Msaada kisheria kuhusu mirathi

Msaada kisheria kuhusu mirathi

changwe

Senior Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
159
Reaction score
44
Samahani naomba kujulishwa mgawanyo wa mirathi kisheria iwapo baba alifariki akaacha watoto wakiwa madogo mahakama na ukoo wa baba ukateua msimazi wa mirathi sasa watoto wameshafikisha miaka 18 wanafuata taratibu zipi kupata haki yao kila mmoja
 
Msimamizi wa mirathi anapaswa kufanya mgawiwo huo ambapo ni vizuri zaidi mkasimamiwa na watu wakubwa wakati wa kugawana. Baada ya hapo, msimamizi wa mirathi atapeleka taarifa juu ya mgawiwo huo na mahakama itaangalia kama mmeridhia...
 
Nashukuru sana nameless girl,msimamizi anagawa mali zile kwa watoto wa marehem tu au pia na ndugu wa marehem kama dada zake na mama yake marehem?
 
Jambo la msingi la kufahamu ni kwamba hata mgawo wa mirathi hufanyika kwa mujibu wa sheria. hivyo bsi ni lazima kwanza ifahamike mirathi hiyo itagawanya kwa sheria za dini, sheria za nchi au za kimila kama haukuachwa wosia. ili kufikia hatua hiyo(kutambua mgawanyo utafanyika kwa sheria ipi) kifungu cha 88 cha sheria ya usimamizi wa mirathi kitafuatwa ili kujua namna mirathi itavyogawanywa. kisha msimamizi wa mirathi ataigawa mali ya marehemu kwa warithi kwa mujibu wa sheria itakayoongoza na kuwasilisha hesabu zake kwa mahakama ili kuona uhalali wa mgawo
 
Samahani naomba kujulishwa mgawanyo wa mirathi kisheria iwapo baba alifariki akaacha watoto wakiwa madogo mahakama na ukoo wa baba ukateua msimazi wa mirathi sasa watoto wameshafikisha miaka 18 wanafuata taratibu zipi kupata haki yao kila mmoja

Watoto wapi wa ndoa au wa nje ya ndoa? We ni dini gani maana waislamu wanatawaliwa na sheria za kiislamu za mirathi. Baba yako alikufa lini na wewe umetimiza miaka 18 lini? Kwa kifupi ili ushauliwe vizuri weka taarifa kamili maana kuna time limitation kwa kila utakachokidai! Kuna mgogoro wowote au?
 
Regards kwa wachangiaji wengine.

Maoni yangu:

1. Je, aliyefariki alikuwa anatumia/anaishi kwa imani ipi ya dini. Ikiwa ni muislam, basi Quran imetoa mgawanyo kamili; ikiwa ni kimila, basi mila zake alizokuwa anaziishi zitaongoza mgawanyo (ila mila zinabagua akina mama na watoto wa nje, ijapokuwa academics na courts of law are jealous of this outdated sheria za kimila); na ikiwa ni mkristo, basi atatumia sheria ya the Indian Succession Act, 1865. Always remember, kuwa mambo haya yote shall be subject to kuwepo au kutokuwepo kwa WOSIA.

Nitaendelea baadae...mpaka jinsi ya mrithi anavyokuja kumiliki urithi wake practically.
 
Nashukuru sana nameless girl,msimamizi anagawa mali zile kwa watoto wa marehem tu au pia na ndugu wa marehem kama dada zake na mama yake marehem?

Inategemea kama hilo swala litafanyika kidini ama kimila...
 
Mirathi inafanyika kwa sheria za nchi watoto wote ni wa ndani ya ndoa marehemu hakuacha wosia kama msimamizi anagawa mirathi wengne watakaohusika ni kina nani tofauti na watoto wa marehem
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi na wosia haukuachwa, kama baba amefariki warithi wa marehemu watakuwa ni watoto na mke wa marehem.
ndugu si warithi hapo hivyo hawahusiki.
 
