Msaada karibu napata presha

Msaada karibu napata presha

nakuonea huruma.mwanamke anaeipenda ndoa yake,hawezi kumjibu mume kama umechoka uamue.mtasema mengine na si ya kuachana.hasa kama ugomvi sio mambo ya ku cheat.maybe kama ni mpole,kitu gani kinachompa ujeuri?au na wewe una makosa yako?
 
Mnaishije kwani? manake kuna watu wanaishi na wenzi wao kama mtu na mzazi wake. Hebu jaribu kumtreat wife wako kama Best friend wako uone kama kuna kitu ambacho hatataka kushare na wewe...
 
Ni mmachame? kama yes basi mwache uendelee na mambo yako mengine tu atakuletea vidonda vya tumbo!
 
Mayassa, kwa umri wangu nimeona mengi...kuna baadhi ya wanawake hata umtreat vipi, wana preconceived ideas kuhusu ndoa kwa ujumla

Ukute huyo anawaza kwamba "hili ***** limeshanifungulia biashara ni muda wa mimi kujijenga" (hoping for the worst case scenario) na hasa pale ambapo walioana bila wote wawili kuwa na one objetive...
 
Wana JF na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa. mke wangu niko naye miaka 3. tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie. Kuepuka shari mm huwa najishusha nakumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. hajui kusema samahani hata pale anapogungua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nn? nami sitaki kuzurura napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa. wakuu mawazo yenu pls!

Nadhani Nyani mzee angefarijika sana,
kama angepata uzoefu kutoka kwa wenye ndoa,
kwani kwa namna moja au nyingine hao,
watakuwa wemekutana na hali kama hii,
katika safari yao ya maisha ya ndoa!
Au Lizzy na Pauline mnasemaje?
 
Ningefurahi kusikia wadada wanasemaje maana siri zingine ktk mambo kama haya wanazijua zaidi.inaweza kuwa ni ushauri wa mashoga, au wapambe au character ya mtu hasa anaposahau alipotoka. Naamini wanawake great thinkers ni wengi.labda nichokoze mada. Kama ww ni mwanamke nn chaweza kupelekea kuwa na tabia kama hii.kwa vile mume mpole? Au kaonyesha kukujali? Au umepata stay wire kwa hiyo hata kimbunga kije nguzo haianguki au ulimbukeni wa kutojua majukumu tu.au pepo. Great thinkers think great.
 
Wana JF na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa. mke wangu niko naye miaka 3. tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie. Kuepuka shari mm huwa najishusha nakumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. hajui kusema samahani hata pale anapogungua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nn? nami sitaki kuzurura napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa. wakuu mawazo yenu pls!

Unqvyozidi kumuachia bila kureact kua umechukizwa na majibu yake ndo anazidi kuku panda... Ila Bahati nzuri sana kama Bishanga alivyosema kapitie thread ya Upole naamini walau utapata jibu... kila la kheri...
 
Ni mmachame? kama yes basi mwache uendelee na mambo yako mengine tu atakuletea vidonda vya tumbo!
Nachukia mawazo ya aina yako....Ingekua ni Wamachame tu wenyewe matatizo wanaume wengi sana wangekua na raha kwenye ndoa zao
 
Mayassa, kwa umri wangu nimeona mengi...kuna baadhi ya wanawake hata umtreat vipi, wana preconceived ideas kuhusu ndoa kwa ujumla

Ukute huyo anawaza kwamba "hili ***** limeshanifungulia biashara ni muda wa mimi kujijenga" (hoping for the worst case scenario) na hasa pale ambapo walioana bila wote wawili kuwa na one objetive...

