Kuhusu taratibu za kufuatilia mirathi inategemea kama marehemu aliacha wosia au hakuacha wosia Mkuu.
Hivyo basi hizo taratibu za kufuatilia mirathi ni kama ifuatavyo;
PALE AMBAPO KUNA WOSIA.
-inabidi mtoe taarifa ya kifo kwa mkuu wa wilaya ndani ya
thelathini(30)
-Msimamizi wa mirathi aende akafungue mirathi mahakamani akiwa na vitu vifuatavyo;
a)cheti cha kuthibitisha kifo.
b)wosia ulioachwa na marehemu
-Mahakama itatoa tangazo la maombi ya kuteuliwa kwa msimamizi wa mirathi kwa muda wa siku 90. Lengo ni kuhakisha kwamba kama kuna mtu ana dukuduku dhidi ya mtu aliyeteuliwa kusimamia mirathi/ wosia awasilishe hoja zake mahakamani.
-kama kutakuwa hakuna tatizo lolote mahakama itatoa barua ya kuhalalisha huo uteuzi na majukumu yake.
PALE AMBAPO HAKUNA WOSIA
-Taarifa ya kifo itolewe kwa Mkuu wa wilaya ndani ya siku 30.
-Kikao cha wanafamilia inabidi kifanyike ili kumchagua atakaesimamia hiyo mirathi.
-Aliyechaguliwa kusimamia hiyo mirathi lazima apeleke barua mahakamani kufungua mirathi akiwa na;
a)Nakala ya maamuzi ya kikao
b)cheti cha kifo.
-Mahakama itatoa tangazo ndani ya siku 90. Endapo itaonekana hakuna tatizo lolote Mahakama itatoa barua kuhalalisha huo uteuzi wa msimamizi na majukumu yake.
•Ingawa mahakama ina utashi wa kumchagua mtu yeyote kusimamia hiyo mirathi. Hii hutokea pale ambapo unakuta hakuna wosia wowote uliachwa au kuandikwa.
Kikomo cha kufungua shauri la mirathi huwa ni miaka 12.
Kama hautafungua hilo shauri ndani ya miaka kumi na mbili na hakuna mtu yeyote anayefuatilia hiyo mirathi itabidi mali zote za marehemu ziwe chini ya serikali.