Msaada hatua za kufuata kabla sijaanzisha biashara

Location nzuri ndiyo silaha sina lingine, location nzuri unauza hata mavi.
 
na asije akachukulia poa kuna chuma ulete kuna kuwaloga wateja waje kuna kikinga biashara isitupiwe uchafu kuna ww mwenyewe kujikinga yaani ukienda kwa mganga asipokuambia lala makaburini basi hapo hajakupa dawa jiandae kuanguka kabla ya muda wako .
πŸ˜‚
 
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo hayo ya kina
 
Aksante! Kwanini kuna biashara zinahitaji lesseni na zingine hazihita? Na hiyo lesseni inapatikana wapi?
 
Aksante sana mkuu umeniongezea kitu kikubwa hapo
 
  • Natumaini mtaji unao
  • Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6
  • Tafuta TIN TRA
  • Lipa kodi
  • Tafuta leseni kwa halmashauri/manispaa/jiji
  • Weka mzigo dukani
  • Weka binti mrembo auze
  • Anza kuhesabu mapato
🀣 πŸ˜‚ Hiyo yapili kutoka mwisho nimeipenda asante sana kwa dondoo hizo
 
1. Mtaji nimedunduliza kwenye kilimo kwa kuwa kilimo ni cha msimu nilitaka nipate chanzo kingine cha mapato
2.Vitenge na vipodozi nataka viviweke sehemu moja kwa maana ya fremu moja
3. Shughuli ninayoifanya kwa sasa, sifanyi chochote nasubiri mpaka msimu wa mvua ufike niingie shambani
4. Eneo ninalotaka kufungua biashara ni miji mdogo ni halmashauri mpya imeanza 2014 mkuu
5. Kwa kuanza nitasimama mwenyewe nione mauzo yakoje
 
  • Natumaini mtaji unao
  • Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6
  • Tafuta TIN TRA
  • Lipa kodi
  • Tafuta leseni kwa halmashauri/manispaa/jiji
  • Weka mzigo dukani
  • Weka binti mrembo auze
  • Anza kuhesabu mapato
Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6...hii ni kodi ya fremu sio?.

Hiyo Kodi inayofuata hapo tena analipa ni ya nini? kama ni kodi ya mapato alipe kabla ya kupata?.
 

Leseni ya Vipodozi tunapata TBS siyo TMDA
 
Niko hapa nachukua madini toka kwa wachangiaji watukufu
 
Mimi naweza nikakupa hint kwenye vipodozi manake ndo nilipo na uzoefu

Kwanza Hiyo biashara Kwa kuiangalia ni rahisi ila ni very complicated

Inaangalia Mazingira yako
Hapa utagusa lifestyle ya wateja unaowatarajia
Kipato na hali ya hewa pia ni muhimu

Katika Vipodoz hasa vya wanawake kuna mambo Kama trend na uwezo wa kipodozi kuleta matokeo Kwa haraka

Kama wateja wako ni watu wa kiwango cha chini hakikikisha product yako ya ghali haizidi 20,000

Nyingi ziwe kwenye 3000-12,000 hivi na chache za 13,000-20,000
Katika hizi bidhaa Utakaangalia zaidi iliyopo kwenye trend fuatilia sana FB Kwa watu wa kundi hili


Kwa Wateja wa kiwango cha Kati changanya bidhaa mpaka za Bei ya 50,000 hivi

Hapa utawapata wengi wanaopenda kupendeza na bidhaa za bei za kati lakini pia uzijue vyema kulingana na trend
Hapa wanazingatia skin care routine tofauti kidogo na kundi la chini

Kundi la juu
Hapa utaweka bidhaa kwanza Kwa kuzingatia Brand kubwa kubwa mfano Laroche, CeraVe,Eliza Jones N.k

Hili ni kundi la watu wanaonunua bidhaa hata moja ya 100,000 bila tatizo
Kikubwa tu ionekane kwenye website kubwa kubwa huko iwe na reviews za kutosha.

Turudi kwenye kundi namba moja ambalo ndo WaTanzania wengi tupo
- hapa panapatikana bidhaa zinazofukuziwa na serikali
-hapa panapatikana bidhaa namba mbili(copy)

-pia kuna bidhaa nyingi zenye matokeo hasi kwa ngozi

-lakini pia ni kundi linalohitaji mtaji Mdogo zaidi

Ukishaelewa unahitaji kushikilia wapi karibu tuongezeane nondo
 
Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6...hii ni kodi ya fremu sio?.

Hiyo Kodi inayofuata hapo tena analipa ni ya nini? kama ni kodi ya mapato alipe kabla ya kupata?.
Atafanyiwa makadirio, na atakuwa analipa kila robo ya mwaka
 
Aksante sana kwa uchambuzi wako wa kina mkuu
 
Heshima yako naomba nikutafute pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…