Msaada: Hawala anataka tugawane mali

Msaada: Hawala anataka tugawane mali

mapenzi sio ugomvi bali ni starehe ya watu wawili. Kwani mapenzi aliumbiwa kufaidi mwanaume peke yake?unafahamu kwamba raha ya mapenzi anayoipata mwanamke ni mara 20 ya mwanaume?

Sasa ni kwa nini raha upate halafu bado ulipwe huo ni ujambazi
Hamna kitu kama hicho

Hivi unapochapwa bakora kinachoumia ni bakora au anayechapwa?
 
Teteteeee sidhani maana Mali ya mzazi Ni ya mtoto siyo mwanamke au ukoo ina maana akitangulia naikamata......nataka mke siyo jambazi.....
Na ndugu zako wakijua jina nila mzazi wenu, je tayari una watoto ukatangulia unawaacha vipi watoto wako! Ndugu zako unawaamini vipi, unazani watoto wanaozurura mtaani wazazi wao hawakuwahi kuwa na mali embu jifunze tena maisha ya ndoa
 
Wazazi wake wanajua wewe ndio mkwe wao, kukaa na mtu miaka mitatu hujazaa nae una tatizo ama ulikua huli...
 
Ni muda Wa miaka mitatu sasa umepita tangu tukutane na huyu binti yaani mwaka 2017 akiwa Single mother yaani ameisha zalishwa mtoto mmoja. Tukabebana hapa sokoni bila kwenda kwao tukayajenga tukakubaliana nikamchukua yeye na mtoto wake tukaanza maisha.

Alinikuta nina nyumba moja na Kiwanja hivi sasa kile Kiwanja nimejenga na tumehamia huko.

Sasa mtafaruku unaanzia pale tulipo kwazana na anataka kuondoka na Mimi ninataka kuachana naye maana visanga vimezidi na yeye anadai tugawane Mali tulizovuna wote kwa muda huo jamani wanasheria Msaada hapo kisheria imekaaje?
Huwezi kukwepa kugawana (hata kwa "fair play" ya kawaida tu, ukiacha sheria). Mmechuma wote, huwezi kumwacha mikono mitupu!

Mali mziweke mafungu matatu:
1. Ulizochuma wewe kabla hamjaanza kuishi pamoja.
2. Alizochuma yeye kabla hamjaanza kuishi pamoja.
3. Mlizochuma (ulizochuma na alizochuma) wakati mpo pamoja.

Namba 1 na 2, kila mtu anachukua chake. Namba 3, mnagawana pasu pasu.

Matunzo ya mtoto unaweza kuyadai kama ukitaka. ...kutoka kwa mama/baba wa mtoto (kwa kuwa hukuwa umemuasili huyo mtoto). Itategemea pia makubaliano yenu yalikuwaje kuhusu huyo mtoto. Kama kwa namna fulani ulizuia baba halisi wa mtoto asilete matumizi kwa mwanae, then sioni haki kwa wewe kudai. Na mna kokotoaje gharama za matunzo ya mtoto (Chakula? Malazi? Afya? Elimu?)
 
Namba 1 na 2, kila mtu anachukua chake
SMU hapo kama baada ya kuoana mali hizo ziliendelea kutumika kama mali ya ndoa kwa pamoja, basi ni mali yenu nyote. UNLESS there was a declaration /agreement kuwa mali kila mmoja alizokutwa nazo zisiwe mali za ndoa.... kuwe na MAANDISHI! Kuna kesi ngoja niitafute kwenye kabrasha langu nikupe uisome
 
Mimi nimefanya kazi ustawi wa jamii na nimesimama mahakamani Mara kadhaa kutoa social inquiry report ya haya Mambo.

