Msaada;jinsi ya kuondoa hofu na kujiamini

Msaada;jinsi ya kuondoa hofu na kujiamini

jakaeama

Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
23
Reaction score
2
Msaada tafadhari,mi ni mwanafunzi nahitaji nijiamini katika masomo yangu ili nifanye vizuri
mara nyingi huwa najawa na hofu na kujiona nishafeli ninapomuona mtu kasoma topic ambayo mi sijasoma
hofu hii huwa nipo nayo muda wote na muda mwingi huwa nafikiria tu nashindwa hata kuchukua hatua na hatimae nafeli kweli
naombeni mnisaidie jinsi ya kufanya niondoe hii hofu maana nimejaribu mwenyewe lakini nimeshindwa na dira ya maisha yangu naona kama vile inapotea!
nitafanikiwaje katika masomo yangu na kuwa active muda wote na hamu ya kujisomea isiishe na wala isiwe ya msimu(leo ipo kesho haipo?
 
Katika maisha utakutana na mambo mengi maguma na marahisi, Lakini kumbuka kuwa mara ukutanapo na suala ambalo liko nje ya uwezo wa kawaida basi muombe sana mwenyezi Mungu kwani yeye ndo muwezeshaji wa yote,
MSIKILIZE MUNGU
 
Jaribu kuongea na kila mwalimu wa kila somo unalosoma umweleze matatizo yako na watakushauri vizuri sana na utafanikiwa!
 
Msaada tafadhari,mi ni mwanafunzi nahitaji nijiamini katika masomo yangu ili nifanye vizuri
mara nyingi huwa najawa na hofu na kujiona nishafeli ninapomuona mtu kasoma topic ambayo mi sijasoma
hofu hii huwa nipo nayo muda wote na muda mwingi huwa nafikiria tu nashindwa hata kuchukua hatua na hatimae nafeli kweli
naombeni mnisaidie jinsi ya kufanya niondoe hii hofu maana nimejaribu mwenyewe lakini nimeshindwa na dira ya maisha yangu naona kama vile inapotea!
nitafanikiwaje katika masomo yangu na kuwa active muda wote na hamu ya kujisomea isiishe na wala isiwe ya msimu(leo ipo kesho haipo?

inaonekan unapenda kujiringanish na wenzio sio kitu kibaya kina madhara sometimes.sasa ww fany hivi.
hakikisha likizo ikifika nenda kapge tuit masomo yenye changamoto na ikiwezakan soma topic zote za somo husika yaa mfano kam unaingia form 3 ikifik mwez wa 12 piga pindi la form n cover topic nyingi huwezavyo ili mkifungua huwe mbele kidogo na wenzio itakupa aman.
pia jarib kutafuta centre za kufany mitihan frequently kujion wap kun udhaif wap huongeze msuli na kujijengea kujiamin
jaribu kumfundish asiye jua itakupa kupanua mawazo zaid kwa ulicho soma na njia nzuri ya kujisomea.
KUMBUKA YEYOTE ANAEZA KUFAULU KAMA AKIAMUA KUJIBIDIISHA NA KUTOKATA TAMAA.KINYUME NI KWELI PIA....
 
Msaada tafadhari,mi ni mwanafunzi nahitaji nijiamini katika masomo yangu ili nifanye vizuri
mara nyingi huwa najawa na hofu na kujiona nishafeli ninapomuona mtu kasoma topic ambayo mi sijasoma
hofu hii huwa nipo nayo muda wote na muda mwingi huwa nafikiria tu nashindwa hata kuchukua hatua na hatimae nafeli kweli
naombeni mnisaidie jinsi ya kufanya niondoe hii hofu maana nimejaribu mwenyewe lakini nimeshindwa na dira ya maisha yangu naona kama vile inapotea!
nitafanikiwaje katika masomo yangu na kuwa active muda wote na hamu ya kujisomea isiishe na wala isiwe ya msimu(leo ipo kesho haipo?

upo level gani katika elimu?
 
