Msaada juu ya mtoto nimehangaika hospitalini bila mafanikiao

Msaada juu ya mtoto nimehangaika hospitalini bila mafanikiao

Hiyo.huwezi kumuuliza Hadharani 😀😀😀
Itapingana na Ethics na sheria..

Ila kwa maelezo atakuwa na oral Candidias
Ni kweli, lakini tambua kuwa ugonjwa wowote hata kama ni malaria inabidi iwe siri ya mgonjwa na mtoa huduma, hakuna magonjwa special yaliyotengwa kwaajili ya kuyawekea usiri. BTW kama vile anavyohitajika kutoa taarifa za magonjwa mengine hata PITC pia ni vyema kuitolea concern kwasababu ni namna tu ya kubaini tatizo ili mgonjwa awe na afya njema
 
Ni kweli, lakini tambua kuwa ugonjwa wowote hata kama ni malaria inabidi iwe siri ya mgonjwa na mtoa huduma, hakuna magonjwa special yaliyotengwa kwaajili ya kuyawekea usiri. BTW kama vile anavyohitajika kutoa taarifa za magonjwa mengine hata PITC pia ni vyema kuitolea concern kwasababu ni namna tu ya kubaini tatizo ili mgonjwa awe na afya njema
Shida inakuja wangapi wanaelewa??
Maaana kuna wengine hawataichukulia kama yeye alivyoichukulia....
Na huenda ikatumika vbaya..
Na ndo maana kuna vingine inabdi kuviongelea PM
 
Poleni na majukumu.

Mwanangu ana miaezi 8 jinsia ya kike amekuwa akisumbuliwa na joto kupanda hasa kichwani na kwenye tumbo. Nilimpeleka hospitali mara 3 hospitali tofauti tofauti lakini tatizo haliishi. Vipimo walivyokuwa wakichukuwa ::

MRDT
URINE
RBG
FBP

Dokta alisema ana maambukizi kwenye damu akaandikiwa dawa na sindano dawa yakuongeza dam
kiukweli amesha maliza lakini sioni mabadiliko mtoto amekuwa kishtuka usiku hataki kula wa kunywa uji hataki.

Naimani humu kuna wazazi kama mm naombezi mawazo yenu madokta karibuni #mzizimkavu karibu upite hata

Pole mtoa mada:

SEHEMU YA KWANZA
(Matatizo haya kwa miezi 2)

1: Homa kwa mwezi mzima

2: Mafua

3: Kikohozi

4: Choo chepesi/laini

5: Kutokula vyema

6: Utando mweupe

7: Urefu wa kiasi cha ugonjwa

8: Damu kupungua

SEHEMU YA PILI
(Madhira)

1: Kwa kuwa kwenye ugonjwa takribani miezi miwili kulingana na hali hapo juu athari ya afya kwa ujumla kuteteleka itakuwepo.

2: Kutokuwa na maji ya kutosha mwilini.

3: Madini kuparaganyika (kupoteza uwiano unaohitajika).


SEHEMU YA TATU
(Approach/uzingatifu wakati wa kutatua tatizo).

A: Hapa huyu ni mgonjwa ambaye anahitaji kuonwa kwa karibu na umakini sana.

B: Kuna mambo ni chanzo na mengine ni matokeo ya uwepo wa yaliyoanza. Hivyo, unahitaji kuwa makini sana si kutibia kila dalili.

C: Vipimo vitahitajika kulingana na historia, ukaguzi wa mwili na hali ya sasa ya mtoto.

D: Kama mtoto amekuwa kwenye antibiotics kwa siku tano likely tunapambana na STRONG ACUTE VS CHRONIC VIRAL INFECTION vs Bacterial Resistant bacteria(if any). Historia nzuri na ukaguzi wa mwili ni muhimu. Pia, kile kipimo cha damu majibu yake yangepatikana yangetupa mwangaza ingawa kwa sasa inahitaji kuanza upya kulingana na siku zilivyopita.

E: Tiba pia inahitaji uangalifu sana, kuna.
mambo ya kufanyia kazi maoema LAKINI kwa umakini kulingana na uchanga wa mtoto na kiasi cha ugonjwa.

SEHEMU YA NNE
(Tiba)

1: Mtoto aonwe na daktari bingwa au mwenye uzoefu mzuri kwa watoto kwenye hospitali ambayo anaweza kupumzishwa au kulazwa ili kufatilia maendeleo yake kwa karibu.

2: Ufuatiliaji wa karibu kwenye tiba kwa kufanya kinachohitajika zaidi kwa mtoto na si kufanya kwa kubahatisha kwani kwa safari aliyopitia mtoto anahitaji umakini mkubwa.

3: Kwa maelezo hapo juu, huyu si mtoto wa kuendelea kutibiwa nyumbani pia anahitaji kituo cha afya ma daktari dedicated/mwenye kujitoa vyema na kufatilia kwa karibu.
 
Nje ya mada kidogo, Kuna dogo anaumwa hapa nimepewa dawa kwenye dispensary flan ya private ila baada ya kufika home nimegundua exipire date yake ni March 2024, yaani mwezi huu... Vp bado inaweza kutumika? au niirudishe maana nimepata hasira sana
 
Nje ya mada kidogo, Kuna dogo anaumwa hapa nimepewa dawa kwenye dispensary flan ya private ila baada ya kufika home nimegundua exipire date yake ni March 2024, yaani mwezi huu... Vp bado inaweza kutumika? au niirudishe maana nimepata hasira sana
watoto ni sensitive sana kwenye suala la afya mkuu....ni heri kurudisha dawa uliponunua kuliko madhara yatokee kwa mtoto....japo in most cases mtoto huwa hapati nafuu yoyote.
 
Pole kwa kuuguliwa na mtoto, naamini humu utapata ufumbuzi..
 
Mpeleke CCBRT. Book appointment kabisa kabla hujampeleka, pale uhakika kukutana na specialist, hospitali zingine unanahatisha tu, u aweza kutana na Dr. Ambaye si specialist.
 
Back
Top Bottom