Msaada kiwanda kidogo cha maziwa

Msaada kiwanda kidogo cha maziwa

Asante kwa michango yenu wote.Ila swali moja hamjajibu course za Sido ni muda gani na wanahitaji elimu gani
 
Familia yetu tuna idea kama yako lakini plan ni pale tutakapoweza kuzalisha maziwa yetu at least kuanzia lita 300 hadi 1000 kwasasa tuna lita 80 kwa siku Mungu akijaalia mwakani mwezi wa 6 tutakuwa na uwezo wa kuzalisha lita 150. Tuko meli moja ushauri utakaotolewa utasaidia wengi
Mmefikia wapi?
 
Kabla ya yote, onana na jamaa wa TFDA ili wakuambie 'sera' zao kuhusu mradi huu.
Maana, unaweza ukawekeza sana, halafu jamaa hawa wakaja kupiga kufuli kiwanda chako.
Jamaa hawa kero sana hawa..!!
kweli mkuu
 
please
Kaka,TFDA na TBS ni taasisi mbili tofauti na ziko chini ya wizara mbili tofauti.
TFDA iko chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii na inasghurika na ubora wa dawa na chakula na usalama kwa mlaji LAKINI TBSA ipo chini ya wizara ya Viwanda,Biashara na Masoko yenyewe inashughulika na viwango vya ubora vya bidhaa vyote katika sekta zote

Naweza nikakusaidia namna ya kufuata procedure na kusajiriwa na hawa jamaa.
Asante
namimi nahitaji msaada wako ktk kusajili bidhaa zangu
 
Naomba ushauri nataka kujua vitu gan vinahitajika kwa ajili ya kiwanda kidogo cha kusindika maziwa na product zake zingine na mtaji ni sh ngapi inabid nitafute maana nataka nianze na iyo ila plan kubwa nataka kudeal na mazao ya kilimo kuyaprocess kwenye viwanda vidogo nitakavyoweza kuanzisha kadiri ya mungu atakavyojalia asante
Mkuu wazo lako zuri
Wadau mbali mbali wamechangia vema nasi ngoja tuongeze au kuboresha kwa namna moja au nyingine ambayo inaweza kuongeza thamani ya maandiko
1. Andaa au tafuta wataalamu wakuandalie maandiko matatu ambayo ni
a)business plan
Hii itakusaidia kuwa mwongozo wa masuala mbali mbali yako kuanzia maelezo ya biashara, vibali vya taasisi mbali ambazo utahitaji kuvipata km TFDA, TBS, vyama vya wahamasishaji unywaji maziwa nk, gharama zote na matarajio yako ya mauzo na faida walau kwa miaka mitatu mbele toka kuanza kuzalisha
2. Business feasibility study
Hii itaangalia masuala mazima ya masoko, bei, washindani na njia mbali mbali za kuifikisha bidhaa yako kwa soko
3. Work plan
Hii itakusaidia kukupa mwongozo wa unafanya biashara na nani kama mdau mshirika na si mteja na mshirika mteja. Itakusaidia kuangalia ufanye biashara vipi na wateja kwa style zipi nk
=>Katika vibali
Hapa msingi wa kupata barua za utambulisho kwenda taasisi nyingine kama manispaa kwa ajili za leseni ya uzalishaji na uuzaji maziwa, tbs ubora na tfda usalama na taasisi au vyama wadau hutokea Sido. Ina maana hii michanganuo yako utaipeleka SIDO wao wana wataalamu watakupa ushauri wa andiko lako, muundo wa kiwanda na vilevile utaalam elekezi. Kwa uzoefu wetu kozi hizi hazina muda maalum na huwa zinakuwa za kukuboresha zaidi na kukupa cheti, hivyo jitahidi kupita kwa wadau wajuzi au kuajili watu wajuzi waliosomea food processing. Hii ina maana katika kupeleka barua mfano tfda ina mana barua inakuwa ya utambulisho inatoka sido baada ya wewe kuwaandikia barua ya kuomba utambulisho tfda au tbs nk!
Tusiogope kuwa tfda labda wasumbufu si kweli kwa sababu umeruka vipengele hivi vya mwanzo. Tfda watakujibu na watakuja wataalam wao kuangalia eneo lako la kiwanda na mpangilio wako umekaaje wa mashine za uzalishaje nk. Lakini tambua mwanzo tayari ulishapata kutembelewa na Sido hivyo hata kma marekebisho yatakuwepo yatakuwa kwa kiwango kidogo.
Suala la kibali toka Tbs ni kweli hupatikana baada ya kuanza kuzalisha bidhaa yako kwani huchukua sample kwa ajili ya kuipima kujua ubora wa bidhaa hiyo. Na tena kwa sasa kama mjasiriamali mdogo ni buree kupata tbs ya bidhaa yako
bf67253bf4fb26ef188e48a420d8a2fa.jpg

Kwa maelezo zaidi tafuta wataalam washauri wa kibiashara walio jirani nawe au karibu i-business consult. Maoni au ushauri email:iconsultbuzness@gmail.com, hotmail 0659211222
 
Mimi ninavyo jua TFDA au TBS hutoa kibali kwa bidhaa ambayo tiyari imeisha anza kazi, TBS hawawezi kukupa kibali halafu ndo ukaanze kutafuta mitambo even TFDA kwa sababu wanakuja kukagua production yako ndo wakupe kibali, so chakufanya hata ukiwaona watakupatia mwongozo tu na wewe utaanza kazi n then watakuja kukagua kuona kama unafuata mashariti yao ndo sasa upewe kibali rasimi au la.

Huwezi pewa kibali kabla hujaanza productions na TBS hivyo hivyo ni lazima uanze kwanza ndo waje kukagua na wana tabia ya kufanya ukaguzi wa kushitukiza utashangaa gari inafunga break mlangoni kwako, so unatakiwa kuhakikisha walio kuambia unayafuata yote.
TFDA wanakagua pia hatua za awali
 
Wazo zuri na Hongera sana, ushauri wangu unahitaji upate roadmap na njia pekee ni kutengeneza business plan mkuu wangu. I can volunteer to guide you and any one who need to come with such kind of projects. Thanks
Mkuu habari. Niko kibaha nahitaji huduma ya Mpangara biashara naanzisha usindikaji wa maziwa
 
Back
Top Bottom