Msaada juu ya kufuatilia mirathi

Msaada juu ya kufuatilia mirathi

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,812
Reaction score
1,373
ndugu wanajamvi naomba utaratibu wa kufuatilia mirathi kuanzia mwanzo kabisa

na jee kina kikomo cha kufungua mirathi mfano baada ya miaka kadhaa kama 10 .sasa je kuna mda maalum wa kufungua mirathi je usipofungua katika mda huo inafungwa??
 
Kuhusu taratibu za kufuatilia mirathi inategemea kama marehemu aliacha wosia au hakuacha wosia Mkuu.

Hivyo basi hizo taratibu za kufuatilia mirathi ni kama ifuatavyo;

PALE AMBAPO KUNA WOSIA.

-inabidi mtoe taarifa ya kifo kwa mkuu wa wilaya ndani ya
thelathini(30)

-Msimamizi wa mirathi aende akafungue mirathi mahakamani akiwa na vitu vifuatavyo;
a)cheti cha kuthibitisha kifo.
b)wosia ulioachwa na marehemu

-Mahakama itatoa tangazo la maombi ya kuteuliwa kwa msimamizi wa mirathi kwa muda wa siku 90. Lengo ni kuhakisha kwamba kama kuna mtu ana dukuduku dhidi ya mtu aliyeteuliwa kusimamia mirathi/ wosia awasilishe hoja zake mahakamani.

-kama kutakuwa hakuna tatizo lolote mahakama itatoa barua ya kuhalalisha huo uteuzi na majukumu yake.


PALE AMBAPO HAKUNA WOSIA

-Taarifa ya kifo itolewe kwa Mkuu wa wilaya ndani ya siku 30.
-Kikao cha wanafamilia inabidi kifanyike ili kumchagua atakaesimamia hiyo mirathi.

-Aliyechaguliwa kusimamia hiyo mirathi lazima apeleke barua mahakamani kufungua mirathi akiwa na;
a)Nakala ya maamuzi ya kikao
b)cheti cha kifo.

-Mahakama itatoa tangazo ndani ya siku 90. Endapo itaonekana hakuna tatizo lolote Mahakama itatoa barua kuhalalisha huo uteuzi wa msimamizi na majukumu yake.

•Ingawa mahakama ina utashi wa kumchagua mtu yeyote kusimamia hiyo mirathi. Hii hutokea pale ambapo unakuta hakuna wosia wowote uliachwa au kuandikwa.

Kikomo cha kufungua shauri la mirathi huwa ni miaka 12.

Kama hautafungua hilo shauri ndani ya miaka kumi na mbili na hakuna mtu yeyote anayefuatilia hiyo mirathi itabidi mali zote za marehemu ziwe chini ya serikali.
 
ndugu wanajamvi naomba utaratibu wa kufuatilia mirathi kuanzia mwanzo kabisa

na jee kina kikomo cha kufungua mirathi mfano baada ya miaka kadhaa kama 10 .sasa je kuna mda maalum wa kufungua mirathi je usipofungua katika mda huo inafungwa??
Marehemu alikuwa mtumishi serikalini?
 
ila mbona kuna mtu alienda RITA akaambiwa mirath mwisho miaka 10??
Mwambie huyo mtu awaulize ni sheria gani
inasema hivyo.

Ila kwa mujibu wa Sheria ya Muda wa Ukomo huwa ni miaka 12 Mkuu.

Kwa maelezo zaidi soma kwenye Schedule-Sehemu ya kwanza katika Sheria hiyo ya Muda wa Ukomo ili uweze kujiridhisha na ninachokwambia Mkuu.
 
Mwambie huyo mtu awaulize ni sheria gani
inasema hivyo.

Ila kwa mujibu wa Sheria ya Muda wa Ukomo huwa ni miaka 12 Mkuu.

Kwa maelezo zaidi soma kwenye Schedule-Sehemu ya kwanza katika Sheria hiyo ya Muda wa Ukomo ili uweze kujiridhisha na ninachokwambia Mkuu.
nashukuru sana mkuu jee unaweza kunipa link ya kusoma hiyo schedule?? nitashukuru sana
 
Ingia Google utaikuta mkuu.

"The Law of Limitation Act, Cap 89 R.E 2002."
 
Kuna umuhimu wa kufungua mirathi endapo wahusika/warithi wanatambulika.na hawana mizozo.
 
Aisee nashukuru sana kwako uliyeuliza swala la mirathi maana nimeenda RITA wananiambia wao hawatoi cheti cha kifo ila wanatoa cheti cha mirathi. Nilivoenda kwa mtendaji kasema inabidi nipewe cheti cha kifo ndo nifungue mirathi Mahakamani.
 
Kama taratibu zote zimefanyika na mahakama ikatoa hati ya usimamizi kwa aliyeteuliwa/chaguliwa lakini Baada ya miaka miwili au mitatu ikatokea labda ndugu wengine hawakuridhika inakuwaje hapo?
 
Back
Top Bottom