Msaada: Kilimo cha Matango, Utaalam na Masoko

Nakubaliana na Malila soko ni la uhakika ,ila msimu huu maana ndo tunavuna ,soko si zuri sana bei imeshuka mno kwa sehemu za pwani.

Mkuu ni kuanzia miezi gani Matango huwa na bei nzuri sokoni?
 
Poleni na majukumu wakuu wa jamvi hili maridhawa.
Naomba mwenye utaalamu juu ya kilimo cha matango anisaidie kujibu hoja zifuatazo:
1. Mbegu kiasi gani zinatosha heka moja.
2. Spacing yake kwenye upandaji ikoje?
3. Msimu mzuri wa kulima matango ni upi.
4. Mahitaji muhimu.
5. Wastani wa gharama za kulima heka moja.
6. Wastani wa mapato kwa heka moja.

Natanguliza shukrani za dhati kwa wote wakaochangia mawazo yao hapa. Ahsanteni sana.

Nawasilisha!
 

Wadau jitokezeni niwahi shambani.
 
Ngoja wataaalamu waje, binafsi nina interest hapa
 
EDUARDO=naam napenda kukupa hongera ila vilevile nenda katafute daktari ktk maduka ya madawa yaliyopo karibu yenu ili wakupe ushauri bora/ KILA LA_KHERI MKUU..
 
EDUARDO=naam napenda kukupa hongera ila vilevile nenda katafute daktari ktk maduka ya madawa yaliyopo karibu yenu ili wakupe ushauri bora/ KILA LA_KHERI MKUU..

Ushauri mzuri lakini maduka mengi wanaweka watu wasiowataalamu. Kuna siku nilikuwa naulizia mbegu ya hoho nikaambiwa kuna mbili za bei tofauti nikamuuliza tofauti yake nini, muhudumu anasema hajui, sikuona sababu ya kuendelea kuuliza zaidi maana nilijua sitapata majibu sahihi
 

Upandaji cm 60 kwa 60 shina hadi shina mstari hadi mstari, tuta hadi tuta inategemea na eneo lako, uwe na uhakika wa maji panda mda wowote, ila matango yanasoko zaidi kipindi cha joto. kuhusu mbegu tembelea maduka au wakulima wa eneo lako watakushauri
 
Habari wakuu,naomba kusaidiwa kuhusu kilimo cha matango kwa wale wazoefu na wataalamu wa kilimo hiki naomba mchanganuo kuanzia mbegu nzur,jinsi kinavyolimwa mpaka kukua yaan kufikia kuvuna inachukua muda gan,pamoja na changamoto zinazojitokeza katika zao hili yaan naitaji kujua hatua zote muhimu za ulimaji wa zao hili pamoja na soko lipo? msaada waku nina eneo kubwa sana la bonde na mto mkubwa upo naitaji kuanzisha kilimo hichi.
 
huku kwetu tunalima ndoo moja 8000-10000
 


Mkuu Martin Mhina, vipi ulifanya hiki kilimo cha matango? naomba unipe uzoefu wako kaka, nami nafikiria hii kitu
 
Wadau habari, nimesikia mahali kwamba matango ni zao linalokua kwa muda mfupi sana na lina faida kubwa. Mwenye utaalam na hatua zote tangu uandaaji wa shamba, aina ya mbegu, uhudumiaji wa zao lenyewe na upatikanaji wa masoko. Asanteni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…