Msaada jinsi ya kuvunja ndoa kisheria

Msaada jinsi ya kuvunja ndoa kisheria

Mayu

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2010
Posts
7,621
Reaction score
12,505
Wakuu mimi nina mke tuliedumu naye kwenye ndoa kwa muda wa mwaka wa 6 sasa na ndoa yetu tuliifunga kanisani.
Lakini sasa ndoa imefikia mahali haiwezi tena kuendele baada ya juhudi nyingi(nisingependa kuliongelea sana hili)

Naomba ushauri wenu wa kisheria ni hatua gani naweza kufanya kisheria ili tuimalize ndoa hii kisheria
Msaada wenu ni muhimu
 
  1. Kama kweli ndoa ni ya kanisani kulingana na maandiko matakatifu utamwacha mkeo kama amefanya uzinzi na imethibitishwa hivyo vinginevyo ni mpaka kifo..
  2. Kama amefanya uzinzi ni kuchukua barua ya Padre / Mchungaji kuipeleka mahakama ya mwanzo na kufungua kesi ya kudai talaka, kesi itapangwa na kusikilizwa maombi yako na kutolewa uamuzi
  3. Lakini yote kwa yote miaka sita ya ndoa ni muda mrefu ambao inaonyesha kwamba mmevumiliana vya kutosha ni kwa nini msiendelee kuvumiliana na kuambua kuachana?...
  4. Kuachana kunaharibu future ya watoto na kuyumbisha mambo mengi ikiwemo uchumi... maana itabidi mambo ya kugawana mali ...kwa kweli kuachana ni vibaya iko haja ya kurudi tena mezani kwa mazungumzo kukaa kama kamati.... nikiwa na maana ya kuurudisha nyuma moyo wako na kujiuliza uliza mara kumi kwamba je kuachana ndio suluhisho...? na hali inavyoelekea wewe ukiwa mwanamume baada ya kumuacha huyo nini kinafuata... isije ikawa kuacha na kuoa ndio mtindo wako
 
Mna watoto???Suala la msingi ni hilo km mna watoto mmejenga I mean mna mali kias gan,Yeye anafaham huo mpango??Nimedivorce 2 yrs ago baada ya mm naye kukubaliana kwa kila kitu na mwisho mtoto yupo kwa bb yake ambaye nipo nae karibu na every friday namchukua nakuwa naye wkend yote
 
Thanx a lot for quick response
Mkuu naomba kaufafanuzi kidogo inamaana mahakama haitakubali sababu nyingine yeyote hadi iwe ni uzinzi kwa ndoa ya kanisani?

Nashukuru pia kwa ushauri wako wa kurudi mezani kwa mazungumzo lakini kwakweli mahali tulipofikia haiwezekani tena, na hii ni ndoa yangu ya kwanza na sitarajii tena kuingia huko
 
Rudia kusoma uzi wa mleta mada.
Ameomba msaada wa kisheria, hajaomba ushauri wa nini kifanyike au nini kinaweza kikatokea.
Nasisitiza tena, Ameomba msaada wa kisheria.
 
Mkuu delako tuna watoto wawili na sina mali za kivile, so i dont think kama hii itakuwa tatizo
Ninachotaka kujua ni namna gani nifanye maana tatizo ni yeye hataki kutoa ushirikiano wa kuachana
Je hatua ni kama alizo zitaja mkuu pilau hapo juu? au unachakuongezea mkuu
 
Last edited by a moderator:
Rudia kusoma uzi wa mleta mada.
Ameomba msaada wa kisheria, hajaomba ushauri wa nini kifanyike au nini kinaweza kikatokea.
Nasisitiza tena, Ameomba msaada wa kisheria.

Wewe ndo soma mara 5 uzi huo namba mbili ndio ushauri wa kisheria/......