Hapo nimekuelewa mkuu..
 
spiritual husband! i have axperienced that before and the situation was just like yours! nilimfungukia saluni ikafika kipindi hataki niende hata kuulizia biashara inakwendaje na always hakukuwa na faida, kila stock ikiisha lazima nitoe pesa mfukoni kununua dawa. kuna siku nilikwenda kwa kushtukiza aliponiona akauliza umekuja fanya nini hapa? i was so shocked na kila kitu ni mimi nimelipia pale, unajua sisi wanaume tunawapenda saaana wake zetu nikageuza zangu mzee home! kuna siku alikuja jioni home akaniambia nimekutana na mchungaji kaniambia chumbani kwako kuna kitu kibaya sana kimewekwa mchungaji akamwambia asali saana ana spirit of death! guys nilikuwa nadhani kuna mwanamme anamtia kiburi lkn niliposikia hayo maneno nikaona kwa nini nisiyafanyie kazi, nikampeleka kwa fernandes ATN akaombewa, SO mkubwa if u r mkristo opt for jesus she will be delivered and you will enjoy her. hapa nilipo na watch MONDAY LIVE SERVICE YA EMMANUEL TV (TB JOSHUA) never a case jesus can not heal, just believe, confess everything and LORD will set you free!! EMMANUEL!!
 
Wana JF na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa. mke wangu niko naye miaka 3. tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie. Kuepuka shari mm huwa najishusha nakumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. hajui kusema samahani hata pale anapogungua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nn? nami sitaki kuzurura napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa. wakuu mawazo yenu pls!

...muulize kwa upole, atakujibu vizuri tu.

Epuka kuuliza kwa lugha ya ukali, au
pale tu panapokuwa pametokea tatizo.
 
yaani natamani tu huo usafiri kwa jinsi nlivyochoka na folen za hapa bongo.USHAURI WANGU KWAKO KAA CHINI NA MKEO MWAMBIE HUPENDI TABIA YAKE NA PIA MARAFIKI NI WAZURI NA NI WABAYA PIA SIYO KWAMBA WATAFURAHIA SANA MAISHA ANAYOISHI YEYE NA MUMEWE, WATAFANYA JUU CHINI ILI KUMHARIBU AKILI JAPO NI MKUBWA.
 
Dawa yake kunyamaza na kuendelea kumtendea wema huku ukiamini kuwa atabadilika. Imani ni dawa.
 
Naweza kuonekana nimetumia lugha mbaya nisamehe kabla hujasoma

Mkeo kabla hujamuoa ulichukua muda kujua tabia yake?

Je mkeo ni mzuri sana na hana elimu?

Wanawake ambao elimu yao ni ndogo afu wazuri wakipata mume wanapenda kumyanyasa na ni rahisi kuendeshwa na kudanganywa na mashoga.

Kuna ndugu yangu alienda nje ya nchi na wife, mke akapigwa lecture na mashoga huko US mume alikuwa anafanya PhD basi mwanamke akahacha kupika anamwambia mmewe mambo ya gender na yeye aingie jikoni huku mwenzie anasoma yeye house wife. Mwisho wa siku bwana karudi bongo mwenyewe na si kuwa alimtaliki, mwanamke kagoma kurudi.

Wanawake waliosoma wana matatizo yao lakini hawadanganywi kirahisi na mashoga.

Huyo atakuwa anadanganywa na marafiki zake huko kwenye bihashara; Utakuta wanamwambia "mimi mme wangu anambii kitu" kumbe wanampotosha ni watii kwa wame zao.

Wewe anzisha varangati, mtimue kwa muda na hivi hana kazi, atakuja kukuomba msamaha na wewe umpe masharti.

Usitoke nje ya ndoa maana hilo litakuwa gonjwa kama kula nyama ya binadamu na wala si solution.

Ningefurahi kusikia wadada wanasemaje maana siri zingine ktk mambo kama haya wanazijua zaidi.inaweza kuwa ni ushauri wa mashoga, au wapambe au character ya mtu hasa anaposahau alipotoka. Naamini wanawake great thinkers ni wengi.labda nichokoze mada. Kama ww ni mwanamke nn chaweza kupelekea kuwa na tabia kama hii.kwa vile mume mpole? Au kaonyesha kukujali? Au umepata stay wire kwa hiyo hata kimbunga kije nguzo haianguki au ulimbukeni wa kutojua majukumu tu.au pepo. Great thinkers think great.
 
