Msaada jamani namna ya kulea kichanga cha wiki moja

Msaada jamani namna ya kulea kichanga cha wiki moja

Idimulwa

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2011
Posts
4,944
Reaction score
2,459
Mama yake kajifungua kwa operation na kufariki Dunia,alikuwa dada yangu ,kwa sasa kanatumia maziwa ya unga Lactogen 1.Naomba jamani kama kuna mbinu zaidi za kitaalamu zenye kuniwezesha kumkuza huyu mtoto mnijuze hapa.

Mie sitajali gharama ..nataka nipambane kwa namna yeyote anko akue huenda akanifuta machozi mbeleni.

Ee Mungu nisaidie pia.
 
Pole Sana Mkuu Na Hongera Kwa Kuwa Na Ubinadamu Wa Namna Hiyo.Ngoja Wataalam Watakuja Kwa Ajili Ya Ushauri Sahihi Kabisa.
 
Hakikisha anapata lishe nzuri ( hayo maziwa ya unga), usiache kumpeleka clinic ili upate ushauri wa kitaalam. Jitahidi asiumwe na mbu kumuepushia malaria. Kila la heri Mungu akukuzie
 
Kaka google kuna majarida mazuri online yatakusaidia na video youtube zipo
 
Hakikisha anapata lishe nzuri ( hayo maziwa ya unga), usiache kumpeleka clinic ili upate ushauri wa kitaalam. Jitahidi asiumwe na mbu kumuepushia malaria. Kila la heri Mungu akukuzie

Ubarikiwe mkuu Mfa maji
 
Last edited by a moderator:
Pole mkuu na hongera kwa kua na utu..MUNGU atakusaidia utamkuza tu..hakikisha anapata lishe nzur na kumlaza katika mazingira saf.
 
Kwa ss maziwa tu ndo mhimu...na usafi wake kuwa mwangalifu nguo zake zipigwe pasi kabla hajavalishwa zikishafuliwa....
Umri huo akilia ni njaa, usingizi au kakojoa anajitaji kubadirishwa zaidi ya hapo labda anaumwa....
Mungu akutangulie, roho imeniuma ila.Mungu atakusaidia
 
Pole sana mkuu,
Mungu Akubariki sana kwa jukumu ulilolichukua la kulea mtoto wa dada yako, na hasa kwa kuwa bado ni mchanga.
Hakuna formula ya ulezi, lakini ninaamini ya kuwa watu wengi humu jamvini na nje ya jamvi hili watakuwa tayari kukupa ushauri kwa kila hatua. Faraja pekee utaipata kutoka kwa Mungu Mwenyewe, naye Atakuongoza katika kumlea malaika huyo. Ushauri zaidi ni kuomba bila kukoma, kila wakati na kila mahali. Kila unapoona changamoto mwite Bwana naye Atakuitika! Ubarikiwe sana!
 
Mkuu Mungu atakulipa kwa wema unaoufanya kwa huyo kiumbe....mungu akutie nguvu na usivunjwe moyo na mtu kwenye safari yako ndefu uliyoianza...
 
Mama yake kajifungua kwa operation na kufariki Dunia,alikuwa dada yangu ,kwa sasa kanatumia maziwa ya unga Lactogen 1.Naomba jamani kama kuna mbinu zaidi za kitaalamu zenye kuniwezesha kumkuza huyu mtoto mnijuze hapa.

Mie sitajali gharama ..nataka nipambane kwa namna yeyote anko akue huenda akanifuta machozi mbeleni.

Ee Mungu nisaidie pia.

Pambana na mbu huyo ni adui namba moja.pili muepushe na feni ni hatari kwa kichanga.jitahidi kuwa makini usije kumlalia usiku pia mwangalie usije kumfunika vibaya akakosa pumzi. Vichanga wengi husumbuliwa na mafua so epuka vumbi na feni pia husumbuliwa na na gesi mwone dkt atakueleza namna ya kumtoa gesi.mungu akukuzie
 
Pole sana mkuu. Mungu ni mwema atakusaidia. Fuata ushauri uliotolewa na wadau hapo juu.
 
Hongera sana. Usiache clinic ya watoto zingatia chanjo. Usisite kujieleza mbele ya manesi wakupe ushauri.
Ukihisi dalili yoyote, Trust your insticts na kuwahi hosp.
Usafi shibe na mapenzi na sala.
Mungu akukuzie.
Mfundishe mapema kulala na kula kwa wakati unaoshauriwa
 
Blsd a lot
Pambana na lactogen mkuu mpakakieleweke otherwise jitahidi uendenqe hospital wakupe siku za chanjo ni muhimu dnt miss nimeendasana ..kingine simamama na Maombi Mungu atakuinua
 
Kwa ss maziwa tu ndo mhimu...na usafi wake kuwa mwangalifu nguo zake zipigwe pasi kabla hajavalishwa zikishafuliwa....
Umri huo akilia ni njaa, usingizi au kakojoa anajitaji kubadirishwa zaidi ya hapo labda anaumwa....
Mungu akutangulie, roho imeniuma ila.Mungu atakusaidia

Umemaliza, mm mke wangu alijifungua akaenda shule, toto limekua kwa lactogen mpaka leo lina akili sijawah kuona. USAFI MUHIMU
 
Nunua daftari andika weight kila ukipima uzito ingawa itakuwepokwenye kadi
 
Ooooooiiiiii, maskini pole sana na mwenyezi mungu atakulinda kwakumlea yatima wallah huto adhirika, akikisha anapata sindano Kama ulivyo, kula Kama kawaida... Ni msichana au Boy? Mnaishi dar?
 
Back
Top Bottom