  1. Kama kweli ndoa ni ya kanisani kulingana na maandiko matakatifu utamwacha mkeo kama amefanya uzinzi na imethibitishwa hivyo vinginevyo ni mpaka kifo..
  2. Kama amefanya uzinzi ni kuchukua barua ya Padre / Mchungaji kuipeleka mahakama ya mwanzo na kufungua kesi ya kudai talaka, kesi itapangwa na kusikilizwa maombi yako na kutolewa uamuzi
  3. Lakini yote kwa yote miaka sita ya ndoa ni muda mrefu ambao inaonyesha kwamba mmevumiliana vya kutosha ni kwa nini msiendelee kuvumiliana na kuambua kuachana?...
  4. Kuachana kunaharibu future ya watoto na kuyumbisha mambo mengi ikiwemo uchumi... maana itabidi mambo ya kugawana mali ...kwa kweli kuachana ni vibaya iko haja ya kurudi tena mezani kwa mazungumzo kukaa kama kamati.... nikiwa na maana ya kuurudisha nyuma moyo wako na kujiuliza uliza mara kumi kwamba je kuachana ndio suluhisho...? na hali inavyoelekea wewe ukiwa mwanamume baada ya kumuacha huyo nini kinafuata... isije ikawa kuacha na kuoa ndio mtindo wako
 
Achana nae tulia mwenyewe maana sasahv wamekua pasua kichwa sana

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Thanx a lot for quick response
Mkuu naomba kaufafanuzi kidogo inamaana mahakama haitakubali sababu nyingine yeyote hadi iwe ni uzinzi kwa ndoa ya kanisani?

Nashukuru pia kwa ushauri wako wa kurudi mezani kwa mazungumzo lakini kwakweli mahali tulipofikia haiwezekani tena, na hii ni ndoa yangu ya kwanza na sitarajii tena kuingia huko

............ Siwezi kuisemea mahakama ... mahakama ndio itaamua jinsi inavyoona hata kwa sababu zingine zinaziridhisha ndoa hiyo ivunjwe.... ila bado nasisitiza hakuna kisichowezekana ... unaweza ukarudisha moyo wako nyuma ukikumbuka chanzo cha mahusiano yenu kilivyokuwa ... jinsi ulivyoanza kufukuzia...jinsi ulivyohangaika kumpa ofa, zawadi mbalimbali, uongo na kweli kwa saaaana n.k.....na jinsi ulivyomuona mwenzako atakufaa maishani hadi kuamua kumuoa.... na kumbuka pia ile siku ulivyoonja mara ya kwanza na kuridhika.....SONGELA
 
Kwa akili yako unadhani wote hupitia hatua hizo? Je, kama huyo mke aliletewa au kulazimishwa na wazazi amuoe? Au alikuwa akipita tu lakini bahati mbaya kitu kikanasa na hivyo kulazimika kumuoa? Na nadhani pia wewe haujui ukweli kwamba zaidi ya 70% ya wanandoa walilazimika kuoa/kuolewa na watu ambao hawakuwatarajia kabisa!
 
.......Kama utafiti wako ni sahihi mimi sijui .............. na kama wewe ulilazimishwa kuoa/kuolewa mimi sio fungu langu... mimi nilitongoza, nilifukuzia nikafanya utafiti ili kujiridhisha ahadi na zawadi za uongo na kweli mpaka nikawini .. ndo nikatangaza kwa wazazi kisha vikao..nk. nk. kwa maana hiyo ndo maana nasema nakumbushia jinsi mahusiano yanavyoanza na baadaye kutokea mpagaranyiko....
 
Sasa hapo ulikuwa unajiongelea wewe au mleta uzi? Hayo ni wewe, na sio wote na kwakuwa ulikuwa unatoa ushauri kwa mtu ambaye hujui chanzo cha mahusiano yao kilikuwaje, hukupaswa kuchukulia kama vile ilivyokuwa kwako. That is my argument, period!
 
