Msaada kimawazo kuhusu usajili wa kampuni ya Uhandisi

Junior16

New Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
4
Reaction score
1
Wadau wa JamiiForums habari zenu, Mimi Ni graduate engineer kwenye kozi ujenzi barabara na majengo ngazi ya Diploma, hivyo Ninaomba msaada wa kimawazo Kuna contractor ambaye alinisihii nimsajilie mwanae kampuni kutumia cheti changu na ya kwamba atanizingatia katika kazi kama engineer.

Naombeni mnisaidie kimawazo
 
Amekuahidi utapata share kiasi gan?
 
Hapo kwenye shares atujaliongelea..kinagaubaga
 
Wadau wa JamiiForums habari zenu, Mimi Ni graduate engineer kwenye kozi ujenzi barabara na majengo ngazi ya Diploma,

Engineer mwenye diploma. Only in Tanzania.

NB: Acha mchezo na taalauma za watu.
 

Wewe umesajiriwa na board ?
 
Ndo nipo kwnye mchakato wa mwanzo kabisa wa usijili..mzee
 
Kwanza tafuta jina la kampuni kisha nenda brela ukasajili , baada ya hapo utaenda CRB (contractors registration board) ipo mitaa ya posta, utapewa form ambayo inaonesha unatakiwa vtu gani usubmit ili uweze kusajiliwa Kama kampuni ya ujenzi. Baada ya hapo Kuna kwnda TRA kulipa Kodi, halmashauri, kisha CRB tena ndo watakupa class (class one ndo kubwa na ndogo ya mwisho Ni class 7). Utapewa class kutokana na vigezo ulivyokua navyo(ambavyo vimeandkwa kwnye form utakayopewa CRB).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…