MSAADA: Kila biashara ikianza kuchanganya nasimamisha kila kitu, nakuja kuzinduka wakati nimeshaharibu pakubwa

MSAADA: Kila biashara ikianza kuchanganya nasimamisha kila kitu, nakuja kuzinduka wakati nimeshaharibu pakubwa

Ahsante sana kaka nimezichukua point zote sita (6) baadhi tayari ndio nazifanyia kazi, mfano nilikuwa nakaa sehemu ambayo mimi ndio msomi jamii yote inayonizunguka ni jamaa zetu tu wa kazi za kawaida na wengine ni wazee wastaafu, nimehama almost mbali kabisa na kuanzia dec 1 ndio Kodi yangu inaanza kusoma.

Then, Kama hutojari au yeyote anayesoma comment hii nataka kujua ni maombi ya aina gani binadamu unaweza kumuomba mungu kwa kuongea nae kabisa ili akutoe kwenye kifungo cha pombe ?

Pili, Ngoja nishare story moja na wewe hapo nyuma kuna rafiki yangu wa kike baada ya kuhangaika sana akaniambia basi twende kwa bwana mmoja hivi (Shekhe) tumefika pale yule jamaa akaniuliza maswali machache ikiwemo jina langu, jina la Mama, jina la baba, akapiga hesabu zake pale akasema wewe tatizo lako ni namba moja. Yaaani utazunguka weee Ila tatizo ni namba moja, Sasa mbona alinipa dawa zake nikatumia lakini sijafanikiwa ?

Ndio maana naomba wajuvi wa Imani yangu (mkristo) natokaje hapa ? Ahsante
Nachojua kuna dawa za asili ambazo watu hupewa kuacha pombe maana kuna ndugu yetu alisumbua sana watu ila alipofikia hatua ya kuchezea kazi, watu ndio wakamuwinda kwa kumchanganyia kwenye "kinywaji" Ila akashtuka, so sijui ipo effective vipi maana hawakuwahi mdaka .. Labda Mshana Jr atachangia

Kuhusu maombi kuna levels, hata mimi tu sipo kiroho sana ila kuna watu wapo deep ambao wanaweza kukufundisha jinsi ya kusali na ukafanikiwa.

Pia naamini kama pombe inakutesa na unahangaika kuachana nayo kiasi hicho bila mafanikio. Aidha tayari una addiction ambayo si rahisi kuishinda au la, Kuna vitu vinakusumbua katika maisha yako na huwa unaitumia pombe kama escape.

Kumbuka brother, unapoamua kung'oa mti kwenye nyumba , huwezi kuondoa matunda, mashina na matawi yake huku ukiuacha mzizi maana bado utamea tu. Kwa hiyo kama pombe ni escape au impact ya kitu flani bhasi yenyewe sio tatizo ila kiini ni kile kinachokupelekea kunywa. Na usipopambana nacho bhasi pombe hutoweza kamwe kuiacha
 
Samahani kwa mwandiko mbovu kidogo ila naandika nikiwa nina hasira sana baada ya jamaa yangu kuniletea taarifa nimekosa zaidi ya mil 2 kizembe sana.

Mimi ni kijana wa taaluma ya sheria na biashara, naweza sema nina kipaji maana nimekuwa msaada kwa watu wengi sana, na pia kuna wengine wamekuwa wakifanya mimi kuwa kama daraja kwako, sio kwamba nipo competent hapana ila nina inborn character ambayo naweza fanya jambo lako likafanikiwa tena kiurahisi tena kwa gharama ndogo sana.

Sasa hapa katikati nilifungua ofisi (mpaka leo ipo) maeneo ya Buguruni. Namshukuru Mungu nilianza kwa masihara tu ila baada ya watu kujua huduma zangu nikaanza kuaminika sana (hata na watu wa humu JF).

Shida ni moja, kwa siku za karibuni nimekuwa napata hali isiyo eleweka, naweza kufunga office hata wiki mbili bila sababu yoyote na wala hata simu sipokei, baadae akili inarudi naambiwa yaani watu walikuwa wananitafuta sana na nimekosa hela kabisa.

Mara ya kwanza niliona ni kawaida tu nikaenda kanisani, nikasali lakini labda mniambie nakosea wapi jamani.

Yaani kwa kifupi, huwa na loose kila kitu hadi nauli nakosa, ila nikija ofisini nikianza kufanya kazi ndani ya muda mchache tu hata wiki mbili, kazi zinachangaya napata clients wapya na madili kibao, nikianza ku take off tu sijui kitu gani huwa kinaniingia basi wale wateja wote nawapoteza na hata kuingia madeni fedheha pamoja na kuitwa tapeli.

