Msaada: Jinsi ya kupunguza au kutokuwa na hasira

Msaada: Jinsi ya kupunguza au kutokuwa na hasira

Wapendwa wa JF habarini, poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kilivyo,

Naomba ushauri ili niweze kupunguza au kuondoa kabisa hasira katika maisha yangu.

Wakuu ninatabia ya kupandwa hasira

Nahitaji ushauri wenu nifanye nini ili nisiwe mtu wa hasira hasira.
Pole sana kwa hiyo hali naamin majbu na ushauri utaupata humu kwa wataalamu zingatia ushauri wao
 
Kwanza, badilisha Avatar/picha yako, nayo ni jipu.

Kisha, tegemea hiyo kampani yako kukusidia na siyo kuwafanya adui zako.

Tena, tumia muda mwingi kufanya kazi na acha stori za majungu na watu wanaokuzunguka

Jitahidi, kuwasikiliza watu badala ya wewe kuwa muongeaji sana na kuona kuwa unaelewa kila kitu.

Kubali mawazo ya wengine wanapokushauli au wanapoongea jambo lolote lile.

Pia, usiwe mbishi, maana hata hapa umeleta matatizo ila bado unaonesha tabia za kibishi bishi na kudharau wanao kusaidia.

Wengine wataongezea.

Nitarudi tena ... ... ...
 
Kwanza maandiko yanasema hasira huketi kifuani mwa mpumbavu.

Hakuna mwanadamu ambaye hashikwi na hasira, kuna hasira mbili duniani.

1. Hasira ya Kimungu (Mfano Yesu alipowafukuza wafanyabiashara hekaluni)

2. Hasira ya kidunia (Watu wanauana kisa mapenzi, pesa n.k)

Sasa Mkuu, sisi tuzungumzie hii hasira ya 2, hii ni hasira mbaya saana na itaweza siku kuja kugharimu maisha yako. Hiyo hasira ina hasara kubwa mno kama hautaweza kuitafutia suluhisho, hasara ni kama ....

1. Hasira ni dhambi

2. Hasira haitendi haki mbele za Mungu

3. Hasira huu shina la uchungu

4. Hasira inakufanya uchukue maamuzi ambayo sio sahihi.

5. Hasira huharakisha jambo hata ambalo linahitaji muda kidogo kutatulika.

6. Hasira haina uvumilivu.

7. Hasira inamshushia thamani na kuchukiwa na jamii.


USHAURI WANGU.

Mkuu embu jaribu kuangalia movies na kufatilia baadhi ya watu duniani ambao wanatatua matatizo yao kwa njia ya mdomo na ambao wapo serious na shughuli zao

Mfano
1. Rais JK Kikwete
2. Vladimir Putin
3. Bernad Membe

Angalia baadhi ya Movies utakutana na watu ambao wanaongea kwa upole na unyenyekevu na ukiwafatilia kwa makini utagundua yafuatayo ....

1. Hawakurupuki.
2. Ni wasikilizaji hata kama watu wanaongea ujinga wao watakaa chini na kuwasikiliza mpka mwisho ujinga wao
3. Hawana majibu ya mkato na dharau
4. Wana heshima ya hali juu
5. Wana utu
6. Huwa wanapenda kushirikisha watu mambo ya hapa na pale
7. Ni wagumu kuchukua maamuzi binafsi wao kama ila wanapenda kushirikisha watu mambo yao kisha kusikiliza ushauri wa watu.

KUBWA ZAIDI NI WATU WA KUTOWEKA MAMBO MOYONI NA NI WEPESI WA KUPUUZIA MAMBO AMBAYO WANAJUA YATAWAKWAZA NA WANANGULIZA KUSAMEHE.

Ishi kama hivyo ambayo wao wanaishi, utabadilika tu, Ukiamua kubadilika utaweza kubadilika Mkuu.

Kila la heri!
 
Wapendwa wa JF habarini, poleni na majukumu.

Kama kichwa cha habari kilivyo,

Naomba ushauri ili niweze kupunguza au kuondoa kabisa hasira katika maisha yangu.

Wakuu ninatabia ya kupandwa hasira hata kwa jambo dogo mimi ni mtu wa kukasirika sana, nikitofautiana tu na mtu kwa jambo lolote lazima nikasirike. Hasira hizi zimenifanya baadhi ya ndugu na marafiki wapungue nimeshindwa kujitawala.

