Poleni na majukumu.
Mwanangu ana miaezi 8 jinsia ya kike amekuwa akisumbuliwa na joto kupanda hasa kichwani na kwenye tumbo. Nilimpeleka hospitali mara 3 hospitali tofauti tofauti lakini tatizo haliishi. Vipimo walivyokuwa wakichukuwa ::
MRDT
URINE
RBG
FBP
Dokta alisema ana maambukizi kwenye damu akaandikiwa dawa na sindano dawa yakuongeza dam
kiukweli amesha maliza lakini sioni mabadiliko mtoto amekuwa kishtuka usiku hataki kula wa kunywa uji hataki.
Naimani humu kuna wazazi kama mm naombezi mawazo yenu madokta karibuni #mzizimkavu karibu upite hata
Pole mtoa mada:
SEHEMU YA KWANZA
(Matatizo haya kwa miezi 2)
1: Homa kwa mwezi mzima
2: Mafua
3: Kikohozi
4: Choo chepesi/laini
5: Kutokula vyema
6: Utando mweupe
7: Urefu wa kiasi cha ugonjwa
8: Damu kupungua
SEHEMU YA PILI
(Madhira)
1: Kwa kuwa kwenye ugonjwa takribani miezi miwili kulingana na hali hapo juu athari ya afya kwa ujumla kuteteleka itakuwepo.
2: Kutokuwa na maji ya kutosha mwilini.
3: Madini kuparaganyika (kupoteza uwiano unaohitajika).
SEHEMU YA TATU
(Approach/uzingatifu wakati wa kutatua tatizo).
A: Hapa huyu ni mgonjwa ambaye anahitaji kuonwa kwa karibu na umakini sana.
B: Kuna mambo ni chanzo na mengine ni matokeo ya uwepo wa yaliyoanza. Hivyo, unahitaji kuwa makini sana si kutibia kila dalili.
C: Vipimo vitahitajika kulingana na historia, ukaguzi wa mwili na hali ya sasa ya mtoto.
D: Kama mtoto amekuwa kwenye antibiotics kwa siku tano likely tunapambana na STRONG ACUTE VS CHRONIC VIRAL INFECTION vs Bacterial Resistant bacteria(if any). Historia nzuri na ukaguzi wa mwili ni muhimu. Pia, kile kipimo cha damu majibu yake yangepatikana yangetupa mwangaza ingawa kwa sasa inahitaji kuanza upya kulingana na siku zilivyopita.
E: Tiba pia inahitaji uangalifu sana, kuna.
mambo ya kufanyia kazi maoema LAKINI kwa umakini kulingana na uchanga wa mtoto na kiasi cha ugonjwa.
SEHEMU YA NNE
(Tiba)
1: Mtoto aonwe na daktari bingwa au mwenye uzoefu mzuri kwa watoto kwenye hospitali ambayo anaweza kupumzishwa au kulazwa ili kufatilia maendeleo yake kwa karibu.
2: Ufuatiliaji wa karibu kwenye tiba kwa kufanya kinachohitajika zaidi kwa mtoto na si kufanya kwa kubahatisha kwani kwa safari aliyopitia mtoto anahitaji umakini mkubwa.
3: Kwa maelezo hapo juu, huyu si mtoto wa kuendelea kutibiwa nyumbani pia anahitaji kituo cha afya ma daktari dedicated/mwenye kujitoa vyema na kufatilia kwa karibu.