Naomba ushauri nataka kujua vitu gan vinahitajika kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kusindika maziwa na product zake zingine na mtaji ni sh ngapi inabid nitafute maana nataka nianze na iyo ila plan kubwa nataka kudeal na mazao ya kilimo kuyaprocess kwenye viwanda vidogo nitakavyoweza kuanzisha kadiri ya mungu atakavyojalia asante
Mkuu wazo lako zuri
Wadau mbali mbali wamechangia vema nasi ngoja tuongeze au kuboresha kwa namna moja au nyingine ambayo inaweza kuongeza thamani ya maandiko
1. Andaa au tafuta wataalamu wakuandalie maandiko matatu ambayo ni
a)business plan
Hii itakusaidia kuwa mwongozo wa masuala mbali mbali yako kuanzia maelezo ya biashara, vibali vya taasisi mbali ambazo utahitaji kuvipata km TFDA, TBS, vyama vya wahamasishaji unywaji maziwa nk, gharama zote na matarajio yako ya mauzo na faida walau kwa miaka mitatu mbele toka kuanza kuzalisha
2. Business feasibility study
Hii itaangalia masuala mazima ya masoko, bei, washindani na njia mbali mbali za kuifikisha bidhaa yako kwa soko
3. Work plan
Hii itakusaidia kukupa mwongozo wa unafanya biashara na nani kama mdau mshirika na si mteja na mshirika mteja. Itakusaidia kuangalia ufanye biashara vipi na wateja kwa style zipi nk
=>Katika vibali
Hapa msingi wa kupata barua za utambulisho kwenda taasisi nyingine kama manispaa kwa ajili za leseni ya uzalishaji na uuzaji maziwa, tbs ubora na tfda usalama na taasisi au vyama wadau hutokea Sido. Ina maana hii michanganuo yako utaipeleka SIDO wao wana wataalamu watakupa ushauri wa andiko lako, muundo wa kiwanda na vilevile utaalam elekezi. Kwa uzoefu wetu kozi hizi hazina muda maalum na huwa zinakuwa za kukuboresha zaidi na kukupa cheti, hivyo jitahidi kupita kwa wadau wajuzi au kuajili watu wajuzi waliosomea food processing. Hii ina maana katika kupeleka barua mfano tfda ina mana barua inakuwa ya utambulisho inatoka sido baada ya wewe kuwaandikia barua ya kuomba utambulisho tfda au tbs nk!
Tusiogope kuwa tfda labda wasumbufu si kweli kwa sababu umeruka vipengele hivi vya mwanzo. Tfda watakujibu na watakuja wataalam wao kuangalia eneo lako la kiwanda na mpangilio wako umekaaje wa mashine za uzalishaje nk. Lakini tambua mwanzo tayari ulishapata kutembelewa na Sido hivyo hata kma marekebisho yatakuwepo yatakuwa kwa kiwango kidogo.
Suala la kibali toka Tbs ni kweli hupatikana baada ya kuanza kuzalisha bidhaa yako kwani huchukua sample kwa ajili ya kuipima kujua ubora wa bidhaa hiyo. Na tena kwa sasa kama mjasiriamali mdogo ni buree kupata tbs ya bidhaa yako
Kwa maelezo zaidi tafuta wataalam washauri wa kibiashara walio jirani nawe au karibu i-business consult. Maoni au ushauri email:iconsultbuzness@gmail.com, hotmail 0659211222