Msaada indicator ya gari ABS imewaka

samilakadunda

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
1,780
Reaction score
355
Naomba ufafanuzi wa taa ya ABS Imewaka hata sijui gari ina shida gani. Nimejaribu kugoogle nimepata maelekezo ila nahitaji msaada wa watalaamu zaidi.

Nini madhara ya kuendesha gari taa ikiwa inawaka?
 
ABS ni kifupi cha anti breaking system,taa inapowaka unaweza kuta ni brake fluid imeisha au cable zake zina tatizo.
 
Ni marekebisho tu, matatizo madogo ambayo hayakuzuii kuendesha gari na haina madhara yoyote, ila ni vyema ukacheck kwa mtaalamu, labda ni waya tu umeachia au umegusa sehemu, au switch imenasia
 
nashukuru kwa ufafanuzi nitaenda kwa mafundi kesho, gari ni noah
 
Gari yako aina gani? Kabla cjakupa ushauri kifundi zaidi
 
Fungua tyre za mbele kuna nyaya utaziona zinatoka hapo chini kwenye tyre zinapanda juu,hzo zitakua zimekatika nadhani japo husemi ni gari aina gani ila kuwaka taa za ABS hata kama unaenda bondeni kwa tata madiba ndo utengeneze nenda tu
 
nimesema ni noah wakuu nashukuru kwa ufafanuzi wenu
 
Ni marekebisho tu, matatizo madogo ambayo hayakuzuii kuendesha gari na haina madhara yoyote, ila ni vyema ukacheck kwa mtaalamu, labda ni waya tu umeachia au umegusa sehemu, au switch imenasia

ndugu yangu swala la break system cio dogo wala la kulichukulia poa linaweza kuleta balaa
 
mkuu kama ni Noah box kitakacho fuata baada ya hapo ni kuwa Gari lazima itaanza kutobadili gia.
na matokeo yake Gari lazima itakuwa inakula MAFUTA sana.

hayo yote ni kuwa Gari yako kwa upande wa Noah speed meter inaendeshwa na sensor za ABS.

na Noah huwa inamtindo wa kujilock system hiyo ya ABS.

MKUU kama upo dar ni chek 0717228064 kwa msaada zaidi hata ukitaka nitakurekebishia tatizo lako maana ndio kazi yangu mm ni FUNDI UMEME na tatizo hilo ni la UMEME.

tutasaidiana ki JF .au ukitaka nakupimia na kukwambia shida yako ni nini
 
Fungua tyre za mbele kuna nyaya utaziona zinatoka hapo chini kwenye tyre zinapanda juu,hzo zitakua zimekatika nadhani japo husemi ni gari aina gani ila kuwaka taa za ABS hata kama unaenda bondeni kwa tata madiba ndo utengeneze nenda tu

mkuu ushauri wako sio mzuri sana kabisa.kwa Gari nyingine taa ya ABS ikiwaka shida huwa kubwa sana.na ukiendelea kuendesha unazidi kufanya uharibifu zaidi .kama kuharibu gearbox n.k

hasa huwa inategemeana ni aina gani ya gari
 
Hapa sjaelewa kitu wakuuu,huyu anasema gear box mwingine anadai ni Brec tuamini kipi hapa?
 
Hapa sjaelewa kitu wakuuu,huyu anasema gear box mwingine anadai ni Brec tuamini kipi hapa?
ABS ni Brake system, Gearbox kuharibika ni matokeo ya Brake na mfumo wake kuharibika.
ABS haiwezi haribu Gearbox direct!.
 
Hebu zima gari tuone kama inaendelea kuwaka
 
Muhimu nenda kwa fundi umeme wa magari wataipima na kugundua mara nyingi ni senser hizo zimekufa au zimekatika au bearing imechoka lakn usibadili tu bila kupima kwa ufasaha ukipima ni simple zaidi
 
ABS ni anti-lock braking system, hii system kazi yake ni kuzua locking-up ya matairi pindi unapofunga brake kwa nguvu (hard braking) hapa inakufanya usipoteze control ya steering pindi unapofunga brake ya nguvu, ambapo system hii inafanya tairi zifunge brake kwa vituo(yaan zinashika na kuachia zinashika na kuachia) hii inakupa room kama dereva kuweza kuliko control/maneuver gari kipindi umefunga brake kali, na pia inazuia gari kuteleza(skidding) wakati wa brake kali. Sasa hii system inafanya kazi kwa kutumia speed sensors zilizopo katika tairi zote za gari husika hzi sensors zina monitor speed rotation ya kila tairi individually, hvo ikitokea sensor yoyote haileti taarifa kwenye computer ya gari (ECU/PCM) basi taa ya ABS itawaka. Kwa hapa bongo unaweza kuta ulikwenda kwa fundi kubadilisha brakepad/brake shoe, au cv joint, au kubadili bearing, wakasahau kuurudishia waya hvo taa ikawaka au actuator motor au solenoids ndani ya ABS box imekufa, au wiring ya system imepata itirafu kama fuse kuungua. So nn hutokea pale taa ya ABS inapowaka: ni hvi mfumo wa brake za gari zinazotumia brake fluid inapotokea abs system haifanyi kazi, automatic gari inajipeleka kwenye mfumo wa kizaman wa brake ambapo mfumo huo ulikua ukikanyaga brake kali tairi itajiburuza na na kukufanya ukose control ya steering yako, na gari inaweza kukuamisha yenye ikakupeleka kwingine, lakin pia ABS isipokua inafanya kazi kunaweza kukawepo na uneven braking pressure katika matiri,,, yaan ndo ile unakuta mtu unafunga brake nzito alafu kati ya tairi nne ni moja tu ndo inafunga nyingne zinatembea (ABS distributes even brake pressure to all tyres).

Ila kujua zaidi tafuta mtu mwenye OBDII scanner akupimie kuweza kujua actual problem iliyopo kwenye system yako..angalizo..kuna mafundi washenzi anaweza ichomoa bulb ndani ya dashboard inayo illuminate ABS ukadhan katatua tatizo kumbe kaondoa bulb.

Labda pia ngependa kuku-uliza hyo ABS inayowaka je na taa ya Parking brake/emergency (Wengine wanaita handbrake) inawaka pia?
 
Mkuu umejibu thread ya mwaka 2015[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]...nahisi jamaa hata hilo gari hana saa hizi!
 
Sometimes hizo wire huwa zinachubuliwa na Tyre kama hazijabanwa vizuri,Kila mtu akiangalia gari atagundua hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…