Msaada je,kesi iliyofutwa inaweza kurudishwa tena??

Msaada je,kesi iliyofutwa inaweza kurudishwa tena??

Lukaku Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2017
Posts
843
Reaction score
740
Naomba ufafanuz ktk hilo na Kama ndio ni aina zipi za kesi ambazo zikfutwa yaweza zkarudshwa mahakaman!?

Natanguliza shkrani na Kama kutakuwa na Maelezo zaidi ntajibu na kufafanua zaidi
 
Naomba ufafanuz ktk hilo na Kama ndio ni aina zipi za kesi ambazo zikfutwa yaweza zkarudshwa mahakaman!?

Natanguliza shkrani na Kama kutakuwa na Maelezo zaidi ntajibu na kufafanua zaidi
Kesi za madai zinaweza kurudishwa mahakamani kama zikifutwa. Kesi inayofutwa kwa hiari ya mdai inaweza kurudishwa ikiwa mdai aliomba kufuta kesi yake lakini pia akaomba ridhaa ya kuirudisha mahakamani baadae. Hapa ni lazima muombaji aombe ridhaa ya kurudisha kesi. Mahakama ikikubaliana nae basi kesi hiyo huondolewa kwenye register ya kesi, na pindi muombaji akitaka kuirejesha kesi hiyo basi atapeleka mahakamani maombi na mahakama itarejesha kesi hiyo na itaendelea. Hata hivyo kama kesi ilishafikia katika usikilizwaji wa mashahidi haitakubalika kurudishwa tena.

Pia kesi iliyofutwa na mahakama kwa sababu ya mdai kutohudhuria mahakamani inaweza kurejeshwa. Mdai lazima apeleke maombi mahakamani ndani ya siku 30 akiomba mahakama kuirejesha kesi yake. Mahakama itapitia maombi hayo na ikiona inafaa na kuna sababu maalumu basi kesi hiyo itarejeshwa.

karibu
 
Asante Sana ndg dragon

Kesi hii ilkuwa imebaki hukumu tu na basi nikaongea na mlalamikaji aifute then tulipane
Na hakimu akanipigia kudhibitasha kuwa mlalamikaji atalipwa lkn pia hakimu akasema "mlalamikaj anaouwezo Wa kuirudasha kesi endapo tu sitomlipa"
Niltaka kuhakik Kama ni kweli au Hakim alikuwa anajarbu kunitishia tu....
By the way kesi ni ya madai
 
.
Mkuu hapo hakimu alikuwa anakutisha tu. Kesi kama yako inaitwa settlement out of court. Hapa inakuwa hivi, wenye kesi wanapatana nje ya mahakama, na wakishapatana wanaitaarifu mahakama kuwa wamepatana. Kwa hatua hiyo mahakama hulifunga kabisa faili la kesi, na kesi inakuwa imeisha. Hakuna hata mmoja kati ya wadaawa atakayeruhusiwa kuomba kurudisha kesi mahakamani tena, hata kama masharti mliyopatana yameshindwa kutimizwa.

Kwa kesi yako mkuu hakimu alikuwa anakutishia tu. haitawezekana kesi hiyo ifufuliwe tena, na kama upande mmoja utaamua kuendelea na mgogoro huo basi itabidi kufungua kesi nyingine upya, na hapa pia vigezo na masharti ya kisheria lazima yazingatiwe, maana si kila kesi hukubaliwa kufunguliwa mahakamani wakati kuna kesi nyingine inayofanana na hiyo ishafunguliwa, hata kama ilikwisha.
 
Daa mkuu ngoja niiandike full story ya kesi hyo hapo baadae then utafafanua kwa kina
 
Kwahiyo wewe unaonekana unataka kufanya ujanja janja, kwa nini usimlipe mwenzio? Mlipe bhana mambo yaishe.
 
Wewe jamaa mwenzio kafanya uungwana kufuta kesi mahakamani ili umlipe lakini kuna dalili zote kuwa unataka kuyeyea
 
Nmefanikiwa kumtoa gerezan six months kesi yke ilikuwa inalindma but now he is free (baba mdogo) mlalamikaj mama yke mdogo!! Ipo hivii.........
Mama yke mdogo alimuita wakae pamoja, pamoja na familia yke baba mdgo baada ya hapo baba mdogo akauza mashamba yake na ardhi aliokuwa anamiliki ili akaishi na mama mdg hyo maisha yakaendelea vzr tu Mara ghafla mama yke mdg akavunjika mguu kwa ajali then ktk kutibiwa huku na kule baba mdgo akaanza kuuza Mali za mama yke mdgo (_ng'ombe,mbuzi ,nafaka +vyakula)
Mama akaznyaka zote hzo soo akaenda kutaifisha vilpouzwa vyote
Waliotaifishwa wakamsaka muuzaj wao Mara paa ndani..
Walalamikaj wakawa wengi ikawa nan sasa afungue kesi???
Busara za Hakim kuamua kuwa mama yke mdg afungue file moja ili atakapolpa wote watapata kupitia kwa mfungua file huyu...
Nimeenda likizo ya mwez Wa kumi/2017 nkakuta hyo kesi then nmerud chuo nkaisimamia nkaongea na walalamikaji wanaopitia mgongo Wa mama yke mdogo then tukafikia maafikiano kuwa tutawalipa mwez Wa tatu hivo basi ndg yngu awe huru mm ntasimamia malipo hayo(takribani million moja) wakakubal sasa ikabaki mfungua kesi kwenda kuifuta siku hyo anaifuta hakimu akaongea na mm kupitia simu ya mama mdg kuwa "*mlalamikaji anaweza kuirudisha kesi pindi tu km hajalipwa*"
Ndio maana nkaulza inawezekana?
-----> shukrani kwa Maelezo ya ndg dragon

Sina maana nataka kumtapeli hyo mama Bali niltaka kujua juu ya kauli ya HAKIMU tu
 
Back
Top Bottom