Msaada juu ya tatizo hili la mkopo wa bank

Msaada juu ya tatizo hili la mkopo wa bank

Samwel Meleka

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2014
Posts
602
Reaction score
268
Wanajamvi kwa mwenye utambuzi juu ya hili, iko hivi Mke wangu ni mmilki wa duka la dawa muhimu za binadamu na amekua akiliendesha tangu mwaka 2009 sasa mwezi wa 11 mwaka huu aliomba mkopo bank ya posta tawi moja mwanza kiasi cha sh 10m akapewa na baada ya kupata hizo pesa zote akaongeza mtaji kwenye hili duka tarehe ya kuanza ikafika akarejesha rejesho la kwanza,

Sasa ghafla wamekuja baraza la famasi na kufunga maduka yote ya dawa ukiachilia famasi, sasa hapa anaanzia wapi maana ana mkopo bank na duka limefungwa je kuna uwezekano wa kuomba bank kusimamisha kwa muda kurejesha wakati anajipanga kutatua tatzo la duka lake,maana pia kadhamini nyumba yangu tafadhali mwenyekuelewa chochote karibu kwa mawazo yako.
 
Wanajamvi kwa mwenye utambuzi juu ya hili,iko hivi
Mke wangu ni mmilki wa duka la dawa muhimu za binadamu na amekua akiliendesha tangu mwaka 2009 sasa mwezi wa 11 mwaka huu aliomba mkopo bank ya posta tawi moja mwanza kiasi cha sh 10m akapewa na baada ya kupata hizo pesa zote akaongeza mtaji kwenye hili duka tarehe ya kuanza ikafika akarejesha rejesho la kwanza,sasa ghafla wamekuja baraza la famasi na kufunga maduka yote ya dawa ukiachilia famasi,sasa hapa anaanzia wapi maana ana mkopo bank na duka limefungwa je kuna uwezekano wa kuomba bank kusimamisha kwa muda kurejesha wakati anajipanga kutatua tatzo la duka lake,maana pia kadhamini nyumba yangu tafadhali mwenyekuelewa chochote karibu kwa mawazo yako.
Awaandikie benki kueleza kwa ninini duka limefungwa na kama kuna masharti aliyopewa na kwa muda gani na ka ameanza kiyashughulikia benki wanaweza kusitisha marejesho kwa muda huo lkn wanaweza kuongeza riba.
 
Asante mkuu kwa ushauri wako,je hii kitu hua inawezekana ikitokea biashara yako inafungwa na bank wasiuze dhamana??mkuu ng'adi lawi.
 
Mkopo sio kitu kizuri hasa pale income flow inapo cease! Unahitajika ufanye mpango wa haraka kujihami!

1. Wajulishe benki kuhusu hali hio na uombe mwongozo wa nini kifanyike. Benki walishakuchezea offside trick pale walipotaka mali isiyohamishika yaani nyumba yako. Waambie benki all important details plus mkakati wako kunusuru biashara yako. Tahadhari: Ni failure kwa loan officers kushindwa kubaini going concern ya biashara yako ya duka; so dont expect much to win on this

2. Angalia baadhi ya vitega uchumi vyako vingine. Income zake zielekeze kwenye kulipa mkopo.

3. Kula mkopo usio na riba somewhere else; ili ulipe huo mkopo wenye riba. Inapatikana wapi? Kwa ndugu, jamaa na marafiki!

4. Thaminisha mali ulizonazo za duka lako la dawa. Then , tafuta namna ya kuuza baadhi kwa bei ya chini ya bei ya soko; lengo ni kupata soko! Hapa unafanya very smart calculated risk! Sometimes a little loss in business is a blessing.

Kukurahisishia hili nasikia kuna kampuni inaitwa For Sale wanajishughulisha na bidhaa ama huduma zinazouzwa kwa bei ya chini ya bei ya soko. Wasiliane nao may be they can help.

Pole sana, yatapita tu!
 