Badili dini tu ni ground tosha au tumia njia hatari kama kumnyanyasa,kutompa haki yake ya ndoa,utende kosa ufungwe au uigize ukichaa mpaka upate cheti cha ugonjwa cha daktari atakaethibitisha huwezi pona kwa ground hizo piga ua talaka lazima itoke
 
Wakuu mimi nina mke tuliedumu naye kwenye ndoa kwa muda wa mwaka wa 6 sasa na ndoa yetu tuliifunga kanisani.
Lakini sasa ndoa imefikia mahali haiwezi tena kuendele baada ya juhudi nyingi(nisingependa kuliongelea sana hili)

Naomba ushauri wenu wa kisheria ni hatua gani naweza kufanya kisheria ili tuimalize ndoa hii kisheria
Msaada wenu ni muhimu

Kama uliapa kanisani kuwa hamtaachana mpaka kufa ni wazi kuwa mahakama inaweza kukusaidia kutengana na mkeo (separation) lakini haina mamlaka ya kuivunja ndoa hiyo.
 
procedures za divorce ziko wazi kabisa,questions considered ni
1)Place where marriage was conducted.
2)Duration of your marriage - ambayo umesema 6yrs
3)Any issues/children?
4)When did the problems begin?
5)What are the problems? - but umesema u cnt disclose
6)What matrimonial properties have you jointly acquired?their worth?

Kama unataka kuachana na mke wako kisheria, there are procedures that need to be followed, like kwenda kwanza Baraza la Usuluhishi linalotambulika kisheria (eg. baraza la kata), ikishindikana kuwasuluhisha,unapewa fomu itakayokuruhusu kwenda Mahakamani, ila ili upate petition yako ya divorce iwe granted lazima uwe na definite reason ambayo imeandikwa katika Sheria ya Ndoa, kama sababu yako haipo kwenye hizo grounds of divorce,wala usijisumbue,Mahakama lazima ijiridhishe kwamba ndoa yenu has "irrepairbly broken down".

So because hauwezi ku-disclose reasons zako, tafuta The Law of Marriage Act,1971 soma section 107,utajua from there
 
Ni hivi..umesema ndoa ya kanisani lkn hujataja ni dhehebu gani. Km ni roman catholic unachotakiwa kifanya ni kwenda kwa paroko wenu umweleze matatizo yako na na nia yako. Yeye atawashauri wewe na mkeo, akishindwa kuwasuluhisha atawaandikia barua muende kwenye mahakama ya ndoa ya kanisa, ipo kurasiri. Huko kesi itaendeshwa kwa kufuata sheria na kanuni za kanisa katoliki.

Na kwa kukukumbusha tu ni kwamba kanisa katoliki halivunji ndoa wanachofanya ni kibatilisha.

Unachotakiwa kufahamu ni factors zipi zinafanya ndoa kuwa batili. Nenda cathedral book shop pale karibu na st.joseph katafute kitabu cha sheria za ndoa nimesahau author wa hicho kitabu bt ni kitabu konachoelezea kanuni zote za ndoa na sababu zinazofanya ndoa kuwa batili. Km sababu zako za kutaka kuvunja ndoa zitaendena na za kwenye hicho kitabu basi uhakika wa kufanya ndoa yenu kuwa batili ni mkubwa. Km huna sababu ujue hutafanikiwa.

Huko kwenye mahakama ya kanisa inaweza kuchukua more than 3 years so usiwe na haraka. Km utafanikiwa mtapewa barua iliyo sainiwa na kardinali pengo kuthibitisha kuwa ndoa yenu ni batili na kila mmoja yupo free kuoa au kuolewa lakini mpka mahakama ya serikali itoe talaka.

Hope nimeeleweka kiasi. Bt hizo process ni kwa kanisa katoliki tu. Madhehebu mengine kwa kweli sina idea.

All the best.
 
Kama mlifunga ndoa kilitheri utaratibu ukoje hadi kufika kwenye devorce ya mahakama
 
Jamani mie nina mtizamo tofauti, pengine ni kutokuelewa sharia ntaomba msaada. Ninaamini mahakama hutoa kitu kinaitwa Divorce decree pale ambapo itadhihirika kuwa ndoa hii imekuwa na ireconciliable differences. NA hii divorce decree si ndio talaka yenyewe au? Mie shemeji yangu alimpeleka dadangu mahakamani walikuwa wameoana kanisani. Na wakakubaliana na ndoa ikavunjwa.
 
Back
Top Bottom