Asante mkuu ngoja nirekaebisheTafuteni wakili mkakate rufaa, ila cha kukusaidia hii stori sio muhimu kumpa kaka yako msaada muhimu ni
1. Andika kosa aliloshitakiwa nalo
2. Taja mahakama kama ni wilaya au Kuu
3. Sema kama alikiri au alikataa kosa
4. Omba msaada wa kisheria/Wakili
Sababu ulivyoandika ni kama vile unachukulia rushwa kama ni haki ya mtu fulani kupewa au kutoa, iyo stori haikusaidii sana sana itakutenga na watu wenye msaada kwako.
Ni hayo tu Mkuu ukiona ni muhimu edit uzi wako ukae kwenye hayo mambo manne niliyokushauri.
Asante mkuuPole!
Naona una taarifa chache sana kuhusu hili suala hujachimba vizuri kufahamu hata mwenendo wa kesi, unasema hukuruhusiwa hata kusikiliza umekuta hukumu tayari na nakala huna.
Tafuta mtu wa kukusaidia kwanza kujua mwenendo mzima wa kesi, upelelezi mpaka hukumu, umesema huna hela ni changamoto ila kwanza hapa lazima uwe mnyenyekevu sana kwa kila utakayetaka msaada wake (hutakosa msaada).
Jamii Forum inaweza kua sehemu ya kwanza kwa wewe kusaidika nimeona kuna wadau wanaomba uwape baadhi ya taarifa PM usiwapuuze! Lakini binafsi cha kwanza fuatiliaa mtiririko mzima wa kesi itakupa mwanga wa wapi pakuanzia.
Sijui chochote kuhusu sheria labda basics tu na nipo tayari kukusaidia japo sijajua kwa eneo gani ila kama ni kweli jamaa kaonewa wewe na familia msilale na yeye huko jela atazidi kujifunza pa kuanzia.
Ni sawa lakini kwa nchi zetu hizi, masikini anaonewa sana, kwenye upatikanaji wa haki yake, juzi kuna jamaa , ameachiwa huru baada ya kukaa jela miaka 34, kwa kosa la mauaji, ambalo jaji aliyemuhukumu alimwambia ushahidi haujitosherezi, wa kukufunga ila kutokana na usalama wako, nakufunga maisha!!hahaaaa!!!badaye jaji mwingine alipoipitia akashangazwa na hiyo hukumu, kutokana na ushahidi, na jamaa hata hakukata rufaa!!mwaka jana anashangaa tu anaachiwa!!!Kama kweli hii story yake ni ya kweli. Shaenda magereza, kila mtu anasema kaonewa wote hawajakosa, nawaambieni mahakimu we go 98% hawafungi mtu kwa kumuonea
Asante mkuu kwa ufafanuzi mzuri maana kaka hakua na risti yoyote waliuziana kienyeji afu shahidi upande wa pili walikua ni askari waliowakamataHapa usisingizie umaskini kwani kaka yako ana kosa na hiyo adhabu aliyohukumiwa miaka 30 ni sahihi kwa kosa lililotokea haijalishi ni kweli amefanya au kwa kukutwa na simu ya wizi kama ushahidi. Tambua mkamatwa na ngozi ndiye mwizi kisheria.
Usisingizie umaskini.
Hapa unataka kutuaminisha kwamba iwe ni kweli kaka yako ni jambazi au sio, ungekuwa na pesa ungetoa rushwa ili kaka yako awekwe huru. Hii haikubaliki. Labda ungesema kutafuta msaada wa sheria sawa.
Una uhakika gani kaka yako sio jambazi?
Kaka yako kakusimulia aliuziwa simu na hakuiba. Haukuwepo wala haukushuhudia akiuziwa simu au kuiba. Yote haya yanawezekana. Una uhakika gani hakuipata hiyo simu kwa unyang'anyi wa kutumia nguvu? Kwa vile hapa kulikuwa na ubishani wa pande mbili DPP akimshitaki kuwa ameiba na yeye anakataa. Mahakama inaamua kulingana na ushahidi wa pande mbili yaani DPP na kaka yako. Yeyote anayeishawishi mahakama kwa ushahidi ndiye mkweli. Lakini mpaka hapo maelezo yako yalipoishia yanaonesha ugumu wa kaka yako kujinasua na hili sakata kwani ushahidi unaonyesha alihusika kwa ushahidi wa kukutwa na simu ila anakana kwa maneno pekee. Simu ni ushahidi wa uhusika. Hata kama angempata muuzaji, kama hana ushahidi wa mauziano na muuzaji akakana kumuuzia bado miaka 30 inamhusu. Hapa kujinasua ni mpaka awe na pesa ya kuhonga kama unavyodai.
Ushahidi.