Mkopo sio kitu kizuri hasa pale income flow inapo cease! Unahitajika ufanye mpango wa haraka kujihami!

1. Wajulishe benki kuhusu hali hio na uombe mwongozo wa nini kifanyike. Benki walishakuchezea offside trick pale walipotaka mali isiyohamishika yaani nyumba yako. Waambie benki all important details plus mkakati wako kunusuru biashara yako. Tahadhari: Ni failure kwa loan officers kushindwa kubaini going concern ya biashara yako ya duka; so dont expect much to win on this

2. Angalia baadhi ya vitega uchumi vyako vingine. Income zake zielekeze kwenye kulipa mkopo.

3. Kula mkopo usio na riba somewhere else; ili ulipe huo mkopo wenye riba. Inapatikana wapi? Kwa ndugu, jamaa na marafiki!

3. Thaminisha mali ulizonazo za duka lako la dawa. Then , tafuta namna ya kuuza baadhi kwa bei ya chini ya bei ya soko; lengo ni kupata soko! Hapa unafanya very smart calculated risk! Sometimes a little loss in business is a blessing.

Kukurahisishia hili nasikia kuna kampuni inaitwa For Sale wanajishughulisha na bidhaa ama huduma zinazouzwa kwa bei ya chini ya bei ya soko. Wasiliane nao may be they can help.

Pole sana, yatapita tu!

Asante mkuu ushauri wako umezingatiwa na nitaufanyia kazi.
 
Nimekumbuka nyingine:

4. Jaribu kwenda kwenye ma benki nyingine uuze huo mkopo wako; then ukope kwao kwa masharti ya kuweka dhamana ya nyumba yako na sio tena biashara ya dawa!

Hope nimekusadia kiasi chake!

Again pole!
 
alikuwa hana tfda receipt, bank haiwezi waelewa marejesho ni palepale
 
Unamaanisha mkopo auuze bank nyingne kwa ileile dhamana je bank itakayonunua mkopo marejesho yatakuaje sasa.
 
aisee pole sana hata mm hiyo hali ilikuta Jan madai yao ni nn? haswa pia lilikuwa ni duka la dawa, duka la dawa muhimu au ni pharmacy
 
alikuwa hana tfda receipt, bank haiwezi waelewa marejesho ni palepale

Mkuu receipt na vielelezo vyote vipo sema sababu hasa ya kufungwa haijajulikana maana yamefungwa almost 90 %ya maduka ya dawa hapa mwanza hususan ilemela na nyamagana.
 
Hata hao waliotoa mkopo wana makosa kwani walipaswa wajiridhishe kuwa biashara unayofanya inaendeshwa kihalali! Na mhusika alikuwa wapi kuhakikisha shgughuli zake ziko safi kisheria? Au alikuwa anajua anachofanya?
 
Mkuu receipt na vielelezo vyote vipo sema sababu hasa ya kufungwa haijajulikana maana yamefungwa almost 90 %ya maduka ya dawa hapa mwanza hususan ilemela na nyamagana.

hii nchi inaendeshwa kwa sheria na taratibu kama hawana sababu ya msingi mbona ni kosa na hao bank hawatakuelewa kama hutakuwa na cbabu za msingi za kuwaeleza mm mwenyewe nilikuwa na duka la dawa najua baadhi ya taratibu
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta.

Mi sina ushauri mkuubwa ila you have to take big risk kwenye hili.

Good luck.
 
Wewe kilichopo cha kufanya mende mkaongee na benki, uwaeleze matatizo yako wakupe ushauri ufanye nini, ila pia muwe muwangalifu sasa katika hatua mnazochukua msije mkakopesha stock mliokua nayo kutaka pesa, mkaingia katika matatizo zaidi au mkakumbana na matapeli wakujifanya wanataka wauzia. Kama ni tangazo andikeni orodha ya stock mliyokua tangazeni kwenye gazeti au social media kuwa muna muna funga Duka la dawa mnawuza stock yenu naamini kuna watu watajiteza kuja nunua.
Nakutakia kila la kheri kwa uwezo wa mwenyeziMungu uvuke salama mtihani huu.
 
