Msaada: Kozi ya ‘Biotechnology and Bioinformatics’ inahusiana na nini?

Zero Conscious

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2022
Posts
254
Reaction score
519
Habari za muda huu tena wakuu.

Naomba msaada na ufafanuzi juu ya Kozi hii inahusika na mambo Gani?

BACHELOR OF SCIENCE IN BIOTECHNOLOGY AND BIOINFORMATICS

Natanguliza Shukrani
 
Habari za muda huu tena wakuu. Naomba msaada na ufafanuzi juu ya Kozi hii inahusika na mambo Gani?

BACHELOR OF SCIENCE IN BIOTECHNOLOGY AND BIOINFORMATICS

Natanguliza Shukrani
Biotechnology is the use of biology to solve problems and make useful products. The most prominent approach used is genetic engineering, which enables scientists to tailor an organism's DNA at will.

Bioinformatics, as related to genetics and genomics, is a scientific subdiscipline that involves using computer technology to collect, store, analyze and disseminate biological data and information, such as DNA and amino acid sequences or annotations about those sequences
 
B.Sc. in Biotechnology and Bioinformatics ni programme mpya pale UDOM ambayo imechukua intake ya kwanza mwaka (2021).

SUA na UDSM pia wanazo programme zinazofanana na hiyo: B.Sc. in Biotechnology and Laboratory Sciences (SUA) na B.Sc. in Molecular Biology and Biotechnology (UDSM). Chuo cha DIT kinatoa Diploma ya Biotechnology.

Mtazamo wangu:

1. Kwa kuangalia trend ya hizi programme mbili za UDSM na SUA hapa Tanzania, Biotechnology ni programme nzuri. Programme hizi zinakupa knowledge na skills zitakazokuwezesha kufanya manipulation ya biological processes mbalimbali katika viumbe hai vidogo kama vile bacteria, virus na fungi ili kutengeneza products ambazo zina manufaa kwa viumbe hai, au kutibu magonjwa mbalimbali, n.k

Kwa lugha nyepesi...huku utajifunza kiundani yale mambo ya Genetic engineering uliyojifunza Advance School kwenye biology. Pia utapata maarifa mtambuka (general knowledge) ya sayansi nyinginezo zinazohusiana na Biotechnology. Kwa lugha nyingine hawa watu wanaitwa "wataalamu wa sayansi za vinasaba".

2. Programme hizi zitakupa ujuzi wa kukusaidia kufanya kazi kwenye taasisi, miradi na mashirika mbalimbali ya tafiti za afya ya binadamu, mifugo, mimea na hata zile zinazohusu viumbe waishio kwenye maji. Kwa Tanzania, baadhi ya sehemu hizo ni kama: IHI, KCRI, NIMR, MITU, TARI, TAWIRI, MDH, ICAP, GCLA, na mengineyo.

Pia ujuzi wa biotechnology unaweza kukusaidia kufanya kazi kwenye viwanda vya chanjo kama vile Hester Biosciences na TVI kwa hapa Bongo. Pia unaweza kupata ujuzi utakaokusaidia kwenda kufanya kazi za udhibiti ubora kwenye sehemu kama vile TBS, TMDA pamoja na viwanda vya vyakula, vinywaji, n.k. Vilevile unaweza kuwa mhadhiri kwenye vyuo vikuu kwa masomo kama: Biochemistry and Molecular Biology, Microbiology, Immunology, Parasitology, n.k

Hizo ni baadhi baadhi ya sehemu maarufu unazoweza kufanya kazi. Pia zipo sehemu nyingine nyingi ambazo sijazitaja.

3. Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba teknolojia hii ni kubwa na kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania matumizi ya teknolojia hii ni madogo kutokana na sababu za kiuchumi kwakuwa kufanya shughuli zinazohusu Biotechnology inahitaji gharama kubwa. Hivyo basi graduates wa programme ya Biotechnology na zinazofanana na hizo wanajikuta wanajaa mtaani kwa kukosa ajira zilizo rasmi.
Kujiajiri katika fani hii inawezekana ila kuna changamoto zake ikiwemo uhitaji wa mitaji mikubwa.
Ila issue ya tatizo la ajira kwa nchi zetu ni tatizo kwa fani nyingi na sio Biotechnology pekee.

Kutokana na ukweli wa kwamba Biotechnology inahusisha masomo mengi ambayo yanahusiana na afya ya binadamu basi graduates wa programme hii wamekuwa wakipambana kutafuta nafasi za kufanya kazi katika hospitali mbalimbali kwakuwa sehemu zinazofanya shughuli za Biotechnology sio nyingi hapa Tanzania ukilinganisha na idadi ya wahitimu. Hili ni tatizo kwakuwa wataalamu hawa wa biotechnology ni kweli wanaweza kufanya kazi za maabara za hospitali lakini hawaruhusiwi kisheria kufanya kazi hiyo.

4. Dunia kwa sasa inakabiliwa na majanga makubwa kama vile COVID-19 na Monkey Pox Virus, climate change, n.k ambayo yanaweza kutatuliwa kiurahisi kwa kutumia utaalamu wa biotechnology. Hivyo basi tunategemea siku za mbeleni nchi zetu zitaona umuhimu wa kuweka nguvu kwenye fani hii na basi sehemu za kufanya ujuzi huu zitaongezeka na tatizo la ajira kwa wataalamu wa biotechnology litapungua (haliwezi kuisha).

5. UDOM wameongeza component moja ya tofauti na UDSM na SUA kwenye programme ya Biotechnology iitwayo "Bioinformatics". Bioinformatics inahusisha matumizi ya biology, statistics na computer science katika kuchakata data mbalimbali zitokazo maabara zinazohusiana na vinasaba. Bioinformatics ni part nzuri ya Biotechnology na wataalamu wa Bioinformatics ni wachache hapa nchini. Uhitaji wake kwa sasa unaweza usiwe mkubwa sana hapa nchini lakini tunatarajia siku za mbeleni uhitaji utakuwa mkubwa hapa nchini na duniani kote.
Curriculum za Biotechnology kwa SUA na UDSM zinayo component ya Bioinformatics lakini curriculum ya UDOM imeenda ndani zaidi kwenye issues za Bioinformatics hivyo basi tunatarajia wahitimu wa UDOM kuwa na ujuzi zaidi kwenye Bioinformatics kuliko hawa wa UDSM na SUA. Ila ili uweze kuielewa Bioinformatics vizuri anza kujenga mapenzi na maswala ya programming kwenye computer, hesabu kidogo especially eneo la statistics na biology kwa sana.

SUMMARY:
Biotechnology na Bioinformatics ni choice nzuri kama una malengo ya kuja kuwa researcher/mtafiti kwenye maswala ya vinasaba vya binadamu, wanyama, mimea na viumbe wengine. Swala la ajira ni changamoto kidogo kwenye Biotechnology lakini hata fani nyingine kama udaktari zina changamoto hiyo kwa sasa.
Kama mtu ataamua kuingia kwenye fani hiyo basi asome kwa bidii ili kupata ujuzi vizuri. Kufaulu vizuri na kuwa na cheti kizuri ni muhimu kwenye issues za competition. Kujiongeza kwa kutafuta connections za watu ambao wapo kwenye fani hii kwa muda mrefu ni jambo la busara pia. Na pia kumtanguliza Mungu katika safari yako ya fani ya Biotechnology ni muhimu zaidi. Ukizingatia hayo basi Biotechnology itakupeleka sehemu nzuri sana kimaisha.

#PASSION IS KEY

~ Biotechnologist
 
Tunashukuru
 
Back
Top Bottom