Msaada: Inamaanisha nini kuona muda na dakika zinazofanana kila mara?

Habari wadau?

Kwa muda mrefu sana kuna jambo huwa limekuwa likijitokeza mara kwa mara kwangu, kwamba mara nyingi nikiwa naangalia majira kwenye saa ya mkononi au simu nakuta masaa na dakika zinafanana.

Mfano 02:02, 10:10, 20:20, 15:15 N.k, yaani naweza kujiuliza hivi saa hivi saa ngapi saa? Nikangalia saa nakuta 12:12 au 05:05 kutegemea na majira ya muda huo.

Au nasema ngoja nikaangalie mazoezi uwanjani naangalia saa 17:17, 18:18, ngoja niamke nijiandae kwenda ofisini nikicheki saa 06:06.

Naombeni msaada wa ufafanuzi kuangalia saa nakukuta masaa na dakika kufanana ina maana gani kiroho, kiakili, kimaisha?

Ahsante.
Angel numbers..zina maana yake....google
 
Hizo ni namba za kimalaika, unapewa taarifa kuwa mambo yako yanaenda BAM BAM.

Mimi kuna kipindi nilikuwa naziona hizo namba za kufanana kila siku, nikaanza kuona mambo yangu yananyooka balaa, kila nikigusa imoo, nikigusa imooo....

Usipuuzie, ni ujumbe wa kukuelekeza jambo.
 
Wanaziita angel hours. Eti wanasema ukiona hivyo ujue malaika wako wa ulinzi anakupa uhakika kwamba mko pamoja. And if you look closely, utagundua mambo yako yanakwenda vyema
Asee inaweza kuwa Kuna ukweli, na ina wezekana hapa duniani Kuna vitu vingi sana vinatokea ikiwa na maana zake.
Mimi huwa inatokea siku kufanana, hata siwezagi kuelezea hii scenario, yani unakuwa sehemu tofauti lakini matukio yanafanana kila kitu na siku nyingine.
 
Hizo ni namba za kimalaika, unapewa taarifa kuwa mambo yako yanaenda BAM BAM.

Mimi kuna kipindi nilikuwa naziona hizo namba za kufanana kila siku, nikaanza kuona mambo yangu yananyooka balaa, kila nikigusa imoo, nikigusa imooo....

Usipuuzie, ni ujumbe wa kukuelekeza jambo.
Amina Mkuu na iwe hivyo inshallaah
 
Nilisoma darasa moja la mambo ya spiritual wanasema ni angel number Kila namba Ina maana nowdays nimesahau 😀😀
 
DUU NAMI WEEKI HII NZIMA NIMEKUWA NAKUTANA NAMBA ZENYE MAGARI MFANI ALHIMISI ANTOKA TU HOME 666 KATKAKATI YA SAFARI 333 NAFIKA JOB 222 DUU NIKASHANGAA NARUDI HOME 222 KISHA 777.LEO SASA NIMEKUTANA NA 777 NA 333 HII IMEKAAJE ?
 
Habari wadau?

Kwa muda mrefu sana kuna jambo huwa limekuwa likijitokeza mara kwa mara kwangu, kwamba mara nyingi nikiwa naangalia majira kwenye saa ya mkononi au simu nakuta masaa na dakika zinafanana.

Mfano 02:02, 10:10, 20:20, 15:15 N.k, yaani naweza kujiuliza hivi saa hivi saa ngapi saa? Nikangalia saa nakuta 12:12 au 05:05 kutegemea na majira ya muda huo.

Au nasema ngoja nikaangalie mazoezi uwanjani naangalia saa 17:17, 18:18, ngoja niamke nijiandae kwenda ofisini nikicheki saa 06:06.

Naombeni msaada wa ufafanuzi kuangalia saa nakukuta masaa na dakika kufanana ina maana gani kiroho, kiakili, kimaisha?

Ahsante.
Angelic numbers
 
Back
Top Bottom