Msaada juu ya hizi button kwenye gari

Button ya MANU imewekwa kwenye gari automatic ili kumpa Dereva option ya kuendesha gari yake kama manual.
The minute ukipress hiyo button tayari wewe una kua una amua engagement ya gia.
Unaamuaje wakati namba za gia hamna
 
Button ya MANU imewekwa kwenye gari automatic ili kumpa Dereva option ya kuendesha gari yake kama manual.
The minute ukipress hiyo button tayari wewe una kua una amua engagement ya gia.

Sasa unaamua vp mkuu wakati gari iko kwenye D
 
Hata mm nashangaa! Utashifti gia wakati hamna stick shift
Wanazingua hao, najua gari ambazo zina double transmission. Huwa zina pande mbili.
Ya kwanza hio ya kawaida then kuna upande wa pembeni wenye alama za + na -
 
nimejifunza mengi hapa..
shukrani sana wadau!
 
Umechanganya [emoji1] [emoji1]
Hapana, OD huwa iko ON muda wote ili kuruhusu gari kuingia kwenye gia ya juu kabisa pale mazingira yanaporuhusu. Kwenye dashboard huoni chochote. Iweke OFF, maandishi yatatokea kwenye dashboard O/D OFF, hivyo kuzuia gari isiingie kwenye gia ya mwisho. Kama gari ina gia 3, OD ON itaruhusu 'gia ya nne'.
 
Ningependa kusahihisha kidogo hapa. kwanza Cruise control ndio inatumika kama uko highway au unadhani njia iko straight unakwenda speed unayotaka halafu unabonyeza cruise control speed inakuwa fix ni mpaka ukanyage break inakuwa canceled. haitumiki ku overtake au milima sio sawa ni hatari zaidi unaweza kuwa huna control ila kama njia ndefu na hutaki kuwa unakanyaga mafuta umechoka unaweka cruise tu speed inakuwa automatic bila kukanyaga mafuta. Kuhusu Man ni kwamba gari nyingi model mpya zinakuwa na option ukitaka kwenda Man unaweza na gari nyingi ukienda Man utaona kwenye dash gear number na kubadili kunakuwa na + na - na ukichange utaona number mbele. L au D hizo ni automatic tu hugusi D ndio haswa drive ila L ikiwa barabara mbaya sana matope labda unaweka L inakuwa heavy. ukienda Man gari zingine utaona S katika gear hapo unaendesha kama Man plus na minus. Nadhani nitakuwa nimeweka mambo sawa tu. Ila Cruise control kwa Tz tabu kidogo maana 50/50 nyingi sana ila unaweza kutumia ni raha yako.
 
Mkuu nadhani cruise control button works differently na power button.
Cruise control huilock accelerator pedal while PWR inafanya mambo tofauti kidogo.
 
Sasa unaamua vp mkuu wakati gari iko kwenye D
Ukiangalia namna hiyo system ilivyo kuanzia chini kuna 1,2,3,D nyingine hua na L,2, 3,D etc unapo press MANU button ukiwa kwenye D gari utaendesha gari kama gari ya manual meaning gari haita jibadili gia hadi wewe ubadili.
Utatoka D utaenda 3,3-2,2-1 kama manual tu.
Umeelewa?!?!
 
Bado umechanganya mkuu. OD inapokuwa On maanake una Overdrive default settings za engine rotation per gear.

Na ikiwa ON maanake engine iwe ina rev zaidi kwenye each gear, haizuii kuingia gia ya mwisho.

Mfano ikiwa off, ukifika rpm 2000-2500 gia inachange, lakini ikiwa On utaona gia inachange labda kuanzia 3500-4500 rpm.

Hili suala la kurhusu gia halina ukweli wowote. OD inafanya kazi kama PWR. Gari za siku izi hukuti OD wanatumia PWR
 
Wanazingua hao, najua gari ambazo zina double transmission. Huwa zina pande mbili.
Ya kwanza hio ya kawaida then kuna upande wa pembeni wenye alama za + na -
Mbona ukitaka kuendesha gari ya automatic kama manual inawezekana sana bila ya hata hio Button ya Manual.

Kama una gari auto, washa mashine, weka L/1 usiweke D, endesha mpaka unapojisikia saivi unataka kuchange gia, pandisha 2 bila kukanyaga breki utaona inaingia gia fresh bila waswas, endelea mpaka ufike D
 
Je, ni wakati gani gari itakuwa huru kuingiza gia ya mwisho kabisa na itakayosaidia kupunguza ulaji wa mafuta? OD ikiwa ON au OFF.
 
Bado sijaelewa boss. Ina maana hizo 1 2 3 ndio namba za gear ama
 
Bado sijaelewa boss. Ina maana hizo 1 2 3 ndio namba za gear ama
Upo sahihi... Hapo unaanzia let say moja, gari ikitembea itadai gia unapeleka 2,tatu mpaka D.
Baadae utafanya change down D kwenda 3, tatu kurudi D Kama manual tu.
Umeelewa hapo chief?
 
Je, ni wakati gani gari itakuwa huru kuingiza gia ya mwisho kabisa na itakayosaidia kupunguza ulaji wa mafuta? OD ikiwa ON au OFF.
Kitu kimoja lazima uelewe, OD kazi yake sio kuzuia gia ya mwisho kuingia. OD sio kazi yake kufanya engine ipunguze kunywa mafuta. Hizi concept futa akilini mwako. Kazi ya OD ni kuiruhusu engine ku rev higher than normal. Nimetoa mfano hapo juu kuhusu ubadilikaji wa gia kutokana na rpm. OD ikiwa On ikiwa Off, kwa mfano engine rev limit ni 7000 rpm, ikifika 7000 rpm gia itabadilika lazima, kwa sababu ikiendelea kukaa kwenye same gear revving itavuka limit na ikivuka limit engine inakata kupeleka mafuta na itakuwa nonsense.
 
Upo sahihi... Hapo unaanzia let say moja, gari ikitembea itadai gia unapeleka 2,tatu mpaka D.
Baadae utafanya change down D kwenda 3, tatu kurudi D Kama manual tu.
Umeelewa hapo chief?
Okay chief. Ahsante
 
Naendelea kujifunza kuhusu overdrive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…