Kumbuka point of reference ya maamuzi ya Mahakama pia huchukuliwa kutoka kwa afisa ustawi. Hivyo ninaongea ninachokijua sibahatishi. Hizi kesi nimeziona nyingi na wanawake wanabwagwa mapema tu...
Duuuh hakika Tanzania tunawatetezi naona kwa mbali muangaza waja pongezi Mkuu....ngoja nitakucheki PM unipatie vielelezo
 
Mnakoseaga sana, single parent tumewazalisha sisi, ni wanawake, wanahisia, wanaweza kupenda tena.
Wengine walibakwa, wengine waliliwa kimasihara mimba zikajaa
Mmmmh maybe kwa niliyoyaona Ni visanga aisee
 
Ninacho jua mm sheria zinasema kama amekukuta na mali hizo sio mali za ndoa lakini pia kama hamjafunga ndoa huyo asikutishie tena hujazaa nae hawezi kukufanya chochote wewe hakikisha document zote ni mali yako unachoweza kufanya ni kumpa kifuta jasho tu lakini kwako hana haki yoyote tena huna mtoto nae acha uoga lakini na nyie vijana kwann unaishi na mke wa mtu?huyo ni mke wa mtu na ndio maana umemkuta na mtoto anataka kurudi kwa mume wako[emoji3]sasa
Kweli bwana yaan ndo utafutaji huo nikaangukia hayo majanga
 
Huwezi kukwepa kugawana (hata kwa "fair play" ya kawaida tu, ukiacha sheria). Mmechuma wote, huwezi kumwacha mikono mitupu!

Mali mziweke mafungu matatu:
1. Ulizochuma wewe kabla hamjaanza kuishi pamoja.
2. Alizochuma yeye kabla hamjaanza kuishi pamoja...
Yaani akinizingua nakaba hapo hapo kwa mtoto kuanzia nywele hadi kucha......Ndala hadi kofia nataka
 
  • Thanks
Reactions: SMU
kwa mjibu wa sheria zipo ndoa za aina tatu,moja ndoa ya kiimani yaani kanisani au msikitini,pili ndoa ya bomani au serikali na mwisho ndoa ya kiimila hii ni lazima upate baraka za wazazi wa pande zote ikiwa ni pamoja na kulipa mahali . kama mulipitia ndoa kati ya hizo tatu basi ana haki ya kudai mgawanyo wa mali ambazo mlichuma pamoja na si alizokuta . kikubwa simama kuwa huyo alikuwa rafiki wa kike sio mke maana ukisema alikuwa mke pia sheria inamtambua maana mkikaa zaidi ya miezi mitatu akipika na kupakua sheria inamtambua pia hivyo simama na kuwa alikuwa rafiki wa kike na hamkuwa na makubaliano yeyote ya kuishi pamoja bali ni kuchovya tu
Kweli eeeeh??!... Ngoja na hilo naandika kwahiyo namuita rafiki Wa like siyo hawala eti....
 
Na ndugu zako wakijua jina nila mzazi wenu, je tayari una watoto ukatangulia unawaacha vipi watoto wako! Ndugu zako unawaamini vipi, unazani watoto wanaozurura mtaani wazazi wao hawakuwahi kuwa na mali embu jifunze tena maisha ya ndoa
Sijazaa naye Mkuu ....ila nilimkuta na mtoto
 
Sijazaa naye Mkuu ....ila nilimkuta na mtoto
Sasa mgawane mali za nini??? Hana mwanao wala nini yani huyoo ni kufukuza kama Mbwaa kokooo...labda kama uliandika jina lake kwenye hati ya nyumba au kiwanja bhasi kazi unayo ila kama haya jina lake halipo Kesho fukuzaa kama mbwa na hatakuwa na cha kufanyaaa.
 
Sasa mgawane mali za nini??? Hana mwanao wala nini yani huyoo ni kufukuza kama Mbwaa kokooo...labda kama uliandika jina lake kwenye hati ya nyumba au kiwanja bhasi kazi unayo ila kama haya jina lake halipo Kesho fukuzaa kama mbwa na hatakuwa na cha kufanyaaa.
Umefura kweli, lakini si waliishi kama mke na mme? Haijalishi hawana mtoto, wakati anajenga alikuwa anapikiwa anafuliwa stress zinapozwa naye, kiasi asimwache hivi hivi
 
Kuna kesi moja mke alikuwa anadai jiko la udongo, mpaka mwanaume akawa anashangaa hajui huko jikoni kama kuna jiko hadi la udongo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom