Jamani kwa wataalamu naomba ushauri wa kitabibu,
Kuna binti alikuwa anasikia maumivu ya kiuno akaenda dispensary daktari akamchoma sindano (siikubuki jina) akampa na dawa za kutuliza maumivu. Lakini asubuhi yake binti kachindwa kuamka kitandani wiki ya tatu sasa. Alirudi hospitali daktari. akasema haelewi ni nini kimemkumba, akapewa referal kwenda hospitali ya rufaa nako wakasema hawaoni tatizo.
Lakini binti miguu imetepeta kabisa ingawa anasikia maumivu. Tukashauriwa tuangalie tiba mbadala ambako alipimwa kwa kipimo chao cha kuscan (wasabato) na kapewa dawa na kufanyishwa mazoezi sasa.Kuna maendeleo kidogo kwani angalu ukimsimamisha anaweza kuvumilia sekunde tano hivi. Lakini bado hawezi hata kuchezesha vidole vya miguu.