Msaada: Hili tatizo limenisababisha nisivune mapapai huu ni mwaka wa 2 sasa

Msaada: Hili tatizo limenisababisha nisivune mapapai huu ni mwaka wa 2 sasa

Mbogo_beichee

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2021
Posts
237
Reaction score
623
Habari zenu wakuu. Naomba niende kwenye mada. Mim ni mkulima natokea Mpanda Katavi. Nimelima mwaka juzi zao la papai na kila mwaka wa mavuno hutokea hili tatizo la kuweka vidoti. Wakati papai linaanza kukua kisha hua kama kibarango ikifikia papai kua kubwa na huanza kuoza kabla halijakomaa vizuri.

Nitaweka picha hapo chini muone inavokua.

Msaada jamani
 

Attachments

  • Screenshot_20250509-120102.png
    Screenshot_20250509-120102.png
    1.1 MB · Views: 42
  • IMG_20250506_150607.jpg
    IMG_20250506_150607.jpg
    593.8 KB · Views: 42
  • IMG_20250506_150547.jpg
    IMG_20250506_150547.jpg
    501 KB · Views: 43
Sifaham sana kilimo hiki lkn si ungewasiliana na Bwana au Bibi shamba kwanza au tembelea maduka ya Pembejeo sometimes unaweza kukutana na wazoefu na wakakipa ushari
Mkuu jf ina wataalamu na wazoefu kuliko hata hao ma bwana shamba.

Kwa uzoefu wangu hizo mbegu sio sahihi
Yaani ni local seed za kukamua na matunda yake yalikuwa yameshaathirika tiyari.

Kingine papai huwa halipendi baridi sana sijui kuhusu mpanda kulivyo hali ya hewa ya huko.
 
kuweka vidoti. Wakati papai linaanza kukua kisha hua kama kibarango ikifikia papai kua kubwa na huanza kuoza kabla halijakomaa vizuri.
Tumia antifungal yenye kiambata cha copper oxychloride ukikosa tumia yenye kiambata cha mancozeb.
Ni vizuri kutumia mapema wakati wa maua, matunda madogo na yanapokaribia kukomaa.
 
Issue siyo mbegu, hapo issue ni magonjwa. Papai linahitaji sana kupiga dawa ya fungus na dawa za wadudu. Ukichelewa tuu hupati kitu
 
Nzi wa matunda huwa wanaharibu matunda kwa hiyo style. Jaribu kuyavuna na kiyateketeza hayo yalioharibika kisha kuna kitu kinaitwa mitego ya nzi. Sijui jina lake kitaalam ila inatrap nzi kabla hajadhuru tunda likiwa changa. Nahisi hao ni nzi wanasababisha hivyo. Natarajia kuanza kilimo hiki mwezi wa 9 niko kwenye maandalizi ya shamba baada y kutoa mahindi.
 
Mi kwangu milimao inakauka kama imepigwa jua kalii, sijui ugonjwa gani walahi
 
Sifaham sana kilimo hiki lkn si ungewasiliana na Bwana au Bibi shamba kwanza au tembelea maduka ya Pembejeo sometimes unaweza kukutana na wazoefu na wakakipa ushari
Bwana shamb hawapatikani kirahis nilipo. Ni polin sana. Mabwana shamba weng wapo mjin.

Maduka ya pembejeo nilienda mwaka jana wakanipa sum ila tatito lipo palepale
 
Mkuu jf ina wataalamu na wazoefu kuliko hata hao ma bwana shamba.

Kwa uzoefu wangu hizo mbegu sio sahihi
Yaani ni local seed za kukamua na matunda yake yalikuwa yameshaathirika tiyari.

Kingine papai huwa halipendi baridi sana sijui kuhusu mpanda kulivyo hali ya hewa ya huko.
Ooh maybe ni kwa sababu ya barid. Maana barid ipo
 
Tumia antifungal yenye kiambata cha copper oxychloride ukikosa tumia yenye kiambata cha mancozeb.
Ni vizuri kutumia mapema wakati wa maua, matunda madogo na yanapokaribia kukomaa.
Kwa sasa nimekubali hasara. Nataka nipruni matunda yote kisha nimwagilizie upya na kupuliza dawa bora zaidi. Naomb maelekezo zaidi ya hizo dawa na namna ya upuliziaji kwa muda (mara ngap kwa week).
 
Issue siyo mbegu, hapo issue ni magonjwa. Papai linahitaji sana kupiga dawa ya fungus na dawa za wadudu. Ukichelewa tuu hupati kitu
Naomba unisaidie dawa gani za kupuliza

Nataka nianze kukuza matunda upya
 
Nzi wa matunda huwa wanaharibu matunda kwa hiyo style. Jaribu kuyavun a na kiyateketeza hayo yalioharibika kisha kuna kitu kinaitwa mitego ya nzi. Sijui jina lake kitaalam ila inatrap nzi kabla hajadhuru tunda likiwa changa. Nahisi hao ni nzi wanasababisha hivyo. Natarajia kuanza kilimo hiki mwezi wa 9 niko kwenye maandalizi ya shamba baada y kutoa mahindi.
Asante ngoja nifatilie hicho kitegeo cha nzi
 
Kwa sasa nimekubali hasara. Nataka nipruni matunda yote kisha nimwagilizie upya na kupuliza dawa bora zaidi. Naomb maelekezo zaidi ya hizo dawa na namna ya upuliziaji kwa muda (mara ngap kwa week).
Wazo zuri kutoa mapapai yote yenye changamoto.
*Mancozeb tumia gram 2.5-3 kwa lita moja ya maji. Muda wa kurudia siku 14.
*Cooper oxychloride tumia gram 3 kwa lita moja ya maji. Muda wa kurudia siku 14 -21 kutegemea na mashambulizi.

Nimetumia kipimo cha gram kwasababu aina hizo za dawa zinapatikana zaidi kwa mfumo wa unga (WP), changanya unga wa dawa vizuri uhakikishe imesambaa vzr kwenye maji kabla ya kupulizia.

NB: usisahau sumu ya wadudu hasa hawa meal bugs tumia Dudu acelamectin inafanya vzr zaidi kwa wadudu wanaofyonza.
 
Back
Top Bottom