Msimamizi wa mirathi anapaswa kufanya mgawiwo huo ambapo ni vizuri zaidi mkasimamiwa na watu wakubwa wakati wa kugawana. Baada ya hapo, msimamizi wa mirathi atapeleka taarifa juu ya mgawiwo huo na mahakama itaangalia kama mmeridhia...

Name less girl, unasoma sheria? Haya mambo yana time limitation? Kila utakachokidai kina time limitation. huyo alitimiza umri wa miaka 18 lini? imepita mika mingapi tangu atimize miaka 18 etc!ni mambo muhimu sana hayo kuyajua
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi na wosia haukuachwa, kama baba amefariki warithi wa marehemu watakuwa ni watoto na mke wa marehem.
ndugu si warithi hapo hivyo hawahusiki.

Mke siyo mrithi a mali za mume wake. Yeye anapata haki yake katika ndoa! Uliza zaidi upate sheria inasemaje
 
"Mke siyo mrithi a mali za mume wake. Yeye anapata haki yake katika ndoa"

Hiyo haki anayoipata inatoka ktk mali waliyochuma na mume wake. mumewe akiwa hai halafu wakaachana inakuwa haki ya kawaida kupata sehemu ya nguvu yake lakini kwa kuwa mumewe amekufa, ni haki ndiyo anaipata toka mali ya urithi.
 
Vp mama wa marehemu nae ni mrithi?

Kwa kuwa sheria inayotumika hapo ni sheria za nchi, mama wa marehemu si mrithi. ingekuwa ni sheria za kiislam basi mama wa marehemu angekuwa ni miongoni mwa warithi.
 
Kwa kuwa sheria inayotumika hapo ni sheria za nchi, mama wa marehemu si mrithi. ingekuwa ni sheria za kiislam basi mama wa marehemu angekuwa ni miongoni mwa warithi.

vp ndugu yangu endapo baba kafarik na mama na watoto wao wa kiume pia wamebak wanawe wa kike na wajukuu wa watoto wa kiume urith unasemaje hapo kwa sheria za nchi?
 
Ni hv ndugu yangu DUNIA TABU mimi na mke wangu tumefariki lakin wakati huo tulikua na watoto wanne,wawil kiume hawa mmoja wa kwanza mmoja wa mwisho na wawil wakike,baadae mtoto wa kwanza wa kiume kafarik wamebak madada na mdogo wao wa kiume ambao hao wote wanangu watatu waliobak wana watoto wao ambao n wajukuu zangu na hata yule kaka yao mkubwa alyefarik aliacha watoto wawil wa kiume ambao nao n wajukuu zangu,sasa hapo urith unagawiwaje ksheria za nch,n wakristo,mila zao n watu wa mbeya.
 
Wanakuja! ingekua cc, wajukuu hawana haki ya urithi kisheria!
 
Inategemea yupi alianza kufariki kati ya wazazi na huyo mtoto.
endapo mtoto alianza kufariki inamaana urithi wa wajukuu utakuwa ni mali ya baba yao. hivyo kwa kuwa babu na bibi zao bado wapo basi urithi wao utaishia kwa mali za baba yao zilizopo wakat huo, babu na bibi wakifa baadae urithi hautawahusu.
lakin ikiwa babu na bibi wameanza kufa, mtoto (baba wa wajukuu) akawa hai anakuwa ni mrithi kama wale watoto watatu wengine. hivyo ikatokea naye akafa, ule urithi wake alotakiwa kuupata utaenda kwa watoto wake, hivyo ktk mchanganuo wa pili wajukuu wa mtoto aliyefarik watakuwa na haki na mali ya babu/bibi yao kupitia ile sehemu ya baba yao. lkn wale wajukuu wengine hawatakuwa na haki ya kupata urithi wa babu/bibi yao kwa kuwa wazazi wao ambao ndiyo warithi halali wapo.
 
Wanakuja! ingekua cc, wajukuu hawana haki ya urithi kisheria!
Mpwa vipi kuhusu mrejesho ulipoenda kwa 'mtaalam' kuwafanyia walokuibia vifaa vya gari??? Nina hamu ya kuupata asee
 
Back
Top Bottom