Msaada: kesi ya ajali ya pikipiki

Msaada: kesi ya ajali ya pikipiki

Kichaka12

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2018
Posts
300
Reaction score
263
Wakuu wanasheria natumaini mko poa.

Nilinunua pikipiki juma tano na niliambiwa kuwa kadi haijafika tukapewa chases number tukarudi. Jumamosi nikiwa safarini nikaambiwa dogo amegonga mtu na huyu dogo hana lesen. Kachukuliwa yeye na pikipiki yeye aliwekwa mahabusu then kuna mtu kaenda kumuwekea dhamana akatoka.

Sasa ni taratibu gani nichukue niipate pikipiki yangu kwa usalam?

Maana askali analazimisha kesi iende mahakamani na dogo aliyegonga na aliyegongwa wamekubaliana tu kuwa mgonjwa ahudumiwe ili mambo yasiwe mengi.

Kama kuna maelezo zaidi nitajibu naomba nisirefushe sana tread.

Natumaini nitasaidiwa.
 
Pole sana ndugu ukiona askari anakuzidia bora uipeleke mahakamani tu linaisha kikubwa makubaliano ya wahusika yamefikiwa
 
Kifupi askari anataka hela(poshokubwa) sababu anajua kosa la kuendesha chombo cha moto huna leseni itakuwa ni kipengele kizito kidogo.
 
Kifupi askari anataka hela(poshokubwa) sababu anajua kosa la kuendesha chombo cha moto huna leseni itakuwa ni kipengele kizito kidogo.
Adhabu zake kwa mujibu wa sheria ikoje kwa kosa la kuendesha pikipiki bila lessen?
 
Pole sana ndugu ukiona askari anakuzidia bora uipeleke mahakamani tu linaisha kikubwa makubaliano ya wahusika yamefikiwa
Yeye pia (askari) anataka kesi iende mahakan sasa kwa mujibu wa hizo sheria jambo haliwezi kuleta tatizo zaidi?
 
Back
Top Bottom