itakupa advantage uanze kwa ufanisi kwa asilimia kubwa.
Jua ni bidhaa gani muhimu ambazo ni lazima uanze nazo,hii unaweza kujua kutoka kwa mahojiano na watu wanaofanya biashara hiyo.Nyingine utaongeza kadiri ya uhitaji,maana mahitaji ya location mbili tofauti,hutofautiana pia.Biashara ni mzunguko wa pesa,usikubali kuweka bidhaa ili mradi ujaze duka tu,jitahidi uweke bidhaa zenye kuhitajika,zinazotoka.
Kwa mtaji utakaanza nao wowote ule,jitahidi sehemu yako ya biashara ivutie.Chagua design nzuri ya kupangilia muonekano wa sehemu yako ya biashara,hutokamilika..mengine unaweza kufanya baadae.
Ukishaanza biashara yako,kuwa mvumilivu,ondoa mategemeo ya mafanikio ya haraka,ipe muda na wekeza mapato katika kukuza biashara katika bidhaa zenye uhitaji na ambazo huna.Wahudumie vizuri wateja wako na kama utaweka mtu mwingine kama muuzaji hakikisha anahudumia vizuri wateja wako.Itakusaidia kuwa na wateja maalumu ambao watakuwa wakirudi mara kwa mara wakihitaji bidhaa fulani.
Hakikisha unaijua biashara yako vizuri ikiwezekana kuliko hata anayekuuzia,kama utaweka mtu,kuwa karibu na biashara,ujue kwa asilimia kubwa kila kinachotokea kwenye ofisi yako.
Kwa yote utakayojifunza kabla ya kuanza biashara hayototosha,jitahidi uwe na utulivu wa kusuluhisha kila changamoto mpya itakayojitokeza na ujiongeze pale itakapobidi ili kuhakikisha biashara yako inaenda vizuri.
🤣 😂 Hiyo yapili kutoka mwisho nimeipenda asante sana kwa dondoo hizo
- Natumaini mtaji unao
- Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6
- Tafuta TIN TRA
- Lipa kodi
- Tafuta leseni kwa halmashauri/manispaa/jiji
- Weka mzigo dukani
- Weka binti mrembo auze
- Anza kuhesabu mapato
1. Mtaji nimedunduliza kwenye kilimo kwa kuwa kilimo ni cha msimu nilitaka nipate chanzo kingine cha mapatoNaomba kufaham yafuatayo kabda sijashauri chochote.
1: Mtaji wa kufungua biashara hiyo umeupataje?
2: Vitenge na vipodozi aina zote unaviweka flame Moja au office tofauti.
3: Unafanya au umewahi fanya kazi/shughuli gani kabda?
4: Eneo/mji unao plan kufungua biashara zako.
5: Utasmama mwenyewe au utamuweka mtu?
Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6...hii ni kodi ya fremu sio?.
- Natumaini mtaji unao
- Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6
- Tafuta TIN TRA
- Lipa kodi
- Tafuta leseni kwa halmashauri/manispaa/jiji
- Weka mzigo dukani
- Weka binti mrembo auze
- Anza kuhesabu mapato
Tafuta sehemu ambayo unadhani wateja wengi wanaishi/wanapita. Bila shaka Una mtaji tayari na umeishafanya forecast ya biashara ukaiona ni endelevu.
Tafuta duka/suppliers utakaponunua bidhaa kwa bei nafuu na ujue jinsi ya kufikisha dukani kwako hizo bidhaa kwa bei nafuu. Bei nafuu i dont mean substandard stuff.
Bahati nzuri biashara yako haihitaji kuwa na leseni zaidi ya leseni ya biashara from halmashauri/Manispaa. Pata TIN ya Biashara na ufanyiwe makadirio TRA ambayo utaanza kulipa baada ya miezi sita. Kama mauzo yako kwa mwaka (gross) yanazidi 11m, nunua machine ya efd, kama hayazidi hapo nenda stationery tengeneza cash sales zinazoonyesha TIN yako na jina.
Oh sorry vipodozi vinahitaji leseni pia from TMDA
You are ready for the business
Niko hapa nachukua madini toka kwa wachangiaji watukufuHabari wanajukwaa hili la biashara!
Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifungue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na wakaka wa NMB, CRDB pamoja na NBC)
Sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
😂😂😂😂😂Angalia mazingira kwanza, kama uswahilini hakikisha umejiimarisha vizuri kwa kinga za kiroho na vijicho. Biashara itaenda.
Atafanyiwa makadirio, na atakuwa analipa kila robo ya mwakaTafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6...hii ni kodi ya fremu sio?.
Hiyo Kodi inayofuata hapo tena analipa ni ya nini? kama ni kodi ya mapato alipe kabla ya kupata?.
Aksante sana kwa uchambuzi wako wa kina mkuuMimi naweza nikakupa hint kwenye vipodozi manake ndo nilipo na uzoefu
Kwanza Hiyo biashara Kwa kuiangalia ni rahisi ila ni very complicated
Inaangalia Mazingira yako
Hapa utagusa lifestyle ya wateja unaowatarajia
Kipato na hali ya hewa pia ni muhimu
Katika Vipodoz hasa vya wanawake kuna mambo Kama trend na uwezo wa kipodozi kuleta matokeo Kwa haraka
Kama wateja wako ni watu wa kiwango cha chini hakikikisha product yako ya ghali haizidi 20,000
Nyingi ziwe kwenye 3000-12,000 hivi na chache za 13,000-20,000
Katika hizi bidhaa Utakaangalia zaidi iliyopo kwenye trend fuatilia sana FB Kwa watu wa kundi hili
Kwa Wateja wa kiwango cha Kati changanya bidhaa mpaka za Bei ya 50,000 hivi
Hapa utawapata wengi wanaopenda kupendeza na bidhaa za bei za kati lakini pia uzijue vyema kulingana na trend
Hapa wanazingatia skin care routine tofauti kidogo na kundi la chini
Kundi la juu
Hapa utaweka bidhaa kwanza Kwa kuzingatia Brand kubwa kubwa mfano Laroche, CeraVe,Eliza Jones N.k
Hili ni kundi la watu wanaonunua bidhaa hata moja ya 100,000 bila tatizo
Kikubwa tu ionekane kwenye website kubwa kubwa huko iwe na reviews za kutosha.
Turudi kwenye kundi namba moja ambalo ndo WaTanzania wengi tupo
- hapa panapatikana bidhaa zinazofukuziwa na serikali
-hapa panapatikana bidhaa namba mbili(copy)
-pia kuna bidhaa nyingi zenye matokeo hasi kwa ngozi
-lakini pia ni kundi linalohitaji mtaji Mdogo zaidi
Ukishaelewa unahitaji kushikilia wapi karibu tuongezeane nondo
Heshima yako naomba nikutafute pmNaomba kufaham yafuatayo kabda sijashauri chochote.
1: Mtaji wa kufungua biashara hiyo umeupataje?
2: Vitenge na vipodozi aina zote unaviweka flame Moja au office tofauti.
3: Unafanya au umewahi fanya kazi/shughuli gani kabda?
4: Eneo/mji unao plan kufungua biashara zako.
5: Utasmama mwenyewe au utamuweka mtu?
Karibu sana mkuuHeshima yako naomba nikutafute pm