Wana JF na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa. mke wangu niko naye miaka 3. tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie. Kuepuka shari mm huwa najishusha nakumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. hajui kusema samahani hata pale anapogungua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nn? nami sitaki kuzurura napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa. wakuu mawazo yenu pls!

Simama kama mwanaume muulize panapotakiwa kuuliza,asipotoa ushirikiano kuwa mkali kama akizidisha ukorofi funga biashara yake,wewe ni mwanaume lazima uwe kiongozi wa familia!
 
Huyo anaujuwa udhaifu wako! Ndio sababu anataka akutawale! Sasa na wewe jikakamue vyovyote vile usijali lolote la si hivyo atakufanyia vibaya huyo! Utakuja umia sana rafiki. NASSOR JANGWA MTANDAONI.
 
Mnaishije kwani? manake kuna watu wanaishi na wenzi wao kama mtu na mzazi wake. Hebu jaribu kumtreat wife wako kama Best friend wako uone kama kuna kitu ambacho hatataka kushare na wewe...

Hapo kwenye red ni maneno mawili tuu lakini yana uzito mkubwa. Probably ndio wewe pekee ambaye umejaribu kuliangalia hili suala kwa upana zaidi. Wengine wame-sympathise tuu na kumshauri mdau achukue action. Lakini hapa inawezekana tunajua tuu nusu ya story nzima. Ni vigumu kutoa ushauri kwenye suala nyeti kama hili kwa kutegemea maelezo mafupi ya upande mmoja. Hata hivyo kama imefikia hatua ya mke wako kukuambia "usinisimange au kama umechoka niambie" then masuala ni magumu hapo.

Kumfungulia duka na kumnunulia gari sidhani kama ni vigezo vya kumfanya mwanamke wa ukweli akuheshimu. Labda wale ambao ni material women. Pia baadhi wakishawanunulia wake zao vitu kama hivyo wanajisahau kabisaaaa. Mwanamke huwa anataka atoshelezwe pia kwenye mahitaji ambayo ni natural kwake. Hili bado hatulijui. Nafikiri ndio maana Mayassa akakuuliza mnaishije kwani? NyaniMzee usinifikirie vibaya, lakini kama umesoma posts zangu kwenye ile topic aliyoianziasha Lizzy ya Upole, nitakuuliza the same brutal question. Mnaishije kwani? Kama Mayassa alivyouliza mlikuwa na common objective mlipokuwa mnaoana? Sio hilo tuu; kama wewe ni mkristu jaribu kusoma Proverbs 18:22 na Isaiah 48:17. Then, jiulize did you do your homework in finding not only a wife but a fit wife? Emphasis kwenye neno "fit".
 
Wana JF na hasa wale wenye weledi na mambo ya ndoa. mke wangu niko naye miaka 3. tuna mtoto 1 wa miaka 3. Nimemfungulia biashara nzuri anaingiza pesa nzuri tu kwa siku. Usafiri nimempa wa kumpeleka kazini kwake na kumuwahisha home. Tatizo moja linanikwaza: nikitaka kujua maswala yanayohusu pesa au marafiki zake hata wa kike tu basi majibu yake huwa ni mkato na ya jeuri na hachelewi kusema usinisimange au kama umechoka niambie. Kuepuka shari mm huwa najishusha nakumtuliza kuwa haikuwa kwa nia ya kumkwaza bali kama mume nina haki kujua. hajui kusema samahani hata pale anapogungua alikosea kauli. Sasa haya maisha dawa yake nn? nami sitaki kuzurura napenda niishi naye kama ahadi ya ndoa. wakuu mawazo yenu pls!

Mkuu hapo umepatikana. Si vibaya kutaka kujua financial status ya hiyo biashara yenu ingawa hujasema ni biashara gani. Huyo mke nae vipi mbona hayuko na uelewa wala hayuko wazi.
My take: Kuna hela inaingia na anakutia ndani sasa sijui kama ni just cuz she's greedy ama ni tamaa ya kujilimbikizia. Kazi unayo na pole na kupandishwa pressure.
 
Back
Top Bottom