Msaada: Hawala anataka tugawane mali

Ok ok ok, Basi pay her off ili asikusumbue Tena! Wengine huwa tunatamani kumwacha Kila kitu ili kuondoa ghasia, we bado unajishauri kumpa sehemu ya mlichochuma mpaka ushikiwe combo (mwanasheria/mahakana) ya Nini yote haya ya kujidhalilisha!
Acha ujinga wewe
 
Acha Basi kumpoteza mwenzio, usumbufu wote huo wa Nini! Mwanasheria atamlipa maneno! Sheria ya ndoa unaijua kweli we! We mpoteze mwenzio! Hapa mawili, mlipe au bariki ndoa, mengineyo utakuja Tena hapa ukilialia hasa akipata kocha mzuri huyo mkeo!
Mimi nimefanya kazi ustawi wa jamii na nimesimama mahakamani Mara kadhaa kutoa social inquiry report ya haya Mambo.

Kumbuka point of reference ya maamuzi ya Mahakama pia huchukuliwa kutoka kwa afisa ustawi. Hivyo ninaongea ninachokijua sibahatishi. Hizi kesi nimeziona nyingi na wanawake wanabwagwa mapema tu.

Hivyo Basi acha kujiweka Daraja moja na mimi. Wewe hata mahakamani sidhani hata umewahi kusimama ukimuelezea hakimu Hali halisi ya Jambo ili afanye maamuzi.

Hii issue Kama angekuwa amefunga nae ndoa na wamezaa ingekuwa serious ila hawajafunga ndoa na hawajazaa ni issue nyepesi sana. Hata hapo kwenye ujenzi inabidi atoe vielelezo kuwa alichangia tofali au mchanga. Kinyume na hapo inakula kwake. Mambo Ni mengi acheni kupigana uongo humu.
 
Ila watu bana Single maza hawezi kukupenda hata siku moja alikuja kwako kwa ajili ya maslahi mapana ya kwake na mtoto wake now anataka kuchuma mali asepe hahahaa.
Mnakoseaga sana, single parent tumewazalisha sisi, ni wanawake, wanahisia, wanaweza kupenda tena.
Wengine walibakwa, wengine waliliwa kimasihara mimba zikajaa
 
Ninacho jua mm sheria zinasema kama amekukuta na mali hizo sio mali za ndoa lakini pia kama hamjafunga ndoa huyo asikutishie tena hujazaa nae hawezi kukufanya chochote wewe hakikisha document zote ni mali yako unachoweza kufanya ni kumpa kifuta jasho tu lakini kwako hana haki yoyote tena huna mtoto nae acha uoga lakini na nyie vijana kwann unaishi na mke wa mtu?huyo ni mke wa mtu na ndio maana umemkuta na mtoto anataka kurudi kwa mume wako[emoji3]sasa
 
Kweli maana ata mamaake aliachwa hivyo hivyo anaishi mwenyewe mwenye.....kuanzia bibi MTU hadi mjukuu Ni ma(single mother's).....
Duu kwahiyo naye anaenda kuunga tela la masingle mother huenda ni karoho kao hawawezi kuishi na ndoa
 
Acha Basi kumpoteza mwenzio, usumbufu wote huo wa Nini! Mwanasheria atamlipa maneno! Sheria ya ndoa unaijua kweli we! We mpoteze mwenzio! Hapa mawili, mlipe au bariki ndoa, mengineyo utakuja Tena hapa ukilialia hasa akipata kocha mzuri huyo mkeo!
Kwahiyo aachane na kesi bali akasawazishe mambo ndoa iendelee, naye mama mkwe vipi kuingilia ndoa ya mtoto wake mpaka matusi? [emoji23][emoji23] kuna wamama wamepinda kweli
 
kwa mjibu wa sheria zipo ndoa za aina tatu,moja ndoa ya kiimani yaani kanisani au msikitini,pili ndoa ya bomani au serikali na mwisho ndoa ya kiimila hii ni lazima upate baraka za wazazi wa pande zote ikiwa ni pamoja na kulipa mahali .

kama mulipitia ndoa kati ya hizo tatu basi ana haki ya kudai mgawanyo wa mali ambazo mlichuma pamoja na si alizokuta. kikubwa simama kuwa huyo alikuwa rafiki wa kike sio mke maana ukisema alikuwa mke pia sheria inamtambua maana mkikaa zaidi ya miezi mitatu akipika na kupakua sheria inamtambua pia hivyo simama na kuwa alikuwa rafiki wa kike na hamkuwa na makubaliano yeyote ya kuishi pamoja bali ni kuchovya tu
 
Na kweli ndio maana nimemwambia hujazaa nae huna ndoa nae sasa anakuwaje mk sasa tatizo la watu wengi hata kama hujui mambo ya kisheria kuwa mdadisi japo kidogo vinginevyo utataabika sana kwenye hii dunia au nunua japo vitabu vya sheria
 
Na kama ameshaondoka kitu gani kitakachomrudisha kisheria?ana ushahidi wowote wa kupeleka mahakamani?
Mbona unaziruka "comments" zinazokupa majibu stahiki? Huyo mkeo kisheria, kama unataka aondoke sharti mgawane kilichopatikana tangu mlipoanza kuishi pamoja. Iko hivyo.
 
Naona bush lawyers mmekomaa kujaza uongo hapa. Hebu nenda kasome kifungu 160(1) cha Law of Marriage Act. Sijui hii miezi mitatu/ sita nyie watu mnaitoa wapi!?
 
Kama ni suala la kutunza wote wametunzana, mbona kiuhalisia wanawake mnakubali nyinyi ni wategemezi kwa ME, lakini mkikaa mbele ya halaiki mnaongea habari ya 50/50!
Achana na hayo....nimekumisije[emoji3531][emoji3531][emoji126]
 
Hata yeye ameuvuruga mtwangio wa mwenzako kwa miaka 3.
Na katika hiyo miaka 3 alikuwa anakula,anavaa,analala bure.
Kwa hiyo hapo ni ngoma droo kama ni muda wote wamepotezeana.
Hamna kitu kama hicho

Hivi unapochapwa bakora kinachoumia ni bakora au anayechapwa?
 
True huyu niliyenaye mwezi ujao naenda kwao..na hili ni funzo siku nikiamua kujenga nyumba nyingine kuanzia Kiwanja naandika jina la mzazi wangu na sitomshirikisha mke
Sasa kama utajenga uandike jina la mzazi sasa huyo mke wanini, si ukae bila kuoa tu huyo mke akae kwako kama back 3? Utakuwa bado mtoto haujakuwa, vipi wewe baba yako alikuwa akiandika majina ya babu yako na mama yako hana chake kwa baba yako? Acha utoto kuwa mwanaume!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…