Msaada huyu dada wajameni

Msaada huyu dada wajameni

Mbimbinho

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2009
Posts
8,328
Reaction score
7,784
Nimetoka kumeet na dada mmoja hivi, ananiomba ushauri, maana yeye hata hajui what to do. Nimeona niwashirikishe, in short mkasa uko hivi,

Huyu dada yupo na bf wake kitambo tu, yeye bado yupo university while her bf ana kazi nzuri tu katika kampuni moja ya simu kubwa nchini. five months ago alipata mimba bf wake akainsist sana waitoe mimba dada wa watu kwa shingo upande akaitoa. Sasa leo nilipokuwa naongea naye ameniambia kuwa ana mimba nyingine na bf wake yupo mad anataka abortion itake place. Mdada kagoma kutoa mimba anadai alipo abort first tym she's been feeling guilt. Binti hataki kwenda nyumbani na mimba pekee, unless wanaenda na jamaa kujitambulisha or harudi kabisa home maana home kwao nako hakupo gud. Alianza dada mtu kapata mimba nyumbani wakampokea kwa shingo upande mama pressure ikiwa juu kidogo, miez mi13 iliyopita mdogo wao wa mwisho naye kapata mimba mzazi nusura apagawe (mzazi ana kisukari) sasa now ni huyu wa katiati, yeye mwenyewe amepanga kutorudi nyumbani kuhofia kumuumiza zaidi mzaz wake. Mi nimemwambia asiporudi hom ndo atamuua mzaz wake bila chenga. Akanambia then hajui wat to do but hayupo tayar kuabort na kalia bati msimamo wake. Nimemwambia amwambie mchizi wake aende kujitambulisha kwao faster but msela hataki hiyo kitu( Binti kafikia kwa msela jijini na home kwao wanajua binti bado yupo chuo mkoani.)
Jamani msaada wa mawazo.., anatia huruma sana wandugu..
 
Daaaaa,athari za NGONO ZEMBE.....any way kam kujitambulisha kutaleta relief akajitambulishe,amsisitze sana
 
namuonea huruma sana kwani hakuona kuolewa na huyo jamaa...
 
Huyo mwanaume kwa nini hataki kwena kujitambulisha na kwa nini anataka demu atoe mimba! Hapo pagumu mwanzo alitoa ila hakujifunza!
 
Maji2 mengne bwana,inamaana lidada lizima la chuo kikuu haliwez jua kuwa huyo mchizi hana mpango nalo zaidi ya kulichezea 2!
 
kwan yeye hakujua madhara y kwenda peku peku ......atoe 2.
 
honestly mwenyewe nimempa kubwa bila kumkeepesha na kumwita mzembe na zezeta. Kinachokera ni kwamba she just aborted few months ago n now she z pregnant again.., na jamaa mwenyewe hataki kwenda kujitambulisha..!
 
mi watu wa hivo wala siwaoneagi huruma 2 be honest
 
akome analo hilo,ajiandae kuwa single mother na hivi hana kazi mbona ataipata pata!!!!
 
pumbavu, msomi gani asiejirekebisha? Mara ya kwanza tuseme ilikuwa kosa na ya pili tena? Kwanza story za arbotion msizilete kabsaaaa humu, kuna watu tumezaliwa tunaogopa dhambi, huyo kwa kitendo cha kukubali mawazo ya huyo tahira mwenzie ya kutoa mimba hata kama ni kwa shingo nyuma, namwona yuko primitive sana, azingatie

1. Kutoa mimba ni kuua(so yeye ni muuaji)
2. Kwenye mapenzi asikubali kuwa mtumwa, kitendo cha kujifanya anampenda sana msela wkt inaonyesha kabisa ni play boy na asie na mapenzi ya dhati kwake ni utumwa wa kishamba
3. Siku zote aitumie elimu yake cha kiwango alicho nacho!
4. Kama hamwelewi mshkaji ni bora akampiga chini kwani mwisho wa siku anaweza kuitafuta sumu.
Shauri lakeee!!!
 
kazi na dawa,mambo ya mimba yanaambatana sana na wanachuo cjui ni kwa nn? yan unakuta wanachuo wanamdaktari spesho for that matter. sku moja tulienda kwenye semina pale udsm nikawafumania akina dada wanabusha yupi daktari bingwa wa kutoa mimba.
bila shaka huyo mwachuo ni wa saut, ndo huwa wanakuwa wapuuzi namna iyo. yan umesoma mpaka unafikia chuo hujaweza kutambua yupo ni mwanaume muonga,
anaywaway nahisidada mtu,mdogo mtu na chakati nacho mimba. daaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah!kuna kitu kinazunguka apo kwao. mkuna kitu apo
 
Nkumbuka maneno ya JK kweli sazingine ni kiherhere mwazo katoa hakujifunza? navip hajmchuguza huyo mchati wake akjua kuwa hana mustakabali nae mwambie aende ustawi wa jamii akmshtaki asipo afiki kujitambulisha ndo tatizo la vijana mchezo wana taka majukum habebi
 
wanawake wengine bwana kaendelea kung'ang'ania. Sasa tumshauri nini wakati jamaa kicheche, kama anaona mimba inafichika sawa cjui ataficha na mtoto. .
 
Nkumbuka maneno ya JK kweli sazingine ni kiherhere mwazo katoa hakujifunza? navip hajmchuguza huyo mchati wake akjua kuwa hana mustakabali nae mwambie aende ustawi wa jamii akmshtaki asipo afiki kujitambulisha ndo tatizo la vijana mchezo wana taka majukum habebi
sa aende ustawi wa jamíi kwa ushahid gani alio nao wkt hata co wana ndoa?
 
Mbona wkt anamkatia msela mauno hakuja ku2omba ushauri?na ole wake atoe hyo mimba...2tadeal nae perpendicularly..
 
girlfriend analazimisha ndoa, mwisho wake itakuwa mateso tu. Hakuna haja ya kwenda kwa mtabiri mwingine. Mpe huu mstari autunze. God bless her.
 
Back
Top Bottom