Msaada, Hivi inakuwaje ukinunua chombo cha moto, chenye madeni TRA nalipa mimi au analipa yule ambae ameniuzia

Msaada, Hivi inakuwaje ukinunua chombo cha moto, chenye madeni TRA nalipa mimi au analipa yule ambae ameniuzia

Wanakikamata...mwenye nacho ndio atahangaikia kukilipia ili akichukue...utalipa wewe ili uwe nacho huru kwa kukitumia, mwenzako hana shida nacho atakuzungusha tu, maana angekuwa na Nia njema angekuambia kabla ya kuuziana. Mshirikishe taarifa mwambie chombo kinadaiwa na kinatakiwa kilipiwe usikie jibu lake alafu Fanya maamuzi yako...kukubali hasara kwako
Kwani usajili unafikiri unasoma kwa nani wakati lazima deni hilo litakuwa ambatanisho na usajili wa mmiliki wa hicho chombo au hujui???
 
Kwani usajili unafikiri unasoma kwa nani wakati lazima deni hilo litakuwa ambatanisho na usajili wa mmiliki wa hicho chombo au hujui???
Tafsiri yake ni kwamba ameuziwa pamoja na deni, japokuwa hakuambiwa na huyo muuzaji
 
Hapo ndio nimekosea kwaiyo nafanya Nini sasa mana chombo kina deni LA jamaaa na hajanipa tax clearance certificate nafanyaje?
Mkataba ulioingia nae wakati wa ununuzi unasemaje? Madeni utalipa wewe au yeye? Au ndo ulinunua bila mkataba?
 
Mkataba ulioingia nae wakati wa ununuzi unasemaje? Madeni utalipa wewe au yeye? Au ndo ulinunua bila mkataba?
Nilininua na mkataba ila hakuna sehemu kwenye mkataba ambayo inaonesha nani atalipa madeni na hakuna kipengele cha madeni kwenye huu mkataba...

Yani mkataba hujaelezea deni lolote juu ya chombo hiki, japo yeye alisema hakidaiiwi..

Sasa nifanye Nini au nitumie njia Gani kumbana
 
Na kwanini ununue chombo kilicho na madeni? Yaani haukucheki kwanza au?
 
Nilininua na mkataba ila hakuna sehemu kwenye mkataba ambayo inaonesha nani atalipa madeni na hakuna kipengele cha madeni kwenye huu mkataba...

Yani mkataba hujaelezea deni lolote juu ya chombo hiki, japo yeye alisema hakidaiiwi..

Sasa nifanye Nini au nitumie njia Gani kumbana
Kama mkataba upo kimya hauongei lolote kuhusu wajibu wa muuzaji kwa matukio kabla ya kuuza gari huo mkataba una mapungufu.

Kama deni si kubwa lipa achana nae, kama ni kubwa pambana nae.

Jaribu kumharass, muonyeshae kuwa unaenda kumletea usumbufu mkubwa.

Unaanza na RB ya utapeli unamwambia kabisa nakufungulia mashtaka ya kunitapeli, apate wito kwanza polisi.

Tumia watu pia kumharass, wape watu namba wampigie pigie kwanini amekuwa tapeli, Iwe bandika bandua, mpaka abadili namba, akibadili anza kumsumbua shahidi wake, polisi vikao kila wiki muitwe.
 
Back
Top Bottom