Nimekumbuka nyingine:

4. Jaribu kwenda kwenye ma benki nyingine uuze huo mkopo wako; then ukope kwao kwa masharti ya kuweka dhamana ya nyumba yako na sio tena biashara ya dawa!

Hope nimekusadia kiasi chake!

Again pole!
Ume prove kweli wewe is the DEALER.
Umetusaidia wengi.

Ila Mhusika kuna kitu kimoja ningependa kujazia hapo.Kwanza Pole kwa matatizo.
Unasema wamefunga maduka yote ya Dawa ukiachilia famas,hapo inamaana duka lako ni la Dawa baridi,na hata hivyo kuna sababu ya kwanini wanayafunga maduka hayo.
Sifa kubwa wanayoangalia na wahusika wengi hushindwa ni kuwa na mfanyakazi ambae ni mfamasia kitaaluma.
Maana kwenye kuanzisha haya maduka watu wengi tunapita njia zile za mkato kwa kumtafuta mfamasia wakati wa usajili kama mdhamini na mhusika,sasa inapotokea wamestukiza ukaguzi basi hapo ndio inakuwa sawa na hizi Dispensary zetu zinazofungwa kila siku.
Naamini serikali haiwezi kufungua dula la mtu kama anavigezo vyote,maana sheria haijabadilika ila watu kuifuata ndio issue.
Halafu acha ubinafsi:-
Huyo ni Mkeo,sasa unaposema ameweka nyumba yako dhamana ni kumtenga.
Sema ameweka nyumba yetu dhamana.
Tusiwe na tabia ya kumuona mke ni mwili mmojka wakati wa kupata pesa tu,maana najua alipopata mshiko,majina kama Honey,Babie,Sweetie yalikuwa kibao.
Leo hii kwenye tatizo inakuwa tena ameweka dhamana nyumba yangu,badala ya kusema yetu.

La mwisho ni kwamba makosa pia yalifanyika kwenye namna ya ku inject huo mkopo kwenye biashara,huwezi kukopa all 10m naa ikaingiingiza kwenye biashara,na kwa ufaham wangu wa maduka hayo ni kamba kama duka limeweza kupewa mkopo huo inamaana angalau lipo vizuri,at least 6 - 7m ingetosha kujaza mzigo wa maana,then iatakayobakia ndio itumike kama back up flani hivi ya mkopo wakati unaisoma biashara husika.Hapo inakuwa inakupunguzia presha pindi ikitokea tatizo.
Yapo matatizo mengi sana,kuna watu maduka yao yanaungua,na mbaya zaidi Bank wanatabia ya kuuliza Bima,yaani kama biashara yako ina bima,na mbaya zaidi hawakuulizi wakati wa kuchukua mkopo,ila wanakuuliza likiishatokea tatizo kama la moto.Sasa hii ni kusema kwamba mkopo wowote unapochukua hakikisha huweki pesa yote kwenye biashara moja.
 
Bank institutions are very unfriendly,hii kitu for sure itakusumbua sana kwani mentality ya hao wenye mabenki ni sawa na mentality ya watawala wetu.
1.Banks husema Watanzania hawakopesheki na ni risk kuwakopesha,na ndio maana rate ziko juu kuliko Kenya.
2.Watawala wetu wanasema Watanzania hawaajiriki,eti wavivu na wezi.Hapa ndio tulipokwama.
 
aisee pole sana hata mm hiyo hali ilikuta Jan madai yao ni nn? haswa pia lilikuwa ni duka la dawa, duka la dawa muhimu au ni pharmacy

Mkuu sababu hasa hazijatolewa mwanzo lilikua duka la dawa baridi baadae wakasema waboreshe ili kua muhimu na ikawa hivyo lakn maajabu wamekuja kupiga makufuli maduka pia na kubeba dawa zilizopo,japo jumatatu wanakutanishwa na mkuu wa mkoa kutafuta suluhu kati ya wamilki na na hii bodi ya famas.
 
