Msaada: Hii mimba imetokeaje?

mike2k

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
1,571
Reaction score
3,448
HELLO WA MMU
Jamani nina shida inanisumbua kichwa mpka na usingizi nimekosa...iko hivi wife wangu alijifungua 28/06/2016...baada ya mwezi mmoja na ka wiki mbili 15/08/2016 akchoma sindano ya kuzuia mimba...kuanzia hapo nikawa nagegeda kama kawaida.

sindano hii hufanya kazi kwa miezi mitatu kwa hiyo ingeisha matumizi 15/11/2016.kipindi chote hicho amekuwa akiona hedhi yake kama kawaida kila ifikapo...kila mwezi..mara ya mwisho nimesex naye 28/10/2016 niliondoka na kwenda masomoni na mwezi wa 11 ameona siku zake kama kawaida...

kinachonichanganya ni kwamba mwezi huu wa 12 hajaona siku zake...Jana kapima mwenyewe kajikuta ana mimba..na sasa hv anahisi kama mtoto anacheza..tarehe 15/11/2016 alichoma sindano nyingine ya kuzuia mimba....

wadau naombeni mnisaidie hapa ushauri....hii mimba imeingiaingiaje wakati mara zote hizo bleed ameona??na mara ya mwisho kulala naye bleed kaona...sasa baada ya mwezi ndo ananiambia ana mimba?

Naomba kujua je unaweza kuwa na mimba na hedhi ikatoka kama kawaida?mtoto tuliyeko naye ana miezi mitano
UPDATE

Yaani ukweli wa mungu huyu binti kuwa na mimba ni msala sana kwangu kiukweli anatakiwa arudi skul coz mtoto wa kwanza alimpatia skull.sasa mimi now najianda arudi shule mwezi wa kwanza alafu ndo ananiambia tena habari za mimba...yaani haipatani na akili kabisa...kwanza ndugu zake wataninyonga kwa maana hawatonielewa kabisa...hivyo hvyo na kwa ndugu zangu pia.....yaani hilo suala halitoeleweka kabisa kabisa....yaani mimi solution yangu kwake ni akubali tu aitoe kwa maana hamna namna yoyote shuleni lazima arudi...yaaani sijui nina nuksi ghan mimi JAMII NILIYOPO IKIJUA hii ni aibu ya mwaka...sijui nitaficha wapi sura yangu...nachanganyikiwa kabisa
 
Usishangae nilikua natumia pills za uzazi huku napata siku zangu kama kawaida kumbe ninaujauzito nilichanganyikiwa hua inatokea aisee.
 
Hata hivyo pengine wakati anachoma tayari alikua nimjamzito kama hadi mtoto alishaanza kucheza.
 
Kwani mimba ni tatizo mkuu?,jiandae tu kulea,
naona unasikitika sana
 
Hata hivyo pengine wakati anachoma tayari alikua nimjamzito kama hadi mtoto alishaanza kucheza.

Mungu amsaidie ajifungue mtoto akiwa mwenye afya na timilifu maana kama alichoma sindano na kuna kitu tumboni lazima period aliyokua anapata ni ya baadhi ya viungo vya mtoto ni mawazo yangu lakini hayo......
Washauri wa afya niliokutana nao wanasema si nzuri kwa afya hivyo vidonge au sindano zitumikazo kupanga uzazi.
 

Mkuu hata usiwaze, inawezekana kabisa, mfano mzuri mimi, Wife alipata hedhi na bado akawa na mimba ilibakia kidogo nimchenjie, sema nikatulizwa. Ila mtoto alipozaliwa hadi niliona aibu maana mtoto alifanana na Mimi kila kitu
 
Hakuna viungo vya mtoto vilivyotoka hapo, ile sindano ya depo provera ni manufactured hormones sawa na zile zinazozalishwa na miili yetu. Hakuna madhara yoyote kwenye embryogenesis.
 
Hata hivyo pengine wakati anachoma tayari alikua nimjamzito kama hadi mtoto alishaanza kucheza.
Nakubaliana na wewe kuwa wakati anachoma hiyo sindano tayari alishakuwa mjamzito. Kwani kucheza kwa mtoto ni around wiki ya 22 ya ujauzito yaani miezi mitano. Walitafuta kinga wakati mimba imeshatunga.
 
Reactions: nao
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…