Yaani hii hali inaniumiza sana sababu baada kama ya wiki moja ndio akili inakuja na nagundua kwamba nina office. Wakati mwingine nachelewesha kazi za watu na mambo mengi kibao.

Juzi tu kulikuwa kazi yaani ya bure kabisa kuna documents fulani hivi kuziandika na kufuatilia vibali kwenye taasisi fulani. Mteja alifika almost 2M sasa huyo jamaa aliyemleta ameniambia alinitafuta karibia siku 4 mpaka kazi akaenda kumpa mtu mwingine. Mimi simu sipokei nimekaa tu sehemu sijielewi ila muda huo nakuwa nakunywa pombe.

Jamani naomba kusaidiwa, mbona nasali sana au sijui kusali? Nina laana? Mbona naomba toba kila siku? Nalogwa (hapa sina uhakika sababu ninasumbuliwa sana na ndoto za ajabu)?

Nifanye nini? Vijana wenzangu wanaendelea mimi nipo pale pale! Nina taaluma, nina office tena ya kwangu, ila maisha yangu hayaeleweki?

Naomba msaada jamani wa kiroho au kimwili.

Mungu awabariki.
Mkuu una mikosi nuksi na vifungo vinavyo kusababisha usiendelee kibiashara nitafute mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate mafanikio katika biashara yako.
 
Watu wengi ambao mambo yao yanaharibika sababu ya utumiaji wa pombe uliopitiliza sio watu wazuri wa kupokea ushauri na kuufanyia kazi.

Hubadilika tu pale mambo yanapokwenda kombo (learning the hard way). Mfano kufukuzwa kazi, kukimbiwa na mke, kupoteza biashara, kuharibu mahusiano na wadau. Etc.

Mkuu jichunguze, achana na visingizio
Fact
 
Nachojua kuna dawa za asili ambazo watu hupewa kuacha pombe maana kuna ndugu yetu alisumbua sana watu ila alipofikia hatua ya kuchezea kazi, watu ndio wakamuwinda kwa kumchanganyia kwenye "kinywaji" Ila akashtuka, so sijui ipo effective vipi maana hawakuwahi mdaka .. Labda Mshana Jr atachangia

Kuhusu maombi kuna levels, hata mimi tu sipo kiroho sana ila kuna watu wapo deep ambao wanaweza kukufundisha jinsi ya kusali na ukafanikiwa.

Pia naamini kama pombe inakutesa na unahangaika kuachana nayo kiasi hicho bila mafanikio. Aidha tayari una addiction ambayo si rahisi kuishinda au la, Kuna vitu vinakusumbua katika maisha yako na huwa unaitumia pombe kama escape.

Kumbuka brother, unapoamua kung'oa mti kwenye nyumba , huwezi kuondoa matunda, mashina na matawi yake huku ukiuacha mzizi maana bado utamea tu. Kwa hiyo kama pombe ni escape au impact ya kitu flani bhasi yenyewe sio tatizo ila kiini ni kile kinachokupelekea kunywa. Na usipopambana nacho bhasi pombe hutoweza kamwe kuiacha
Aisee Ahsante sana sana na Sana, nitaendelea kusoma uzi huu maana nateseka na najiona kabisa nateseka sababu huwa napata majuto makubwa Sana, Ukiendelea kupata mawazo mengine basi usichoke kuandika naamini ipo siku nitatimiza mwaka bila kunywa pombe, nikiweza hapo Basi Tena sitakunywa tena pombe kwenye maisha yangu. Ahsante sana
 
Matatzo yako ni mawili kwanza pombe na kuamini uchawi jitahd uachane nayo.
 
Ajiri mtu Kuna watu wengi wanatafuta sehemu za kujishikiza nankupata uzoefu mtu huyo sio lazima.umlipe saaana wengi tunaogopa kuaniri watu kumbe tunajibebesha kazi nyingi mpaka tunachoka Ni afadhali ofis Iwe wazi hata kama were upo bize ...lakininpia Ni Jambo la kiroho hilo lengo Ni kukurudisha nyuma Kuna msari fulani umecholewa usiuvuke ukitaka uuvuke tu lazima uzingue....you need blood of Jesus kuweka makbo sawa
 
Nipo kwenye process ya kuajiri mtu ahsante Sana kwa ushauri. Kuhusu hii ya kucholeshwa line nahisi nataka kuamini Ila nakuwa mzito sana sababu sitaki kuiweka kichwani, Ila naomba njia sahihi ya kuomba au kusali ili kuifuta hii line mkuu, Kama hutojari na unajua please share nami hata PM
 
Back
Top Bottom