Hata hao waliotoa mkopo wana makosa kwani walipaswa wajiridhishe kuwa biashara unayofanya inaendeshwa kihalali! Na mhusika alikuwa wapi kuhakikisha shgughuli zake ziko safi kisheria? Au alikuwa anajua anachofanya?

Mkuu duka lipo kisheria lina usajili na malipo yote yapo sawa tatzo kumbe wanampango wa kuyaondoa ndo tetes zilizopo.
 
Ume prove kweli wewe is the DEALER.
Umetusaidia wengi.

Ila Mhusika kuna kitu kimoja ningependa kujazia hapo.Kwanza Pole kwa matatizo.
Unasema wamefunga maduka yote ya Dawa ukiachilia famas,hapo inamaana duka lako ni la Dawa baridi,na hata hivyo kuna sababu ya kwanini wanayafunga maduka hayo.
Sifa kubwa wanayoangalia na wahusika wengi hushindwa ni kuwa na mfanyakazi ambae ni mfamasia kitaaluma.
Maana kwenye kuanzisha haya maduka watu wengi tunapita njia zile za mkato kwa kumtafuta mfamasia wakati wa usajili kama mdhamini na mhusika,sasa inapotokea wamestukiza ukaguzi basi hapo ndio inakuwa sawa na hizi Dispensary zetu zinazofungwa kila siku.
Naamini serikali haiwezi kufungua dula la mtu kama anavigezo vyote,maana sheria haijabadilika ila watu kuifuata ndio issue.
Halafu acha ubinafsi:-
Huyo ni Mkeo,sasa unaposema ameweka nyumba yako dhamana ni kumtenga.
Sema ameweka nyumba yetu dhamana.
Tusiwe na tabia ya kumuona mke ni mwili mmojka wakati wa kupata pesa tu,maana najua alipopata mshiko,majina kama Honey,Babie,Sweetie yalikuwa kibao.
Leo hii kwenye tatizo inakuwa tena ameweka dhamana nyumba yangu,badala ya kusema yetu.

La mwisho ni kwamba makosa pia yalifanyika kwenye namna ya ku inject huo mkopo kwenye biashara,huwezi kukopa all 10m naa ikaingiingiza kwenye biashara,na kwa ufaham wangu wa maduka hayo ni kamba kama duka limeweza kupewa mkopo huo inamaana angalau lipo vizuri,at least 6 - 7m ingetosha kujaza mzigo wa maana,then iatakayobakia ndio itumike kama back up flani hivi ya mkopo wakati unaisoma biashara husika.Hapo inakuwa inakupunguzia presha pindi ikitokea tatizo.
Yapo matatizo mengi sana,kuna watu maduka yao yanaungua,na mbaya zaidi Bank wanatabia ya kuuliza Bima,yaani kama biashara yako ina bima,na mbaya zaidi hawakuulizi wakati wa kuchukua mkopo,ila wanakuuliza likiishatokea tatizo kama la moto.Sasa hii ni kusema kwamba mkopo wowote unapochukua hakikisha huweki pesa yote kwenye biashara moja.

Upo sawa sehemu kubwa but duka la huyu mke wangu lipo kisheria na ameliendesha tangu mwaka 2009 pia ukaguz wa kila aina umepita na ukiliacha salama shida imeanzia kwenye kuliboresha toka baridi kua muhimu na pia alifanya hivyo na mamlaka huska wakalipitsha shida imekuja ni kua eti eneo lilipo sasa halitakiwi duka la aina hiyo tena ispokua famas eti duka la aina hii lipelekwe nje ya mji upo hapo mkuu.
 
Back
Top Bottom