Msaada juu ya afya ya uzazi

Msaada juu ya afya ya uzazi

kamsongole

Senior Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
111
Reaction score
15
wandugu naomba mnisaidie kujua hili, mimi nilitakiwa kuanza kubridi tarehe 9 mpaka 12 kwa muda wa siku nne. Tarehe nane ilipofika nikasikia maumivu makali mpaka hiyo tarehe 12 ila mpaka sasa sijabridi na maumivu yamepungua. Tatizo litakuwa nini wandugu? Naomba msaada wenu.
 
Naomba msaada wenu ndugu zangu. Mi nilitakiwa kuanza period yangu ya kila mwezi tarehe 9 mpaka 12 mwezi huu na dalili zote nilikuwa nazo lakini mpaka sasa sijaziona siku zangu. Tatizo litakuwa ni nini? Naomba mnisaidie wazoefu na Madoctor
 
Naomba msaada wenu ndugu zangu. Mi nilitakiwa kuanza period yangu ya kila mwezi tarehe 9 mpaka 12 mwezi huu na dalili zote nilikuwa nazo lakini mpaka sasa sijaziona siku zangu. Tatizo litakuwa ni nini? Naomba mnisaidie wazoefu na Madoctor

Kwa vile mdau aliye tangulia hujajibu swali lake inaonyesha hauko kwenye mtandao kwa sasa maana kulikuwa na maswali kadhaa ya kuku uliza,ila sasa nitajibu kwa ujumla tu sababu zinazo weza kukusababisha kukosa hedhi ni pamoja na-
>kupata mimba
>kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango,kuacha kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango na hii inaweza ikachukua siku hadi miezi mpaka hata sita kurudi hali ya kawaida.
>kuwa na msongo wa mawazo(depression) au stress
>kunyonyesha mtoto
>kutumia madawa mf baadhi ya antibiotics,nk
>kubadili mazingira yenye hali ya hewa tofauti
>menopause-kufikia kikomo cha kupata hedhi kuanzia age ya 45-
Baadhi ya sababu ndo hizo unaweza check ipi ina kuhusu.
 
ndiyo nimefanya tendo la ndoa karibuni kwa sababu nimeolewa. Sijawahi kutumia uzazi wa mpango
 
Je vipi na fibroid inaweza kumzuia mtu asiingie kwenye period
 
Na vipi mtu akipata mimba inachukua muda gani mpaka ionekane kwenye vipimo?
 
Inaweza kuwa ni mimba na kama haitakuwa mimba inaweza kuwa ovarian cysts,POLE SANA
 
Back
Top Bottom