Wakuu mimi nina mke tuliedumu naye kwenye ndoa kwa muda wa mwaka wa 6 sasa na ndoa yetu tuliifunga kanisani.
Lakini sasa ndoa imefikia mahali haiwezi tena kuendele baada ya juhudi nyingi(nisingependa kuliongelea sana hili)
Naomba ushauri wenu wa kisheria ni hatua gani naweza kufanya kisheria ili tuimalize ndoa hii kisheria
Msaada wenu ni muhimu
- Kama kweli ndoa ni ya kanisani kulingana na maandiko matakatifu utamwacha mkeo kama amefanya uzinzi na imethibitishwa hivyo vinginevyo ni mpaka kifo..
- Kama amefanya uzinzi ni kuchukua barua ya Padre / Mchungaji kuipeleka mahakama ya mwanzo na kufungua kesi ya kudai talaka, kesi itapangwa na kusikilizwa maombi yako na kutolewa uamuzi
- Lakini yote kwa yote miaka sita ya ndoa ni muda mrefu ambao inaonyesha kwamba mmevumiliana vya kutosha ni kwa nini msiendelee kuvumiliana na kuambua kuachana?...
- Kuachana kunaharibu future ya watoto na kuyumbisha mambo mengi ikiwemo uchumi... maana itabidi mambo ya kugawana mali ...kwa kweli kuachana ni vibaya iko haja ya kurudi tena mezani kwa mazungumzo kukaa kama kamati.... nikiwa na maana ya kuurudisha nyuma moyo wako na kujiuliza uliza mara kumi kwamba je kuachana ndio suluhisho...? na hali inavyoelekea wewe ukiwa mwanamume baada ya kumuacha huyo nini kinafuata... isije ikawa kuacha na kuoa ndio mtindo wako

Mna watoto???Suala la msingi ni hilo km mna watoto mmejenga I mean mna mali kias gan,Yeye anafaham huo mpango??Nimedivorce 2 yrs ago baada ya mm naye kukubaliana kwa kila kitu na mwisho mtoto yupo kwa bb yake ambaye nipo nae karibu na every friday namchukua nakuwa naye wkend yote
Rudia kusoma uzi wa mleta mada.
Ameomba msaada wa kisheria, hajaomba ushauri wa nini kifanyike au nini kinaweza kikatokea.
Nasisitiza tena, Ameomba msaada wa kisheria.
Thanx a lot for quick response
Mkuu naomba kaufafanuzi kidogo inamaana mahakama haitakubali sababu nyingine yeyote hadi iwe ni uzinzi kwa ndoa ya kanisani?
Nashukuru pia kwa ushauri wako wa kurudi mezani kwa mazungumzo lakini kwakweli mahali tulipofikia haiwezekani tena, na hii ni ndoa yangu ya kwanza na sitarajii tena kuingia huko
Kwa akili yako unadhani wote hupitia hatua hizo? Je, kama huyo mke aliletewa au kulazimishwa na wazazi amuoe? Au alikuwa akipita tu lakini bahati mbaya kitu kikanasa na hivyo kulazimika kumuoa? Na nadhani pia wewe haujui ukweli kwamba zaidi ya 70% ya wanandoa walilazimika kuoa/kuolewa na watu ambao hawakuwatarajia kabisa!............ Siwezi kuisemea mahakama ... mahakama ndio itaamua jinsi inavyoona hata kwa sababu zingine zinaziridhisha ndoa hiyo ivunjwe.... ila bado nasisitiza hakuna kisichowezekana ... unaweza ukarudisha moyo wako nyuma ukikumbuka chanzo cha mahusiano yenu kilivyokuwa ... jinsi ulivyoanza kufukuzia...jinsi ulivyohangaika kumpa ofa, zawadi mbalimbali, uongo na kweli kwa saaaana n.k.....na jinsi ulivyomuona mwenzako atakufaa maishani hadi kuamua kumuoa.... na kumbuka pia ile siku ulivyoonja mara ya kwanza na kuridhika.....SONGELA
Kwa akili yako unadhani wote hupitia hatua hizo? Je, kama huyo mke aliletewa au kulazimishwa na wazazi amuoe? Au alikuwa akipita tu lakini bahati mbaya kitu kikanasa na hivyo kulazimika kumuoa? Na nadhani pia wewe haujui ukweli kwamba zaidi ya 70% ya wanandoa walilazimika kuoa/kuolewa na watu ambao hawakuwatarajia kabisa!
Sasa hapo ulikuwa unajiongelea wewe au mleta uzi? Hayo ni wewe, na sio wote na kwakuwa ulikuwa unatoa ushauri kwa mtu ambaye hujui chanzo cha mahusiano yao kilikuwaje, hukupaswa kuchukulia kama vile ilivyokuwa kwako. That is my argument, period!.......Kama utafiti wako ni sahihi mimi sijui .............. na kama wewe ulilazimishwa kuoa/kuolewa mimi sio fungu langu... mimi nilitongoza, nilifukuzia nikafanya utafiti ili kujiridhisha ahadi na zawadi za uongo na kweli mpaka nikawini .. ndo nikatangaza kwa wazazi kisha vikao..nk. nk. kwa maana hiyo ndo maana nasema nakumbushia jinsi mahusiano yanavyoanza na baadaye kutokea mpagaranyiko....