Kang
JF-Expert Member
- Jun 24, 2008
- 5,655
- 2,506
Ume prove kweli wewe is the DEALER.
Umetusaidia wengi.
Ila Mhusika kuna kitu kimoja ningependa kujazia hapo.Kwanza Pole kwa matatizo.
Unasema wamefunga maduka yote ya Dawa ukiachilia famas,hapo inamaana duka lako ni la Dawa baridi,na hata hivyo kuna sababu ya kwanini wanayafunga maduka hayo.
Sifa kubwa wanayoangalia na wahusika wengi hushindwa ni kuwa na mfanyakazi ambae ni mfamasia kitaaluma.
Maana kwenye kuanzisha haya maduka watu wengi tunapita njia zile za mkato kwa kumtafuta mfamasia wakati wa usajili kama mdhamini na mhusika,sasa inapotokea wamestukiza ukaguzi basi hapo ndio inakuwa sawa na hizi Dispensary zetu zinazofungwa kila siku.
Naamini serikali haiwezi kufungua dula la mtu kama anavigezo vyote,maana sheria haijabadilika ila watu kuifuata ndio issue.
Halafu acha ubinafsi:-
Huyo ni Mkeo,sasa unaposema ameweka nyumba yako dhamana ni kumtenga.
Sema ameweka nyumba yetu dhamana.
Tusiwe na tabia ya kumuona mke ni mwili mmojka wakati wa kupata pesa tu,maana najua alipopata mshiko,majina kama Honey,Babie,Sweetie yalikuwa kibao.
Leo hii kwenye tatizo inakuwa tena ameweka dhamana nyumba yangu,badala ya kusema yetu.
La mwisho ni kwamba makosa pia yalifanyika kwenye namna ya ku inject huo mkopo kwenye biashara,huwezi kukopa all 10m naa ikaingiingiza kwenye biashara,na kwa ufaham wangu wa maduka hayo ni kamba kama duka limeweza kupewa mkopo huo inamaana angalau lipo vizuri,at least 6 - 7m ingetosha kujaza mzigo wa maana,then iatakayobakia ndio itumike kama back up flani hivi ya mkopo wakati unaisoma biashara husika.Hapo inakuwa inakupunguzia presha pindi ikitokea tatizo.
Yapo matatizo mengi sana,kuna watu maduka yao yanaungua,na mbaya zaidi Bank wanatabia ya kuuliza Bima,yaani kama biashara yako ina bima,na mbaya zaidi hawakuulizi wakati wa kuchukua mkopo,ila wanakuuliza likiishatokea tatizo kama la moto.Sasa hii ni kusema kwamba mkopo wowote unapochukua hakikisha huweki pesa yote kwenye biashara moja.
Duka la Dawa Muhimu halihitaji kuwa na pharmacist, ndo point nzima ya mradi huu kuleta maduka yanayoweza kuprovide basic medicine kwa wananchi bila complication ya kufungua Pharmacy ya kweli ulikuwa unapitia kozi fupi tu unafungua.
Sasa sielewi imekuwaje TFDA wameamua kuyafunga baadhi ya maeneo nadhani kuna wakubwa wanaona inawapunguzia biashara kwenye pharmacy zao.
Kwa upande wa deni itabidi ulipe kivyovyote, benki inaweza ikaadjust muda wa mailpo labda lakini kwa vile umeweka nyumba deni limekuwa lako pia sio la biashara tu, hii ndo hatari ya ku cosign loans.