Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Nachojua kuna dawa za asili ambazo watu hupewa kuacha pombe maana kuna ndugu yetu alisumbua sana watu ila alipofikia hatua ya kuchezea kazi, watu ndio wakamuwinda kwa kumchanganyia kwenye "kinywaji" Ila akashtuka, so sijui ipo effective vipi maana hawakuwahi mdaka .. Labda Mshana Jr atachangiaAhsante sana kaka nimezichukua point zote sita (6) baadhi tayari ndio nazifanyia kazi, mfano nilikuwa nakaa sehemu ambayo mimi ndio msomi jamii yote inayonizunguka ni jamaa zetu tu wa kazi za kawaida na wengine ni wazee wastaafu, nimehama almost mbali kabisa na kuanzia dec 1 ndio Kodi yangu inaanza kusoma.
Then, Kama hutojari au yeyote anayesoma comment hii nataka kujua ni maombi ya aina gani binadamu unaweza kumuomba mungu kwa kuongea nae kabisa ili akutoe kwenye kifungo cha pombe ?
Pili, Ngoja nishare story moja na wewe hapo nyuma kuna rafiki yangu wa kike baada ya kuhangaika sana akaniambia basi twende kwa bwana mmoja hivi (Shekhe) tumefika pale yule jamaa akaniuliza maswali machache ikiwemo jina langu, jina la Mama, jina la baba, akapiga hesabu zake pale akasema wewe tatizo lako ni namba moja. Yaaani utazunguka weee Ila tatizo ni namba moja, Sasa mbona alinipa dawa zake nikatumia lakini sijafanikiwa ?
Ndio maana naomba wajuvi wa Imani yangu (mkristo) natokaje hapa ? Ahsante
Kuhusu maombi kuna levels, hata mimi tu sipo kiroho sana ila kuna watu wapo deep ambao wanaweza kukufundisha jinsi ya kusali na ukafanikiwa.
Pia naamini kama pombe inakutesa na unahangaika kuachana nayo kiasi hicho bila mafanikio. Aidha tayari una addiction ambayo si rahisi kuishinda au la, Kuna vitu vinakusumbua katika maisha yako na huwa unaitumia pombe kama escape.
Kumbuka brother, unapoamua kung'oa mti kwenye nyumba , huwezi kuondoa matunda, mashina na matawi yake huku ukiuacha mzizi maana bado utamea tu. Kwa hiyo kama pombe ni escape au impact ya kitu flani bhasi yenyewe sio tatizo ila kiini ni kile kinachokupelekea kunywa. Na usipopambana nacho bhasi pombe hutoweza kamwe kuiacha