Nahitaji ushauri wenu nifanye nini ili nisiwe mtu wa hasira hasira.
Kama una bunduki Piga risasi hasira itaisha.
 
Bora wewe walau unatambua tatizo lako.ushauri wangu ni kama ifuatavyo.
1.Fanya meditation na mazoezi ya yoga,yanasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa jazba na hasira.
2.Pendelea kufanya vitu vinavyokufurahisha,tafuta kampani ya watu wacheshi
3.Mpende na kumwogopa muumba wako na fuata mafundisho ya imani yako.
4.Usipende kuweka dukuduku moyoni,kuwa mtu wa kupotezea mambo madogomadogo,tafuta kitu uwe unafanya pindi unapokuwa umekasirishwa,kunywa maji,oga,lala etc.
5.
b0d28331eb3903abfc53bf46ca5bab8f.jpg
 
Tumia njia zifuatazo,

1) Njia ya kuhesabu Namba kuanzia juu kushuka chini , hasira zikikupanda kabla hujachukua uamuzi wowote anza kuhesabu kimoyo moyo kuanzia labda 50 49 48 47 46......mpaka unafika 1. Hii inasaidia sana kupunguza hasira.

2) Tumia breathing meditation, Anza kushusha pumzi na kupandisha Fanya hivyo angalau robo saa.

3) Kunywa Maji ya baridi au nenda kabisa kaoge Maji ya baridi.
 
Yasome hayo maandiko ya Mungu na kuyatafakari kwa kina pia jaribu kukutana na watu wa kiroho kwa maombezi, wakati mwingine ni shetani,mapepo na hata tabia fulani za kurithi umefungamana nazo kwahiyo bila maombi ni kazi bure.
Sawa mkuu
 
Pole Sana kwa hilo maana mara nyingi hali kama hiyo inakupa majuto sana baada ya kujikuta umemkasirikia mtu kwa sababu isiyo ya msingi.
Ila kwa wewe kujua ni tatizo tayar ni nusu ya jibu. Mm pia kuna wakati nilipitia hali kama ya kwako nilijitahidi kuacha nikashindwa,ilibidi nimwombe Mungu sana na kujilazimisha kuacha hasira hatimaye nilifanikiwa kupunguza sana hasira. Jitahidi kuwa mtu wa ibada na kumwomba Mungu au kuwashirikisha wengine wakuombee nina hakika utafanikiwa. All the best
Sawa mkuu ntafanya hivyo
 
Kwanza, badilisha Avatar/picha yako, nayo ni jipu.

Kisha, tegemea hiyo kampani yako kukusidia na siyo kuwafanya adui zako.

Tena, tumia muda mwingi kufanya kazi na acha stori za majungu na watu wanaokuzunguka

Jitahidi, kuwasikiliza watu badala ya wewe kuwa muongeaji sana na kuona kuwa unaelewa kila kitu.

Kubali mawazo ya wengine wanapokushauli au wanapoongea jambo lolote lile.

Pia, usiwe mbishi, maana hata hapa umeleta matatizo ila bado unaonesha tabia za kibishi bishi na kudharau wanao kusaidia.

Wengine wataongezea.

Nitarudi tena ... ... ...
Ushauri ni mzuri ila sio muongeaji,mpigaji majungu,na sijaonesha ubishi na dharau yoyote hapa
 
1.Fikiria matokeo ya utakachokifanya
2. Sema Mungu nisaidie ipungue hii hasira
3. Dharau, mdharau anaekupandisha hasira, afu jisemee hakuna mtu anastahili jasho langu au hasira yangu


itaacha mm namalizaga kwa mtindo huo.. sitakagi ngeu na mamizigo ya hasira
 
Mkuu njia rahisi saana ni hii

Ukiona umeudhika sana unataka kufanya kitu kishicho cha kawaida au hata kimekutokea kitu ukapanic do this;


Vuta pumzi kubwa na zuia kwa second 5 had 10 kisha pumua taratibu fanya hivyo mara kadhaa hasira zitapungua na utapata relief na brain itafanya kazi rationally.

Unashauriwa pia kufanya hivyo mara kwa mara hata kama haupo kwenye hali ya hasira itakusaidia sana kutokua short tempared na hata kuwa na maaamuzi rational kwenye mazingira magumu.
 
Back
Top Bottom