ABS ni anti-lock braking system, hii system kazi yake ni kuzua locking-up ya matairi pindi unapofunga brake kwa nguvu (hard braking) hapa inakufanya usipoteze control ya steering pindi unapofunga brake ya nguvu, ambapo system hii inafanya tairi zifunge brake kwa vituo(yaan zinashika na kuachia zinashika na kuachia) hii inakupa room kama dereva kuweza kuliko control/maneuver gari kipindi umefunga brake kali, na pia inazuia gari kuteleza(skidding) wakati wa brake kali. Sasa hii system inafanya kazi kwa kutumia speed sensors zilizopo katika tairi zote za gari husika hzi sensors zina monitor speed rotation ya kila tairi individually, hvo ikitokea sensor yoyote haileti taarifa kwenye computer ya gari (ECU/PCM) basi taa ya ABS itawaka. Kwa hapa bongo unaweza kuta ulikwenda kwa fundi kubadilisha brakepad/brake shoe, au cv joint, au kubadili bearing, wakasahau kuurudishia waya hvo taa ikawaka au actuator motor au solenoids ndani ya ABS box imekufa, au wiring ya system imepata itirafu kama fuse kuungua. So nn hutokea pale taa ya ABS inapowaka: ni hvi mfumo wa brake za gari zinazotumia brake fluid inapotokea abs system haifanyi kazi, automatic gari inajipeleka kwenye mfumo wa kizaman wa brake ambapo mfumo huo ulikua ukikanyaga brake kali tairi itajiburuza na na kukufanya ukose control ya steering yako, na gari inaweza kukuamisha yenye ikakupeleka kwingine, lakin pia ABS isipokua inafanya kazi kunaweza kukawepo na uneven braking pressure katika matiri,,, yaan ndo ile unakuta mtu unafunga brake nzito alafu kati ya tairi nne ni moja tu ndo inafunga nyingne zinatembea (ABS distributes even brake pressure to all tyres).
Ila kujua zaidi tafuta mtu mwenye OBDII scanner akupimie kuweza kujua actual problem iliyopo kwenye system yako..angalizo..kuna mafundi washenzi anaweza ichomoa bulb ndani ya dashboard inayo illuminate ABS ukadhan katatua tatizo kumbe kaondoa bulb.
Labda pia ngependa kuku-uliza hyo ABS inayowaka je na taa ya Parking brake/emergency (Wengine wanaita handbrake) inawaka pia?