Msaada: Inamaanisha nini kuona muda na dakika zinazofanana kila mara?

Mkeo atazaa mapacha
 
Kuwa makini maana ukiona dakika za majeruhi ujue unakaribia kufa
 
Ebu angalia saa sasahivi
 
Na mimi naongezea kuna jamaa yangu kaimeza saa yote kichwani.Ukimuuliza saa ngapi sasa hivi anakujibu saa nne na dk 38 ukicheki ni kweli .Hata ukimuamsha usingizini atakwambia hii saa tisa na dk 13 na ni kweli.Ni jini huyu sijui?!
 
Hii kitu imewahi kuwa inanitokea sana miaka flani hivi hapo nyuma. Yaani kila nikiangalia saa nakuta inafanana namba zote. Na ilikuwa inanitokea kwa siku hata mara nne. Naona siku hizi imekwisha
 
haya mambo usiyaapuze ndugu yangu. Hebu ngoja nikupe mfano wangu, ilikuwa inatokea hivyo kila saa 12.34 bila kujali ni mchana au usiku. nikaja kugundua ni ex wangu aliyekuwa ananifanyia manifestation. ikatokea tu siku moja tukaongea na akawa muwazi kwamba " I was manifesting you" nikajua ndio maana ya ile. Na ili kuthibitisha, kila nikiiona 12.34, najua ni yeye na mimi nampotezea, muda si muda, nikapigiwa simu na polisi muda huo huo 12.34 kwamba huyo demu kapatwa na majanga fulani.

Pili, huwa sina kawaida ya kuamuka usiku saa 9, ikatokea week 6 mfululizo naamka mido hiyo. Ikaja kutokea kumbe mama yangu alikuwa anaamka usiku huo kuanza kuniombea. Aliniambia yeye mwenyewe bila kumuuliza.
Sasa connect the dot na watu wa karibu yako, Utapa tu majibu.
 
MAANA YA NAMBA HIZI ZA MALAIKA (ANGELIC NUMBERS)

11:11 - weka nia zako pindi unapoziona namba hizi zikijirudia rudia kwako! Zingatia fikra zako na uwe na mawazo chanya yaani mawazo mazuri. Mungu anafanya kazi na wewe kukuletea yote mazuri unayotamani kwa wakati huu

12:12 - jitayarishe kuyaondoa mabaya yote maishani mwako. Mwenyezi Mungu anakusaidia kusafisha na kuyaondoa yote ambayo hayakunufaishi tena maishani mwako iwe watu au vitu

3:33 - uko salama na unalindwa, ondoa wasiwasi wako uliokuwa nao na ufuate ndoto zako utimize matamanio yako

4:44 - malaika wako wapo karibu na wewe, unalindwa na kuongozwa. Pia ni ishara kuwa haja zako zitatimia

5:55 - mabadiliko mazuri yanakuja. Kutakuwa na mabadiliko makubwa mazuri katika maisha yako, jitayarishe. Kitu kipya kizuri kinakuja

111 - amini hisia zako na usikilize moyo wako

222 - upo mahali sahihi, ondoa wasiwasi wako

333 - malaika wako wanakusaidia

666 - ni wakati wa kujitafakari na kutathmini kile kinachoendelea maishani mwako

777 - bahati iko upande wako. Mambo mazuri yapo karibu kutokea

888 - kila kitu kitakuwa sawa kwako. Pesa zinakuja

999 - achana vitu au watu ambao hawakunufaishi tena maishani mwako

000 - una uwezo wa kuunda au kukikamalisha chochote unachokitaka

Naam ulimwengu wa kiroho hauwezi kuwasiliana na wewe kwa njia hizi za duniani huku kuzungumza ana kwa ana au kupigiana simu.

bali ulimwengu wa kiroho unazungumza na sisi kupita ishara, ndoto, alama, mbalimbali ikiwemo hizi za namba zinazojirudia rudia kila wakati, manyoya, mawingu, harufu ya perfume nzuri, wanyama, ndege, mimea, mwanga (Nuru) n.k.

Leo tupo kwenye hizi namba za malaika ambapo ikitokea ukakutana na namba hizi mara kwa mara basi ujumbe wako ndio huo kama nilivyoutafsiri hapo.

Namba hizi unatakiwa uzione zaidi ya mara 3 ndipo zitakuwa zimekusudiwa kwako. Namba unaweza kuziona kupitia namba za mwisho za simu unazopigiwa, kwenye saa wakati unaangalia muda, kwenye namba za vocha, kwenye mita band za radio (frequency), plate number za magari, kwenye comments na likes humu mitandaoni, risiti za malipo, na sehemu yoyote nyingine ambazo utaweza kukutana na namba hizi.

Suhendra haya tayari
 
HHahahaha
Na mimi naongezea kuna jamaa yangu kaimeza saa yote kichwani.Ukimuuliza saa ngapi sasa hivi anakujibu saa nne na dk 38 ukicheki ni kweli .Hata ukimuamsha usingizini atakwambia hii saa tisa na dk 13 na ni kweli.Ni jini huyu sijui?!
Hahahaha hiyo kali
 
Reactions: EEX
Nitaanza kulifanyia kazi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…