Inaelekea ushahidi pekee ulio nao wewe na kaka yako ni KAZI YA UMACHINGA, SIMU AMEINUNUA basi. Wakati DPP ana ushahidi wa mtu aliyefanyiwa ujambazi na kuporwa vitu kadhaa na pengine cheti cha matibabu, ushahidi wa umiliki wa simu na kaka yako kukamatwa akiwa na hiyo simu ya wizi akiitumia. Unadhani hapo ni nani mwenye ushahidi thabiti na kamili.
Katika utetezi wa kaka yako kukutwa na simu ya wizi atakuwa amesema ameuziwa. Kitu ambacho hata jambazi au asiye lazima atasema hivyo kama sehemu ya utetezi. DPP atakuuliza umeuziwa na nani? Unatakiwa umtambue muuzaji na umuoneshe hakimu mahakamani hapo kama ushahidi ikiwa muuzaji atakuwepo. La kama hayupo uonyeshe karatasi za mauziano. Huna vyote wewe ni mwongo tu sawa na waongo wengine wanaotumia maneno kulaghai. Pia kama muuzaji yupo hapo na akakana kumuuzia ndugu yako, na hakuna ushahidi bado miaka 30 itamhusu kwa kosa la unyang'anyi.
Nini cha kufanya.
Kama anaona kaonewa akate rufaa. Ila ajipange na ushahidi na sio Maneno maneno tu. Vinginevyo kama unavyoamini katika rushwa ya pesa kama unavyodai haukuwa na pesa, utafute pesa ya kumtoa kama unaamini inaweza kumtoa.
Ni sawa lakini kwa nchi zetu hizi, masikini anaonewa sana, kwenye upatikanaji wa haki yake, juzi kuna jamaa , ameachiwa huru baada ya kukaa jela miaka 34, kwa kosa la mauaji, ambalo jaji aliyemuhukumu alimwambia ushahidi haujitosherezi, wa kukufunga ila kutokana na usalama wako, nakufunga maisha!!hahaaaa!!!badaye jaji mwingine alipoipitia akashangazwa na hiyo hukumu, kutokana na ushahidi, na jamaa hata hakukata rufaa!!mwaka jana anashangaa tu anaachiwa!!!
Jamani naomba kuuliza!
Ni simu tu ndio sio vizuri kununua kwa mtu au hata bidhaa za ndani kaama radio, vitanda, fridge nk
Naombeni ufafanuzi kijana wenu nisije kwenda Jera Mana naogopa saana
Kuna rufaa mkuu, usimkatishe tamaa... Awatafute akina Tito Magoti kule Twitter wanaweza kumuelekeza kile kituo cha sheria...Mambo yakishafika kwa pilato huwa magumu.
Kama kumchoma mngemuwahi mapema kule kule kituoni.
SawaMuamini Sana na awe na office, tabu Sana kununua vitu kwa mtu
Ni kosa sana kununua vitu vya wiziDada yangu alikuwa na tabia hiyo ya kununua vitu vya wizi aliwekwa ndani siku tatu akili ikamkaa Sawa
2% iliyobaki inatosha kuchunguza kama kaonewa.Kama kweli hii story yake ni ya kweli. Shaenda magereza, kila mtu anasema kaonewa wote hawajakosa, nawaambieni mahakimu we go 98% hawafungi mtu kwa kumuonea
Mkuu ni vitu Kama simu au hata vitu vya ndani????Ni kosa sana kununua vitu vya wizi
2% iliyobaki inatosha kuchunguza kama kaonewa.
Afanye kutriger kama alivyolileta hapa, attention iwepo ya kutosha atapata msaada.Kabisa, go ahead
Afanye kutriger kama alivyolileta hapa, attention iwepo ya kutosha atapata msaada.
Inawezekana.Sha deal na watu wengi WA hivi unakuta ajaonewa
Pole sana, God is the judge, muchie Mungu amuhukumu kwa haki au kateni rufaa kama familiaKwa ufupi kesi ya kaka angu yeye ni machinga, aliuziwa simu na mtu baada ya kuitumia hiyo simu kama wiki mbili alikamatwa
Kosa ile simu aliyonunua iliporwa kwa nguvu kutumia silaha na kupora vitu baadhi ikiwemo pikipiki, na katika sakata hilo walikamatwa watu watatu akiwemo na yeye.
Wakapelekwa polisi kwa upelelezi badae kesi ikaenda Mahakamani wamekaa miezi tisa mmoja wao alitoka wiki mbili zilizopita wakabaki wawili.
Leo ilikuwa siku ya hukumu na imetokea kama nilivyoeleza hapo juu,
Nimeongea na kaka amelia sana anasema wamefungwa kwa kukosa hela ambapo mwenzao kesi ya pamoja ametoka kwa kutumia pesa. Kwa upande wetu pesa hatuna familia ya kimasikini
Naomba msaada kama kuna utaratibu upi tuutumie kama familia, imeniuma sana kuona kaka anafungwa miaka yote hiyo.
yuda exalioth
Jamiiforms
geita