mkuu jakaeama, naomba nikupe ushauri huu,

anza mwaka 2014 kwa kuweka mipango mikakati tangible katika masomo yako, panga ratiba yako ya kusoma ambayo utaifuata kila siku (angalia masomo yako pendwa, kama ni science ama arts, kwa kifupi yale yatakayounda combination yako, yape kipaumbele sana na muda wa kutosha!, ama kama uko advanced level, basi komalia yote!)
pili, wewe ni mwanafunzi, kumbuka hiki ni kipindi cha mpito, hivyo jaribu kupunguza mambo ya ujana ambayo hayana msingi kwako wala productivity yoyote, tumia muda huo kujisomea vitu vingi kadri uwezavyo.
tatu, kuwa social na wanafunzi wenzio, jaribu wakati mwingine kuwa mchaguzi wa marafiki, chagua productivie students ambao mtashare mawazo katika masomo na kuendelezana hapa na pale. hapa simaanishi uwatenge baadhi ya wenzio, hapana, namaanisha kuwa kuna kampani nyingine zinapotosha na kutoa kwenye ramani kabisa.
nne, punguza muda wa kukesha kwenye social networks kama hapa, fb na kwingineko. fanya tu kama una spare time and not otherwise.

pokea na ushauri mwingine kutoka kwa wadau!
 
Last edited by a moderator:
KUJIAMINI: Hakikisha unasoma topic zote na unazielewa, fanya jitihada zako zote hata kwa kupitia hao wanafunzi wenzako unaowafahamu kuwa wamesoma hizo topoc ambazo we hujasoma. Jiandae mapema na vema kabla ya mtihani na ujaribu kujipima kwa kujaribu kukumbuka ulichosoma. Ukifanikisha hili hautakuwa na wasiwasi na mtihani kwani naamini ndio tatizo lako.
HAMU YA KUSOMA: Ndugu yangu ili uwe na ari ya kusoma fanya yafuatayo:
1. Yathamini masomo na uyape nafasi ya ukombozi ktk tabu na changamoto zinazokulkabili ktk maisha yako.
2. Weka malengo yani unataka ufike wapi kielimu, Na ujue kusoma ndio ngazi ya kufikia malengo yako.
3. Kama unatoka ktk familia maskini tengeneza picha ya nyumbani kwenu kila unapoanza kusoma na ujiapize kuwa unaingia vitani ili kuikabili hali hiyo kupitia elimu.
4. Epuka kuwa na marafiki wasioleta changamoto na wanaokatisha tamaa. Wengi hujikuta wanafuata makundi ambayo huwaposha kuwavunja moyo kila wanajaribu kusoma, kwa mf usiogope kuambiwa umetumwa na kijij.
 
Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa, ongeza maombi zaidi kwa Mungu na usipende kukaa peke yako peke yako.
 
kuondoa hofu ni kufanya maswali mengi sana na kutulia wakati wa mtihani na kutoingia katika kila group discussion au kutokimbilia kusoma kila kitabu zaidi sana jitahidi kumsoma mwalimu wako atatunga vipi na usome nondo zake sana. wee angalia wanaopata first class huwa wanakuwa consistrncy na notice za mwalimu, maswali mengi na hawajichanganyi kila group
 
Kuna mstari wa shairi upo kwenye wimbo aliimba 'Afande Sele' na 'Dogo Ditto' unasema "Aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea".

The same apply to you! You have got a psychological ploblem that needs to solved psychologically. From now stop thinking negatively instead think positively and all what you think will become true!

Anza sasa kufikiri kuwa hata kama wamesha soma topic za mbele, nikisoma notice za mwalimu tu, mimi ndiyo nitaongoza kuwa na alama za juu halafu niwashangaze na tuition zao. Soma kwa bidii notes za Mwl na jiunge kwenye group discussion pamoja na hao waliosoma topic za mbele.

Hakikisha unaelewa kila kipengele na pitia past paper nyingi za mwalimu wako.

Kuifanya hivyo, utapata banda kwa kila somo!
 
nawashukuruni nyote@young teacher@mshua na wengine wote maana ushauri wenu umenifungua kiasi fulani
 
Back
Top Bottom