LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 578
Nikisema nianike kila kitu hapa jamvi ni dogo, nawashukuru sana wote mlionipa ushauri na wengine kunitukana na kuniita MALAYA, hadi nimejianika hapa juwen kuna tatizo. Hamumjui mume wangu yukoje na y niliingia huko kwenye uhusiano nikiwa ndani ya ndoa. Hakuna ajuaye alinifanya nini hadi nikatoka nje. Alichokifanya hakielezeki. Na huko kutiwa mara 3 sio kila siku. Kuna walioshangaa nimwambie dr nishindwe kumwambia ndugu , hospital ningepataje msaada bila kusema ukweli??? Mmenishambulia sana ila nimepata pa kuanzia. Hata mliofuta pole kwangu nawashukuru pia . Mimi si malaika nna mapungufu pia. Niliowakwaza kwa kuomba ushauri jf mnisamehe.
Ushauri wangu dada, kuwa wewe, unapokuwa hapa jamvini usiweke jambo kwa kufurahisha tu,
Hata kama una malengo hayo , bora uoneshe mapema tu, kwamba hili jambo nimweka kuchangamsha jukwaa.
Lakini leo unaongelea mchumba, kesho boyfriend, kesho kutwa mume na ndoa, watu watasindwa kukuelewa kabisaaaaaaaaa!!!!!
Na utakosa ushauri kwa sababu hiyo.
Hata hivo, unaye Mungu aliyekuumba kwa sura na mfano wake,
Yupo Mungu anayekupenda kuliko kitu/mtu yeyote hapa duniani,
Yawezekana ni kweli akili yako imefika mwisho wala hujui ufanye nini kuhusu hilo.
Lakini, pia Mungu hapendi wewe uteseke, tena uteswe na kiumbe ambacho na chenyewe kinaishi kwa neema ya Mungu.
Mi sipo kwenye ndoa, labda linaweza kunifanya nisielewe vizuri namna ya kukushauri, lakini yupo Mungu ambaye anatuwazia mawazo ya amani. Muombe Mungu, chukua ushauri wa watu, ule unaoona utakufaa, ufanyie kazi, na utafanikio.
Ninakuombea furaha, na amani ya moyo wako. Mungu akupiganie katika mapito yote hayo unayopitia, hatimae uwe mshindi.
Barikiwa.