ile simu aliyonunua iliporwa kwa nguvu kutumia silaha na kupora vitu baadhi ikiwemo pikipiki, na katika sakata hilo walikamatwa watu watatu akiwemo na yeye.
Kaka yako hajafungwa kwa kosa la kuiba simu yeye kafungwa kwa kosa la robbery. Hapa simu haihusiki kwa sababu yeye hakukamata na simu ingawa alinunua simu ya wizi ,tukio la pili la kuibiwa na majambazi wenye silaha ndo kesi yenyewe.
Kitu ambacho ninahisi, maelezo ya kaka yako wenda kukili makosa, hilo ki kosa kubwa kwenye kesi kama hizo.
Nahisi harufu ya kumchongea kesi kuna mtu alikuwa akimtafuta, sasa kapata nafasi.
Kesi kama hizo bila pesa,lazima usote, mambo ya kusema utatokea muujiza sahau.
Weka haki pembeni hilo swala ilibidi mtumie pesa huko police.ilibidi muuze hata kiwanja chake .
Option ilobaki ni kukata rufaa.
Tatizo hamna hela, na kibaya zaid hata hiyo pesa kwa sasa inaweza isisaidie.
Kutokana na imani yangu kichwani nina wazo ambalo ni la kibinadamu zaidi.. Mkifanikiwa kukata rufaaa, angalieni na mazingira mengine kama mtabahatika kupata mtu sahihi. Nimetoa ushauri huu kwa sababu ya experience ya kesi ninazoona mahakamani. Siku ya kusikilizwa rufaa chochote cha weza tokea.life is not fair lazima kuangaika huku na huku.siku zote haki ucheleweshwa
Nb. mimi ni mristo safi nampenda Bwana yesu.