MrGeneous
JF-Expert Member
- Oct 3, 2020
- 562
- 285
"Kujiunga na Jeshi' kauli yako utata wake umeanzia hapo.
Neno Jeshi ni pana .. kuna jeshi la polisi, zimamoto, uhamiaji,magereza , jwtz, Jkt..
Kila kimoja wapo kina utaratibu wake katika kujiunga ila kiufupi majeshi yote hapo juu yapo wizara ya mambo ya ndani ukitoa (JWTZ na JKT haya yapo wizara ya ulinzi).
Hayo ya mambo ya ndani utaratibu huwa wa kituma maombi kama kilichofanyika majuzi hapa.
JKT na Jwtz ndipo swali lako limejikita nadhani .. kupita ngazi za mtaa ni raia anayependa kujiunga mafunzo ya JKT hivyo lazima utambulisho wake wa kimakazi utambulike katika serikal za mitaa.. mwenyeki / diwan wako lazima akupe barua ya kukutambulisha ngazi za juu kuwa bwana Abrah ni mkazi, kata hvyohivyo, wilayani huko pia ndiko usauli unafanyika na vipimo vya afya kisha majina yatakayo fuzu watapangiwa katika vikosi vya JKT.
Kuingia JWTZ maranyingi huchukua waliomo katika makambi ya JKT kwa kujitolea au wanafunz wa kidato cha sita wanaopelekwa kwa mujibu wa sheria.
Wenzangu wanaweza kukazia ambapo sijatolea maelezo vzur.
Sahihi....kwa kuongezea jwtz wakitaka specila course mara nyingiii huaga wanakuja kuchukua uraiani ko wanatoa tar ya usaili mnaenda kufanya usaili pale kurasini kwenye kambi yao ya jwtz